Nyusi ameshinda uchaguzi wa Urais nchini Msumbiji

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,349
Tume ya uchaguzi ya Msumbiji imemtangaza Rais Filipe Nyusi kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais kwa asilimia 73 ya kura na chama chake cha FRELIMO kitakuwa na asilimia 74 ya viti vya Bunge, Chama Kikuu cha Upinzani cha RENAMO kimeyakataa matokeo hayo, kikidai uchaguzi ulikuwa umegubikwa na udanganyifu na vitisho.
_
Tume pia imemtangaza mgombea wa RENAMO, Ossufo Momade kuwa amepata asilimia 22 ya kura zilizopigwa, katika Bunge lenye viti 250, FRELIMO kimepata viti 184, RENAMO 60 na Chama cha MDM viti 6, RENAMO hawajapata hata kiti kimoja katika chaguzi za majimbo, ambapo Magavana wamechaguliwa moja kwa moja kwa mara ya kwanza.

 
Nyusi kaamua kuwanyoosha wapinzani,yaani hata kwenye uchaguzi wa majimbo hawajapata hata jimbo moja😂😂😂,uchaguzi ulikuwa na miyeyusho mingi mpaka basi,Renamo mpaka kwenye ngome zake kashindwa kuchukua jimbo,ilihali wao ndio walipendekeza magava nao wachaguliwe sio wateuliwe na Rais,kuna mwanamuziki aitwaye Refiller boy ambaye aligombania ugavana jimbo la Gaza na chama chake cha Nova Democrácia,huyu ndio alifanyiwa figisu mpaka namuonea huruma jinsi anavyolalamika😂😂😂
Nalog off
 
Ndiyo chaguzi za Afrika, Kenya enzi za Moi marehemu wengi sana walimpigia kura, ni mpaka yeye mwenyewe aliporidhia kuondoka madarakani lakini hakuondolewa kwa sandukuwla kura.
 
Ndiyo chaguzi za Afrika, Kenya enzi za Moi marehemu wengi sana walimpigia kura, ni mpaka yeye mwenyewe aliporidhia kuondoka madarakani lakini hakuondolewa kwa sandukuwla kura.
Ujue unapoiga jambo ni lazima utalizidisha au utalipunguza,yaani kama Frelimo wamejifunza kufanya figisu kutoka CCM basi naweza amini wamewapita.
Mwaka 2017 ilifanyika sensa ya Taifa kuna jimbo linaitwa Gaza hii ndio ngome ya Frelimo,Frelimo kupitia Tume ya uchaguzi ikaongeza idadi ya wapiga kura ili kupata wabunge wengi zaidi,hawa watu wa sensa wakaikataa idadi ya tume ya uchaguzi kwa kusema idadi hiyo itapatikana kuanzia 2040 kwa kuwa wakazi wengi wana umri chini ya miaka 18,hii yule mwenyekiti wa sensa akajiuzulu kwa kuipinga idadi hii ya tume ya Taifa ya uchaguzi na msaidizi wake akauliwa wakati wa kampeni.
Na hapa ndipo wapinzani walipokosea kwa kuamua kwenda kwenye uchaguzi wakati figisu wameziona live bila chenga na hapo ndipo kukatokea tena kutoaminiana wanachama ndani ya Renamo,wapo waliomuona Ossufo Momade ni msaliti na kitengo cha askari wa Renamo kikiongozwa na Mariano Nhongo kuasi na kutomtambua kiongozi wao.

Hii nayo inataka kutokea Tanzania ambapo Rais kashatangaza kuwa wapinzani wasitangazwe washindi,sasa sijui wanashiriki uchaguzi wa kazi gani😇
Nchini Msumbiji uchaguzi wa wabunge,huwa kinachaguliwa chama na sio mtu,yaani iko hivi mtagombania wenyewe ndani ya chama chenu na atakayepata kura nyingi ndiye atakuwa mbunge (mfano: ccm ndani ya chama wanaogombania jimbo la Ubungo na matokeo ni hivi
1.Edward Simjui 1000
2.Filomena Ndimu 880
3.Abdala Miyeyusho 610

Cuf nao wakafanya uchaguzi wao wa ndani na mshindi namba
1.John Tindo 1000
2.James Fungo 879
3.Mwanaidi Nyau 617

Chadema wakafanya uchaguzi wao wa ndani na washindi wakawa hivi
1.Eliza Shayo 1000
2.Kasim Mwanakwetu 86
3.Asha Ndalandefu 69

Tuchukulie ccm ndio kashinda kwenye jimbo la Ubungo ina maana Edward Simjui ndiye anakuwa mbunge na ikitokea kwa namna yoyote akaacha kuwa mbunge basi ina maana namba 2 bi Filomena Ndimu ndiye atakayechukua nafasi yake,hapa hata mbunge akiamua kuunga mkono juhudi basi chama hakipotezi mbunge wala diwani kwa kuwa uchaguzi hautorudiwa.
Uchaguzi pekee utakaorudiwa ni Rais au meya. Meya atakapoacha umeya kwasababu yoyote ile mtu kutoka chama chake ndiye atakayekaimu nafasi na baadae kutajwa tena kwa siku uchaguzi,style yao ni nzuri kwenye kupunguza pesa za kufanya uchaguzi wa marudio,hawataki kusikia mara mtu kupita bila kupingwa na figisu nyenginezo.
Nalog off
 
Kweli jamaa wamekua wachumba tu sa hivi,wanaamini kabisa box la kura litawapa ushindi.
Wanarudije porini wakati Djakama hayupo tena duniani? Baada ya jakama kufa jamaa wa renamo wamepoa sana
 
Afu napenda RENAMO wanyooshwe kisawasawa maana wao hua hawampendi Mtanzania na hawana huruma na Mtanzania kwani wanaamini FRELIMO wanapata support kutoka Tanzania
 
Hivo naona leo ni shangwe tu na mikate leo italiwa sana wasalimieni nanyupu, mweda, lichinga
 
Afu napenda RENAMO wanyooshwe kisawasawa maana wao hua hawampendi Mtanzania na hawana huruma na Mtanzania kwani wanaamini FRELIMO wanapata support kutoka Tanzania
Renamo kuja kukaa sawa itachukua muda,sasa hivi wanacheka jino pembeni,tendo la uongozi wa chama kutoka kabila la Ndau na kwenda kwa wamacua kinawaumiza mandau wengi ambao wanapendelea waendelee kuongoza hasa kaka wa Dhlakama na mpwa wake Yvone Soares wanataka wawepo madarakani,kwahiyo wanatumia ukabila uliowanufaisha wao kwa kumuharibia Ossufo Momade na kumwita pandikizi la Frelimo ndani ya Renamo,njia alizokuwa akizitumia kiuongozi ndizo anazotumia Ossufo kwa kuweka watu wake anaowaamini watafanya naye kazi kwa maelewano.
swali la kizushi: je ? Wabunge wa Renamo wataenda kuapa au wataendelea kutoyatambua matokeo😂😂😂
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…