Nyumba inapangishwa ipo kijitonyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba inapangishwa ipo kijitonyama

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Kitomai, Jan 5, 2011.

 1. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ina vyumba vitatu. Ipo kijitonyama Kisiwani. Ipo vizuri sana. Inapangishwa kwa sh 400,000 kwa mwezi. Maelewano yapo. Wahi usichelewe. Mawasiliano 0784 225 000
   

  Attached Files:

 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Vyumba vingapi vya kulala?
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kitu kimesimama hiki kwa wale wenye nyumba ndogo changamkeni
   
 4. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Vyumba vitatu vya kulala
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  nzuri sana tatizo ka TGS D kote kataishia humo kwenye kodi
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  dah aisee hili deal la ukweli
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Subiri niangalie mshahara : 350,000*12= 4,250,000. Less PAYE,NSSF,mh! Anyway,Kodi 400,000*12= 4800,000 /=duh! Nkikopa lak 6 sawa ila mwaka huu sitakula wala kulipa nauli. Sijui nkope? Nimeshtuka sitaki tena,ntakufa kwa presha bure!!
   
 8. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mbona cm yako tunakupigia haupokei mkuu au ushapangisha nini?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha hapo si bora uishi mwenyewe na mama nanihii
   
 10. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na wewe umeanza kazi ya udalali?
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu yaani maisha ya bongo ni utapeli mtupu. Hivi hii nchi ina mcha Mungu kweli ukitoa watoto wadogo. Maana vipato na matumizi ya watu haviendani kabisa.
  Utashangaa mpangaji wa hiyo nyumba mshahara wake ni 500,000 kwa mwezi na ana mke na watoto wawili na hana biashara nyingine, wife yuko home na jamaa ana gari la kutembelea na anatumia simu tatu zinazouzwa laki sita kila moja.

  Hapo ndipo ninachoka kabisa!
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unakuta kalani wa mahakama ya mwanzo amempangia nyumba ndogo hapo bado bili za umeme na maji, chakula, usafiri, vinywaji, kujiremba n.k
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  nchi hii hakuna wala rushwa wakubwa kama watumishi wa mahakama. Nilikuwa najiuliza kila siku kwa nini vijana wengi wanakimbilia kusoma sheria au kwenda kusoma Lushoto chuo cha usimamizi wa mahakama, kumbe wanajua ukitoka huko unanyookewa milele mradi uajiriwe tu. Makarani, mahakimu na majaji nchi hii hakuna msafi hata mmoja.

  Kuna mmoja alikuwa pale kimara mahakama ya mwanzo kama hakimu inasemekana kwa siku alikuwa anatoka na pesa nyingi sana. imagine hakimu mahakama ya mwanzo ana nyumba kadhaa hapa mjini za kupangisha, ana simu za nguvu, anaishi kijitonyama kwenye nyumba yake mwenyewe, watoto wake wa kike wanasoma Marian girls bagamoyo-ada kwa mwaka 1.2ml plus na pengine anao wawili au watatu au wako aga khan mzizima. na ana daladala kama nne hivi coaster-Japan, na amenunua zote kwa mkupuo..................... na pay slip yake inasomeka tsh 260000
   
 14. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 565
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Mnahamrabia jamaa biashara yake ya kupangisha....fungua mjadala mpya wa hiyo topic....issue hapa ni nyumba inapangishwa are u interested or not ....basi!!!
   
 15. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hakuna sheria inayomkataza mtu kuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja. Nadhani ili halina marumbano. Mtu mmoja anaweza kuwa na vyanzo zaidi ya mia moja vya mapato.
  Matharani, kuna mtumishi mmoja wa serikali ambaye naye analipwa mshahara wa sh 500,000. Mtumishi huyu ana duka hapo nyumbani kwake, ana genge la nyanya, vitunguu, matunda na mboga mboga. Amefuga ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kuku wa nyama na mayai, ana guest house, ana nyumba moja ya kupangisha ambayo mbele yake ina frem za maduka ambayo nayo anayapangisha. Ana vijibaiskeli vya kusambaza maji kawapatia vijana ajira , ana baba shop ya kunyoa manywele n.k.. Mkewe nyumbani anapika maandazi, vitumbua na chapati anasambaza katika migahawa.Huyu jamaa ana vyanzo visovyopungua kumi ninavyovijua mimi. Huyu ni mtu hodari na mchapakazi kweli kweli. Anatoka mikoa ya kaskazini, anaishi Mbezi ya shamba. Ukienda kumtembelea nyumbani kwake unakutana ana kwa ana na shombo la mifugo kama una-aleji nalo unaweza kuondoka bila kusema bai bai! Lakini yeye na familia yake wamelizoe kama wale jamaa wanaoishi kandokando ya dampo la kigogo. Majira zake hawlipendi hilo shombo wanapenda maziwa,mayai na nyama, maana huyu jamaa kila ifikapo siku kubwa lazima achinje! Wewe una vyanzo vingapi vya mapato? Kama unachokimoja tu cha huko Sirikalini, ushauri wa bure fungua banda la chips mayai hapo mtaani kwenu maana wakazi wa Dar hawapendi wugari! wanataka sana rede medi chips mayai zilizoandaliwa na mafuta ya koreeeeea!
   
 16. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Pengine ana vyanzo vingine vya mapato ambavyo ambavyo havipo bayana kwetu.
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  naona mpaka umebold, yaani biashara ya magenge nayo inaielezea kwa kudefend mpaka unaibold? unadhani hata tume ya maadili ya watumishi wa umma ina inawaangalia watumishi wenye biashara za magenge za mtaji wa sh 50,000 na mabanda ya swine? pathetic.
  ni vyema kusoma posts za wengine ukazielewa wanachomaanisha. if you can not analyse, it is better not to comment anything.
   
Loading...