Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,075
- 79,465
NYUMA YA PAZIA LA UTAWALA.
Na. Robert Heriel.
Maandishi ya Robert Heriel, kwa Lugha ya Kiswahili.
Makala hii isomwe kwa akili kubwa kwa wenye akili kubwa. Isomwe kwa akili ndogo kwa wenye akili ndogo. Lakini yote ya yote naomba nieleweke kuwa Mada hii ni habari za kimkakati na siri kwa walio wachache.
Mtawala ni mtu anayetumia udhaifu wa watu wengine kuwaongoza na kuwamiliki. Hujipa Mamlaka na madaraka kwa kutumia Udhaifu wa watu wengine. Huwatumia watu kama mali yake.
Hii ni tofauti kidogo na Kiongozi. Kiongozi ni mtu anayeshirikiana na watu wengine katika kutatua matatizo ili kufikia mipango waliojiwekea. Kiongozi hupewa Madaraka na mamlaka na Wenzake. Kiongozi hamiliki mtu bali yeye ni sehemu ya hao watu.
Katika Dini. Mungu ndiye Mtawala. Yeye ndiye anaongoza dunia na kuimiliki. Mungu sio kiongozi kwa kuwa yeye sio mmoja wetu. Yeye ni Mtawala. Hatukumchagua ila yeye ndiye katuchagua.
Mtawala hufanya vile atakavyo bila kuingiliwa na mtu. Haulizwi wala kukosolewa kwa kuwa yeye ndiye mmiliki. Kila Afanyalo mtawala ni haki hata kama linaumiza wengine.
Historia ya Dunia inaonyesha kuwa Wapo watu waliamua kujichukulia maamuzi ya kuwa Watawala. Kutokana na nyongeza walizokuwa nazo. nyongeza za maumbile yenye nguvu kuliko wengine, nyongeza ya akili kuliko wengine, wakaamua kuwatawala wale waliodhaifu.
Hapa ndipo mada yetu Ilipo.
Kulingana na Biblia, tunaona mahali Mungu akimuambia Hawa kuwa Mwanaume atakutawala.
Mwanzo 3;16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Neno kutawala linamaana kadhaa, Mosi mamlaka juu ya mwanamke, madaraka na Umiliki dhidi ya Mwanamke.
Ili uwe Mtawala ni lazima uwe na Sifa zifuatazo;
1. Akili Kuliko unachokitawala.
2. Nguvu kuliko unayemtawala.
3. Propaganda
4. Umoja kuliko wanaotawaliwa.
Mambo hayo manne ndiyo yanamsimamisha Mtawala kwa ngazi ya Binadamu na viumbe hai hapa duniani.
Ukisoma Maandiko hayo hayo mwanzoni kabisa tunaona Mungu akiwapa Mamlaka Wanadamu kuwatawala viumbe wengine waliopo ardhini, angani na Majini.
Mwisho tunaona Nuhu(hapa sio Mungu) akitoa utawala miongoni mwa jamii za wanadamu. Tunamuona Hamu akipewa laana na Baba yake kuwa atakuwa mtumwa wa Shemu na Yafethi. Yaani atatawaliwa.
Mambo yanayojitokeza hapa.
1. Mwanadamu ni mtawala wa Dunia.
2. Mwanamme ni mtawala wa Mwanamke.
3. Jamii ya Shemu na Yafethi ni Watawala kwa jamii za Hamu.
Unachopaswa kukumbuka ni kuwa Tawala mbili zimetolewa na Mungu ambazo ni Mwanadamu kutawala duniani na vilivyomo. Pili, Mwanaume kumtawala Mwanamke.
Hiyo ya Tatu ni Laana kutoka kwa Nuhu wala sio Mungu. Hii nimeona niiweke sawa huko mbele nitaeleza.
Ili utawala lazima ukejeli na kuponda udhaifu wa wale unaotaka kuwatawala. Lazima utumie matusi na dhihaka kwa wale unaoenda kuwatawala.
Lazima uyaponde na kuyakosoa madhaifu yao. Kisha ukiyaponda na kuyakejeli kinachofuata unawaambia kuwa pamoja na madhaifu yenu lakini wewe unaweza kuwasaidia.
Lengo la Watawala kuwatukana na kuyaponda madhaifu ya wanaotaka kuwatawala yaani watawaliwa ni kuwafanya wajione duni mbele yao. Wajione ni kweli wanastahili kutawaliwa. Hicho ndicho wanakitafuta na wakikipata basi mtawaliwa ujanja utakuwa umemuisha.
Wakoloni walipokuja Bara la Afrika walitumia mbinu ya Kuziponda na kuzitukana tamaduni, sayansi na vyakula vya kiafrika. Walidhihaki na kuwaita Waafrika ni Manyani. Waliwaona Waafrika hawajastarabika.
Wakifanikiwa Kuwadunisha na hatimaye Muafrika alikuwa duni mbele ya Mtu mweupe mpaka hivi leo. Rasmi Bara la Afrika likatawaliwa na Wageni na watu weupe wakageuka watawala na Waafrika wakawa Watawaliwa.
Jamii za Kiafrika zilizobisha zilichezea kichapo. Na hapo hoja ya nguvu ya mtawala ikaonekana wazi.
Miaka ya sitini Waafrika wakawa wamechachamaa kujitawala. Lakini hakukuwa na uhalisia zaidi kutokana na kuwa Wazungu waliona kuwatawala Waafrika moja kwa moja haina manufaa kama kuwapa uhuru wao.
Waliona kuna manufaa mengi kuwapa uhuru kuliko kuendelea kuwatawala. Wakaona Ukoloni mamboleo ndio suluhisho la wakati huu. Ndicho kilichotokea.
Kwa habari za mwanaume na mwanamke. Ni miaka mingi imepita bado Mwanamke yupo chini ya utawala wa mwanaume. Pamoja na jitihada zilizofanyika lakini bado Mwanamke yupo chini ya utawala wa Mwanaume.
Hata huu mpango wa kuwapa Wanawake uhuru ni mkakati wa Watawala kujinufaisha. Sijajua kama jambo hili Wanawake wanalijua
Watawala wameona kumpa mwanamke uhuru kunafaida zaidi kuliko kumnyima uhuru.
Makampuni makubwa kwa kuligundua hili. Kwa makusudi yanapigana kufa kupona. Liwake jua inyeshe Mvua lakini Mwanamke apewe uhuru. Naam unaitwa uhuru mamboleo.
Najaribu kufikiri kuwa endapo Mwanamke hatapewa uhuru bila shaka biashara nyingi zitalala. Makampuni mengi yatafungwa na kupata hasara.
Hivyo chakufanya ni kuwapa uhuru ili watawala wapate faida.
Biashara za vipodozi, urembo na mavazi zinategemea zaidi mwanamke awe huru ili ziuzike. Nani asiyejua kuwa nguo nyingi siku hizi ni zile zinazomuonyesha Mwanamke akiwa uchi.
Bado lengo la Watawala ni lile lile kuwakashifu wanawake kuwa ni watu wajinga wasiojitambua. Watu wasiojielewa. Lakini kwa mwanamke hawezijua hila hii ya Watawala.
Biashara za Filamu za Uchi zitadoda ikiwa uhuru wa Mwanamke utabanwa. Biashara za umalaya nazo zitadoda. Nani asiyejua.
Biashara za kuongeza makalio, nyonga na maziwa zitadoda.
Mtawala ni mtu anayeishi kwa Propaganda. Muda mwingi huutumia kuunda maneno na kuyavumisha hata kama hayana ukweli.
Wanaume wamefanikiwa kuunda propaganda kuwa wanawake ni viumbe dhaifu. Hii imetapakaa kila kona. Wanatumia Media na dini kueneza uzushi huu ili waendelee kumtawala mwanamke. Nani asiyejua kuwa hata sisi wanaume tunamadhaifu mengi tena usishangae yakawazidi hao wanawake. Lakini Propaganda imetufanya tuwatawale hawa wenzetu.
Ipo propaganda nyingine isemayo Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe. Lengo la hii propaganda ni Kuwagawa wanawake ili wasipendane. Ni mbinu ya Kuwatawala wanawake kwa urahisi.
Ndio maana nikasema moja ya mambo yanayojenga watawala ni Umoja. Wanaume wao ni wamoja na kamwe hawataruhusu Wanawake wawe kitu kimoja. Ili wapate uhuru wao.
Watawala huwapa uhuru watawaliwa ikiwa kuna manufaa. Ndio hata wanaume hufanya hivyo kwa Wanawake. Siku hizi mwanamke anaweza kuamua asitolewe mahari au Aolewe bila bikra. Mwanaume akakubali kwa kuwa inamnufaisha.
Mwanaume aliyemtawala anaweza fanya jambo baya. Mfano kuzaa kabla ya ndoa lakini ipo propaganda inayowasapoti isemayo Huna hata mtoto wa kusingiziwa. Au wewe ni kidume.
Lakini jambo hilo hilo likifanywa na Mwanamke ambaye ni mtawaliwa utasikia wewe ni malaya. Utasikia nani aoe single Mother. Wengine wameunda propaganda kuwa Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni kununua kiwanja chenye mgogoro. Au kuanza mechi ikiwa 0-1.
Mtawala siku zote hakosei hata kama amekosea. Mtawaliwa hata kama hajakosea unaweza shangaa akiambiwa amekosea.
Watawala wa Kizungu sio kwamba huko kwao hakuna mauaji. Hakuna ubakaji. Sio kwamba hakuna Rushwa lakini kamwe huwezi sikia wakizodoana wenyewe kwa wenyewe.
Wapo viongozi huko Ulaya wanaoongoza kama Wafalme. Wapo wanaoongoza zaidi ya mihula minne lakini kamwe huwezi sikia Wakizodolewa. Sababu ni kuwa wao ni watawala. Wanaumoja na wanajua kucheza na Propaganda.
Njoo Afrika. Yakitokea Mauaji kidogo. Utasikia wazungu wakipiga kelele ooh! Muafrika ni Muuaji si mnaona. Ikitokea vita au Ufisadi utasikia wakitukana.
Lengo lao ni kutufanya watawaliwa tujione dhaifu. Usishangae kusikia muafrika akijidharau kuwa sisi waafrika ndivyo tulivyo. Sisi tuna roho mbaya. Sisi ni masikini. Hayo ni matokeo ya Propaganda za Watawala.
Katika kufanya hivi watawala hujifanya kutoa msaada kutusaidia. Sio kwa sababu hatuna uwezo bali ni kwa sababu tumeshakuwa watumwa wao. Wameshatutawala kiakili na kimipango.
lengo lao sio kutuona tukifurahi bali kutufanya tuzidi kuwatukuza na kujiona sisi ni duni na wao ni bora.
Hata wanawake nao wamekuwa wakuwa wakitaka kuhudumiwa na Wanaume. Wao huona ni haki yao kuhudumiwa kumbe wamejiweka kwenye kundi la kutawaliwa. Hiyo yote ni matokeo ya watawala ambao hapa ni wanaume.
Lengo sio kuwasaidia wanawake bali kuwafanya wazidi kujiona wao ni duni kuliko wanaume. Siku hizi Wanaume wameamua Kuwapa uhuru wa kujitafutia na kusoma.
Lengo ni kupunguza kazi ya kuwatawala. Kupunguza gharama ya kuhudumia koloni. Siajabu siku hizi mwanamke akajilipia mahari.
Siajabu siku hizi mwanamke akawa tayari kuwa na wanaume wawili akidhani ni unafuu kumbe ndio anajitia kwenye utumwa zaidi.
Mwisho nimalize kwa kusema kuwa Watawala wanabadilika na kubadilisha mbinu kulingana na wakati na unafuu watakaouona.
Utawala utadondoka ikiwa halikuwa ni tamko la Mwenyezi Mungu. Lakini siku zote mwanadamu atakuwa mtawala wa Viumbe wengine kama Mungu alivyosema.
Tawala zingine ni changamsha Genge.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300