Kumekuwepo na kasumba vijana wengi kuwaogopa wanawake wenye mafanikio ya kipato au kielimu, mathalani ni nadra sana kijana ambaye hana elimu kubwa kutaka kumuoa binti wa Mwenye elimu, hivyo hivyo wanawake wenye kipato wanaogopwa sana wanaume wenye vipato vya chini, wengi huogopa kutongoza wakisubiri zali la mentali.
Maisha hayako hivyo usimuogope mwanamke aliyesoma au mwenye ikitokea umempenda mwambie na akikubali tumia fursa hiyo kufikia malengo yako na hata kumzidi.
Niwape ushuhuda kidogo kipindi namchumbia mke wangu nilikuwa na elimu ya kidato cha nne na mke wangu alikuwa na shahada ya kwanza akiendelea na shahada ya pili nilimueleza ukweli akanielewa ugumu ukawa kwa wazazi wake na wangu wakati mwingine ilinilazimu nidanganye kuepusha aibu, Lakini baada ya kuoana nilijawa na uchungu wa mafanikio nikasomaa kwa bidii lengo likiwa tulingane elimu nikafanikiwa kwa hilo hivi hivi tupo droo zile aibu za kwamba wewe msomi unaolewaje na mtu ambaye hajasoma zimeisha. Ikumbukwe kwamba kabla ya kumuoa pamoja na kuwa na ufaulu mzuri wa kidato cha nne sikuwa na mpango wa kusoma kupitia yeye nimepata elimu ambayo inanisaidia.
Hivyo basi kupitia mafanikio ya mwenza wako yanaweza kukufanya ukafikia malengo yako kwa kukuinspire, mara nyingi jamii itakuvunja moyo mara "unaoaje mwanamke msomi atakusumbua" usiwakilize bali tumia changamoto hiyo kufikia malengo yako..
Nimeleta mada hii kwa sababu leo kuna binti amehitimu chuo kikuu alikuwa na mpenzi toka sekondari amemkataa eti kisa kasoma.