Nyumba ndogo (shairi)

Nyumba ndogo (shairi)

Joined
Jan 4, 2012
Posts
61
Reaction score
23
1. Nyumba ndogo si fahari,si pendo ulimbukaji,
Pendo lisilo Nadhari, Daima unyatiaji,
Mara nyingi in kaburi, la kufukia mitaji,
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.
2. Sababu ya nyumba ndogo, Sisaliti Ndoa yangu,
Make simpi kisogo, nikenda jivisha pingu,
Katu Siwanii kago, kwa mwendo wa vanguvangu,
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.
3. Ina pendo la mizungu, na mzo mzo hadaa,
Kusudi ugawe fungu, wana washinde na njaa,
Ndipo hapo Mcha Mungu, sishiriki nakataa!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.
4. Asonazo hupumbaa, kwa zile stihizai,
Akawa Kama kichaa, kwa Penzi la ulaghai,
Kwake aone kinyaa, japo sekunde hakai!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.
5. Tatizo jitumbukize, kumuoa kwa papara,
Mkeo umfukuze, yeye atwae kitara,
Atakuja akulize, ukabaki na izara!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo
6 zamani alikubeba, Kama mwana mbelekoni,
Kukuganda Kama ruba,ukadhani umewini,
Uchao sasa adhaba, na ya kale huyaoni!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.
7. Kaditama kina BABA, tangu Leo jifunzeni,
Ya nje sio mahaba,na Hilo jiepusheni,
Tuyakidhi matilaba, ya familia nyumbani,
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Lambert F. Chialo (Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713961860
 
Back
Top Bottom