Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,497
- 119,432
Kuna mtu anayeifuatilia [angalia] hii documentary inayoonyeshwa na ESPN?
Ina sehemu tano. Sehemu ya kwanza ilionyeshwa Jumamosi iliyopita kwenye chaneli ya ABC na sehemu ya pili inaonyeshwa leo kwenye chaneli ya ESPN.
Ni documentary inayohusu kesi ya mauaji ya watu wawili, Ronald Goldman na Nicole-Brown Simpson [mke wa zamani wa O.J.] waliouwawa kikatili huko Brentwood, kiunga cha jiji la Los Angeles, Marekani.
People of the State of California v. Orenthal James Simpson - ndo lilikuwa jina rasmi la kesi hiyo iliyoendeshwa katika mahakama ya county ya Los Angeles.
Hii kesi ilibatizwa jina la 'kesi ya karne' kutokana na mvuto iliyokuwa nao kwa Wamarekani na hata nje ya Marekani.
Katika kesi zote ambazo nimewahi kufuatilia, iwe kwa ajili ya kikazi au raghba tu, nadhani hii ndo iko juu kuliko zote.
Kwa anayetaka kujua zaidi kuhusu hiyo kesi basi na afuatilie hiyo documentary.