Nyumba za kupanga jijini Dar, Jipu linalohitaji kutumbuliwa

Zeyn

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
344
180
Katika jiji hili lenye pilikapilika nyingi na idadi kubwa ya watu nyumba za kupanga zimekua ni tatizo kubwa.

Ni uonevu kumpangishia mtu chumba kwa miezi 12 yaani mwaka mzima, Imekua ni tabia sugu sasa kwani popote utakapotafuta chumba utaambiwa bei ni kiasi fulani kodi ya miezi 12 mpangaji akishuka sana ni miezi 10.

Hii inasababisha hata huduma katika nyumba hizi za kupanga kua mbovu,mfano marekebisho muhimu katika nyumba n.k

Ikiwa mtu amepanga kwa miezi mitatu na kukawa na tatizo fulani katika nyumba hiyo ambalo linachukua muda kushughulikiwa mtu anaweza kuacha hata muda uliobakia ikiwa ni mwezi au miezi miwili katika mkataba wake na kutafuta sehemu bora zaidi kwake.

Lakini iwapo umepangishiwa kwa mkataba wa miezi 12 na ndani ya mwezi matatizo kama hayo yamejitokeza unaweza kuacha miezi 11 iliyobakia ama baada ya miezi mitatu tatizo halishughulikiwi ama kuna matatizo mengine yanayokusababisha usitake kuendelea kuishi hapo je utaweza kuacha miezi 9 iliyobakia.

Hili ni tatizo na kwa ushauri wangu/ombi langu na malalamiko mengi niliyoyakuta mitaani mamlaka husika ziingilie kati suala hili.angalau miezi maximum ya kumpangishia mtu iwe ni miezi 6.

Muwe na siku njema.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kweli kabsa hili ni tatizo...ila tuchukue kama changamoto tuwezi kuishi kwenye nyumba zetu. NHC ndo ilikuwa iwe mkombozi lakini imeshindikana.
 
Suruhisho kama wadau walivyo comment hapo juu NHC ndo ilikuwa ufumbuzi wa tatizo matokeo yake imekuwa kinyume.
Huwa nashangaa sehemu kama pale mchikichini kuna vijumbajumba vingi vidogo uwanja mkubwa why japo waliwauzia wale watu kwanini wasizungumze nao kisha vikapigwa nyundo unamjengea mtu ki apartment kama nyumba yake ilivyokuwa nyingine inabaki kuwa mali ya NHC.
 
Kuna kipindi fulani Mh January Makamba alisema analivalia njuga hili swala la nyumba za kupanga dar, sijui alilifikisha wapi huyu mheshimiwa. Nyumba za kupanga dar ni uwanja mgumu unaoendeshwa na madalali na wapo wanaosema dar bila madalali haiwezekani.
 
Kabla ya kuanza kuwashika mashati private sector, wabane kwanza National Housing Corporation kampuni iliyoanzishwa kuwahudumia wananchi wasiojiweza kupata makazi matokeo yake nao wanafanya biashara..

Biashara Huria ukianza kumpangia mtu mwenye mali yake siku akiacha kutoa huduma pindi uharibifu unapotokea usilalamike.., na kama wewe unataka kutoa kodi kwa mwezi na wapo watu kumi wanaohitaji hio huduma na wanao uwezo wa kutoa kwa mwaka unategemea nini kitatokea
 
Alafu kuna na hii tabia ya kuropoka bei!! Yaani unakuta nyumba ni ya kawaida sana ila mtu anakutajia bei kuuubwa utadhani anakupangishia meli au Ghorofa.
Nadhani ni muda muafaka wa serikali kujua kuna nyumba ngapi za kupangishwa nzima nzima na ni ngapi wana pangisha chumba na sebule au chumba pekee na wenye nyumba wawe registerd katika manispaa. Alafu madalali wawe pia registered. Kisha serikali iweke bei elekezi kwa kila mtaa na kwa square mita au square futi.
Hii itaongezea serikali/manispaa mapato na pia itaondoa usumbufu wanao pata wananchi. Na hata NHC wanaweza kuweka mipango yao sawa kwa kujua ni wapi kuna shida ya nyumba.
 
Tunajenga uchumi wa aina gani mpaka serikali iingilie maisha yetu karibu katika kila jambo? Private sector haiwezi kujiendesha yenyewe japo kidogo kwa kutegemea supply and demand? Serikali imeingilia shule private, sasa iingilie hata nyumba za watu waliojenga wenyewe kwa pesa zao? Kuna nchi yo yote ina/li-yoendelea inayofanya hivi? Kazi ya serikali ni kujenga mfumo imara wa kiuchumi utakaowezesha wananchi wengi kuwa na kipato cha kati (middle class). Hili likifanyika matatizo kama haya yatajilainisha yenyewe tu. Serikali kujitandaza kila sehemu ni udhaifu na ni kufungua mianya mipya ya rushwa na ukiritimba. Kuna mambo mengine serikali siyo suluhisho bali ni chanzo cha matatizo.
 
Hakuna nchi ambayo ilipiga hatua kwa kuangalia low ya Demand and Supply ina taja bei gani. Nchi zoote za ulaya zilianza na Protectionism na pia serikali ikajenga nyumba nyingi sana za makazi ya raia wake na baadae ndio waka waachia private sector. Sasa kwa hizi serikali zetu dhaifu zina hitaji kujenga strong base kwanza kabla ya kuenda full kwenye market economy. Jiulize, China, Singapore na other Asian tigers walipitia njia gani hadi wakafika hapo walipo.
 
Sure, NHC eti nyumba za gharama nafuu ni sh m 60 kianzio milioni kumi,
Na serikali ije na mpango wa kukusanya Kodi ya VAT kwa wenye nyumba kwani tunawalipa hela nyingi Sana kwa mwaka. Waziri wa fedha hili lianze julai MOSI badala ya kuongeza being za soda kusanya kwenye nyumba za kupanga.
 
Si bora miez 12,,hiyo kodi sasa mmmmmmh chumba kimoja kizur elf70,60,50, hapo mwez1 unampa na dalali pesa yake
 
Yeni hilo ndio jipu lililoiva kabisa linalosubiri kutumbuliwa,CIO muda tuu pia hats mamlaka husika ziangalie kodi ambazo watu wanatozwa ni kubwa sana
 
Kuna kipindi fulani Mh January Makamba alisema analivalia njuga hili swala la nyumba za kupanga dar, sijui alilifikisha wapi huyu mheshimiwa. Nyumba za kupanga dar ni uwanja mgumu unaoendeshwa na madalali na wapo wanaosema dar bila madalali haiwezekani.
Hivi kwa mfano mkuu..hivi bila dalali unawezaje kupanga au kupangisha?
 
NHC ingekuwa na nyumba nyingi za kupangisha kama URAFIKI kusingekuwa na bei za ajabu ajabu
 
Kuna kipindi fulani Mh January Makamba alisema analivalia njuga hili swala la nyumba za kupanga dar, sijui alilifikisha wapi huyu mheshimiwa. Nyumba za kupanga dar ni uwanja mgumu unaoendeshwa na madalali na wapo wanaosema dar bila madalali haiwezekani.
Mwandishi wa siku nyingi wa gazeti la Mwananchi Bwana Richard Mabala kwenye ukurasa wake wa Makengeza huwaita waheshimiwa eti waishiwa
 
Back
Top Bottom