Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Hii ni nyumba ya kihistoria iliyojengwa na muingereza ambayo baada Tanzania kupata uhuru nyumba hiyo ilianza kutumiwa na Mkuu wa mkoa ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mmoja wa wasomi wachache waliokuwa Tanzania ndugu Dr. Wilbert Kleruu.
Kwa wale wanaoijua historia na wale waliosoma sheria jina Said Mwamwindi na Dr. Kleruu (Said Mwamwindi v R (1972) HCD 212 ) sio majina mageni kwao.Pia kuna chuo cha Ualimu kimejengwa kuenzi kazi iliyotukuka ya Dr. Kleruu.
Kwa bahati mbaya nyumba hii haijatumiwa tena na wakuu wa mikoa waliofuata baada ya kifo cha Dr. Kleruu kutokana na kile kinachosemekana kuwa uoga.Nyumba hii imekuwa ikitumiwa na Jeshi.
Mbaraka Mwinshehe naye amepata kumuimba dr. Kleruu