Nyumba ya Tigo

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Jamani mimi naipenda ile nyumba inayoonekana kwenye tangazo la Sajili na Ushinde la Tigo. Kuna mtu mwenye picha inayoonekana vizuri ya nyumba ile au amabaye anafahamu naweza pata wapi ramani yake?
 
huyo jamaa walitajadau la milioni 4 naweza kumuhusisha na ccm...pesaa mbele!!! kama ni picha ambassador najaribu kutafuta...free of charge
 
Bomba sana nyumba ile.....lakini kama mchoro to ni 4m/= tutashindwa kuijenga....pale Kijitonyama nyuma ya sayansi kama unaelekea BoT flats kabla ya Hotel ipo nyumba hii...sijui mwenyewe ni nani
 
Du nyumba hii tamu sana, kumbe wengi tunaitamani!!! Kuchora ramani kweli gharama, lakini kama mtu anayo na aliipata bure kuna haja gani ya kuwauzia wabongo wahangaikaji wenzako! TAMAA, WABONGO KILA KITU DILI!!! Mwenye nayo jamani aiweke hapa, nani alitengeneza hilo tangazo? lazima atakuwa nayo picha, na anajua nani alileta- huyo ndiye mwenye floor plan, maana bila floor plan picha haina maana.
 
huyo jamaa walitajadau la milioni 4 naweza kumuhusisha na ccm...pesaa mbele!!! kama ni picha ambassador najaribu kutafuta...free of charge

mkuu ambassador hatafuti picha ya nje..! anataka kutumia picha ya nje na utengeneza ramani ya ndani bila kubadili muonekano wa nje.

tena 4M ni msaada tu kwa kuwa ni mwana jamvi.
 
mkuu kama upo serious hiyo kitu unapata na wala sitaki hata senti mpaka uridhike na kazi....!!!! wewe tu!
 
Kwa nini kupata tabu, wapo wachoraji mahiri hapa mjini, tena kwa bei nzuri na kitu kinatoka kuliko hicho cha tigo. Kweli ile picha inavutia sana, na nimeipenda sana! Tena siku hizi actectures wapo wengi wazuri mno, vijana mjini toka chuo cha ardhi wako very innovative, wanacheza na computer wanakutolea standard mchoro kwa muda mfupi sana, si kama zamani basi mchoraji unazunguka naye mchoro tu miezi!
 
Niliacha mambo ya kuchora uchoraji michoro enzi hizo baada ya kuhisi kibiongo kinaanza kunitoka kwa kukaa muda mrefu kwenye stuli na drawing board,lakini loh siku hizi kama unapiga picha vile kwenye digital camera,hakika dunia imebadilika
 
mkuu ambassador hatafuti picha ya nje..! anataka kutumia picha ya nje na utengeneza ramani ya ndani bila kubadili muonekano wa nje.

tena 4M ni msaada tu kwa kuwa ni mwana jamvi.

mkuu kama upo serious hiyo kitu unapata na wala sitaki hata senti mpaka uridhike na kazi....!!!! wewe tu!
Niko serious sana, na kama ulisoma mawazo yangu vile. Nahitaji kwa nje itoke vile vile ingawa kwa ndani tunaweza cheza nayo na huyo archtecture. Kama unayo please help!
 
Niko serious sana, na kama ulisoma mawazo yangu vile. Nahitaji kwa nje itoke vile vile ingawa kwa ndani tunaweza cheza nayo na huyo archtecture. Kama unayo please help!

poa mkuu ..! kama unayo hiyo picha naiomba ili kazi ianze mara moja...!
 
huo mnaotaka kuufanya ni wizi .............

namshangaa mtu anasema ati mmoja anao mchoro awape na wenziwe................sasa anatarajia architects wale wapi?

nchi haiwezi kuendelea kama hatujaheshimu professions za kila mtu
 
mkuu sio wizi ...manake kazi itafanya na architect pia...!
 
Ethics za architects zinakataza ku copy kwa aina yoyote ile kazi ya mwenzio bila ya kuwasiliana na original creator wa hiyo kazi..........wewe unalengo la kumtafuta?
 
Ethics za architects zinakataza ku copy kwa aina yoyote ile kazi ya mwenzio bila ya kuwasiliana na original creator wa hiyo kazi..........wewe unalengo la kumtafuta?

hakuna mtu anaekopi kwa sababu hakuna ramani...! tunatumia picha to come up with the internal arrangement of rooms..! u cant call this copying..! afterall the plans wont b the same..!
 
Ethics za architects zinakataza ku copy kwa aina yoyote ile kazi ya mwenzio bila ya kuwasiliana na original creator wa hiyo kazi..........wewe unalengo la kumtafuta?

Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia zote!
Lakini naona kwenye computer yako umejaza pirated PDF copies za vitabu vya watu! simu yako imejaa milio ya bongofleva na gospel za wasanii wanaoishi nyumba za kupanga! Hata hiyo Laptop unayotumia umeweka Window7 ya wizi!
Kwa mazingira ya sisi hohehahe, ukiona karamani ukakapenda, kukakopi na kukamodifai ni akseptabo japo ni iligo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom