Nywila(password) kwenye simu yako inaweza kukukosesha msaada wa haraka

bartaizo

JF-Expert Member
Jun 19, 2013
236
86
Watu watatu walipata ajali ya gari na hawakujitambua kabisa. Raia mwema akatokea sehem ya ajali na akataka kupiga simu kwa msaada. Bahati mbaya hakuwa na simu.

Kwenye ajali kulikuwa na simu 6 lakini zote zilikuwa na PASSWORD. Mwisho wake wakakosa msaada wa kuwahishwa hospitali na hatimaye wakafariki wote.
.
.
Mama Mjamzito alianguka ghafla nyumbani kwake akiwa na mwanae mdogo wa kike. Alivyoona mama yake anagugumia maumivu huku hajitambui, alichukua simu ya mama yake ili ampgie baba yake kwa msaada zaidi. Kwa bahati mbaya simu ilikuwa na PASSWORD. Akachelewa kuwahi kupata huduma na mwisho akapoteza maisha.

Nani mwenye makosa?

USHAURI

Wewe una thamani sana kuliko taarifa unazoziwekea usalama katika simu.

Weka PASSWORD katika WhatsApp, Facebook, Message, Gallery n.k

Acha upande wa Phonebook na Calls bila PASSWORD, siku moja yawezekana ukaokoa maisha yako au ya wapendwa wako.

PASSWORD katika simu yako yaweza pelekea umauti wako.

Fikiria mara mbili.
 
Hawa itakuwa wanaishi kisiwan hata majiran hawana mpka baba apigiwe simu aisee........
 
Umeongea pointi mkuu,ila fahamu pia hiyo iko mara 2 waweza kupata mauti au kuokoa taarifa zako muhimu zilizoko kwenye simu hasa upande wa phonebook.(maana wengine tumeifadhi baadhi ya no za siri za huduma fulani)
 
Kuweka maneno siri kwenye simu ni dalili kuwa unayoyafanya ni maovu. Hakuna lingine

Kama ni mtoto eti atachezea simu basi weka lock ya kawaida.
 
Watu watatu walipata ajali ya gari na hawakujitambua kabisa. Raia mwema akatokea sehem ya ajali na akataka kupiga simu kwa msaada. Bahati mbaya hakuwa na simu.

Kwenye ajali kulikuwa na simu 6 lakini zote zilikuwa na PASSWORD. Mwisho wake wakakosa msaada wa kuwahishwa hospitali na hatimaye wakafariki wote.
.
.
Mama Mjamzito alianguka ghafla nyumbani kwake akiwa na mwanae mdogo wa kike. Alivyoona mama yake anagugumia maumivu huku hajitambui, alichukua simu ya mama yake ili ampgie baba yake kwa msaada zaidi. Kwa bahati mbaya simu ilikuwa na PASSWORD. Akachelewa kuwahi kupata huduma na mwisho akapoteza maisha.

Nani mwenye makosa?

USHAURI

Wewe una thamani sana kuliko taarifa unazoziwekea usalama katika simu.

Weka PASSWORD katika WhatsApp, Facebook, Message, Gallery n.k

Acha upande wa Phonebook na Calls bila PASSWORD, siku moja yawezekana ukaokoa maisha yako au ya wapendwa wako.

PASSWORD katika simu yako yaweza pelekea umauti wako.

Fikiria mara mbili.
Katika vitu ambavyo vimenishinda ni pamoja na kuweka password na patterns kwenye simu, wala sioni kitu cha maana cha kukificha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true...mi pia ilishanitokea kwa ndugu yangu bahati nzuri namimi nilikua ndio nimefika hospital nikakuta wauguzi wanahaha namna ya kufanya mawasiliano na ndugu wa mgonjwa huku wameshika simu ya mgonjwa hawajui wafanyaje.. Kama Mungu tu aliniongoza kwenda hospitali mda ule aisee
 
Simu yangu lazima iwe na password, email yangu ipo wazi na ina mambo ya muhimu mno

Uwezekano wa wewe utapata ajali ni mdogo kuliko wa kupoteza simu yako kisha ikapekuliwa na info muhimu kuchukuliwa au kutumika kutapeli

Pia hata ukipata ajali wanaweza kutoa line na kuweka simu nyingine na kuona majina

simu yako weka password, muhimu tembea na kitambulisho ukipata ajali watakutambua
 
Mkuu ni kweli hili lilitokea mwezi uliopita wa 6 nipo kwenye daladala kuna sister du alidondoka na kupoteza fahamu,Watu wakachukua simu yake wawapigie ndugu zake kuulizia kujua kama ana tatizo la kuzimia tukakuta cm ina password tulichoamua ikabidi tumwambie dereva apige uturn kwenda hospitali ya karibu tukamuacha wanampa huduma ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom