Nyoni hajafukuzwa kazi amepewa likizo kupisha uchunguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyoni hajafukuzwa kazi amepewa likizo kupisha uchunguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kakakuona40, Feb 10, 2012.

 1. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana tulipewa taarifa humu na wanajami kuwa Nyoni ameachishwa kazi, taarifa zile ni za upotoshaji kabisa kilichotokea ni kuwa amepewa likizo ya lazima kupisha uchunguzi, na kama iliyozoeleka na tanzania yetu hii Uchunguzi waweza kuwa positive au negative ikiwa tuhuma dhidi yalke zitashindwa kuthibitika ina maana kuwa dada yetu ataendelea kupeta katika wizara.

  Pia nimepitia magazeti na taarifa mbali mbali sijaona tuhuma dhahiri dhidi ya Mponda labda mnisaidie wana JF, watu lazima walete mifano na uthibitisho hata wa tuhuma moja ambayo mh. Mponda anayo. Mwacheni apige kazi mweshimiwa.
   
 2. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  ubalozi uswiss au uk unamsubiri huyo
   
 3. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hao huwa hawakutwi na tuhuma hata kama anazo tuhuma na ushahidi ukapatikana,
  so akirudi kitarani mgomo unaanza upyaaaaa,
  na madai yanakuwa makali zaidi,aondoke kabisa hatumtaki
   
 4. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  akifukuzwa huyo mama ntatembea uchi
   
 5. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  kwa wenzetu mtu akikutwa na kimada analazimika kuachia madaraka. Huku kwetu hata ukiua wanaendelea kukutetea kwamba umeua bila kukusudia. Dah! Anyway,kuna clinical coats mnh amepewa kila daktari,gharama yake ni sh 350000 kila koti. Yana nembo ya mariedo.
   
 6. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mponda ndiye mkuu wa sekta ya afya hapa nchini. Anatakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kuisimamia na kuleta maboresho, ingawa muda si mrefu kuna watu humu watakuja na maelezo kuwa aliikuta sekta ikiwa hivyo kwa hiyo si kosa lake.
  Lakini hata kama kwa minajili hiyo niliyoitaja hakuwa na ulazima wa kujiuzulu, basi sasa hivi inambidi sababu kutowajibika kwake kumesababisha vifo vya watu wengi ambao wangeweza kuwa hai leo hii. Hili ni doa kubwa katika maadili ya uongozi, hivyo dhamira yake inapaswa kumsuta.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi dhidi yao waanzishwa
  [​IMG] Madakatari kurejea kazini leo
  [​IMG] Posho zao zaongezwa mara moja  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Stephen Ulimboka, akizungumza kwenye mkutano wa madaktari na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika ukumbi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jana.


  Wakati madaktari wamekubali kusitisha mgomo wao na kurejea kazini leo huku wakiipa serikali mwenzi mmoja kutekeleza madai yao, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Brandina Nyoni, na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa wamesimamishwa kazi.

  Hatua ya kuwasimamisha kazi watumishi hao waandaamizi ilifikiwa jana baada ya madaktari kuwashtaki kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
  Madaktari hao walisitisha mgomo wao mara baada ya kukutana na Pinda katika mkutano ambao walizungumza bila vigogo hao wa wizara kuwepo.
  Mkutano huo ulihudhuriwa na madaktari na wauguzi. Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Memejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana na waganga wakuu wa manispaa za Jiji la Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Madaktari, Dk. Ulimboka Stephen, alisema leo watarejea kazini baada ya Waziri Mkuu kuwaahidi kuwatekelezea madai yao ndani ya siku 14.
  Alisema watakutana Machi 3, mwaka huu ili kubaini kama serikali imetekeleza jambo hilo au la na kwamba watawajulisha madaktari walioko mikoani warejee kazini huku wakisubiri utekelezaji wa serikali.
  Awali, Pinda alitangaza kuwasimamisha kazi Nyoni na Dk. Mtasiwa na kusema amefikia hatua hiyo kutokana na kupokea malalamiko mengi dhidi yao.
  Alisema zipo tuhuma mbalimbali dhidi yao zikiwemo sare za wauguzi na vifaa vya kupima Ukimwi vilivyonunuliwa vikiwa ni feki na kwamba mwenye mradi ni mmoja wa vigogo wizarani.
  “Vifaa hivyo vya kupimia Ukimwi havikuwa katika ubora na vilikuwa vinaonekana ni feki na mradi huo tumeambiwa ni wa wizara na hata tenda ya usafi katika Hospitali ya Muhimbili tumejulishwa ni mradi wa mtu wizarani,” alisema Pinda.
  Pinda alisema kutokana na malalamiko hayo, ameona ni lazima pawepo na tatizo na kuamua kuwasimamisha ili kupisha vyombo vya dola kuchunguza.
  Alisema tuhuma hizo zikibainika hatua zitachukuliwa dhidi ya watendaji hao na kuongeza kuwa vigogo hao watapatiwa barua ya kusimamishwa na kwamba watateuliwa watu wa kukaimu nafasi hizo.
  Pinda alisema Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, watachukuliwa hatua na Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa ndiye aliyewateua.
  “Rais naye atachukua hatua kwa Dk. Mponda na Dk. Nkya kwa kuwa ndiye aliyewateua kwani kumekuwa na mzozo katika wizara hiyo tunataka kuiboresha,” alisema Pinda.
  Baada ya Pinda kutangaza uamuzi huo, madaktari hao walifurahi na kudai kuwa kwa sasa watakuwa na uhuru wa kueleza matatizo yao.
  Kuhusu madai ya madaktari waliogoma, Pinda alisema alikabidhiwa maazimio manane ya madaktari hao mgomo ulipoanza ambayo aliyafanyia kazi.
  Alisema baadhi ya maazimio hayo amekwisha kuyashughulikia na mengine kuyaundia kamati kwa ajili kuyafanyia tathmini.
  Alisema kamati hiyo imepewa siku 14 kumaliza zoezi hilo ikiwa chini ya usimamizi wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na baada ya hapo itatolewa ripoti.
  Kuhusu madaktari walioko kwenye mafunzo kwa vitendo ambao walihamishwa na kupelekwa katika maeneo mengine amelishughulikia na kuhakikisha wamerudishwa katika Hospitali ya Muhimbili.
  POSHO ZAPANDA
  Kuhusu posho ya dharura ambayo inatolewa kwa madaktari bingwa ya Sh 10,000 imepandishwa hadi Sh. 25,000.
  Wanaopata Sh. 3,000 watapata Sh. 10,000, waliokuwa wanapata Sh. 5,000 watapata Sh. 15,000 na waliokuwa wanapata Sh. 10,000 watapata Sh. 20,000.
  Hata hivyo, alisema viwango hivyo ni vya muda hadi bajeti ya mwaka 2012/13 itakapopitishwa.
  Kuhusu posho ya mazingira hatarishi, alisema kuwa jambo hilo ameridhia na kwamba ni haki yao kupatiwa.
  Alisema ameiagiza kamati hiyo kuangalia makundi ambayo yanafanya kazi katika mazingira hatarishi ili kupewa kipaumbele.
  Kuhusu posho ya nyumba kwa madaktari, alisema serikali inashughulikia suala hilo kwani kuna mpango wa ujenzi wa nyumba kwa madaktari ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Alisema kamati itakuja na majibu ya suala hilo.
  Akizungumzia posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu, Pinda alisema suala hilo linatakiwa kuangaliwa kwa wafanyakazi wote wa afya na kwamba kamati itakuja na majibu.
  Kuhusu usafiri, aliwataka wajisajili katika mfuko wa utumishi wa kuwakopesha wafanyakazi magari.


  NYONGEZA YA MSHAHARA

  Kuhusu ongezeko la mshahara ambalo madaktari hao walipendekeza kufikia Sh. milioni 3.5, alisema jambo hilo kwa sasa haliwezekani kwa kuwa bajeti imeshapangwa.
  Alifafanua kuwa kamati itafanya tathmini na kuja na majibu kwa ajili ya bajeti ijayo.
  Kuhusu bima ya afya kwa madaktari, alisema ni haki yao na kwamba litashughulikiwa.
  Pinda aliwataka madaktari kutokukubali kutoa rufaa pale wanavyopatiwa vibali kutoka wizarani kwani ni jukumu lao kujua kama mgonjwa huyo anatakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi au la.
  “Msikubali kupokea kimemo kutoka wizarani fanyeni kazi kwa taaluma zenu na msikubali kuingiliwa,” alisema na kuongeza: “Na nyie madaktari mnakosea kuwakubalia hivyo vimemo vyao itafika mahali kutafanyika biashara ya wagonjwa, haiwezekani kwenda kijanja kijanja.”
  MADAI DHIDI YA NYONI
  Nyoni anadaiwa kuwa na tuhuma 18, zikiwamo za kujinufaisha mwenyewe, za upendeleo kwa watu wake, na zinazoingilia masuala ya zabuni kinyume cha taratibu.
  Kwa kuwa jana hatukuweza kumpata kwa simu yake ya mkononi tumeamua kucha kuchapisha tuhuma hizo hadi atakapopatikana.

  SPIKA: SERIKALI IMETUSIKIA
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameeleza hatua zilizochukuliwa na Bunge katika kutatua mgomo wa madaktari kwamba Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Pinda wamekubaliana na ushauri uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.
  Makinda alisema tangu mwanzo wabunge walipoomba mwongozo wa Spika kuhusiana na mgomo wa madaktari, aliwaeleza kuwa kulikuwa na kauli ya serikali ambayo itatolewa kuzungumzia tatizo hilo.
  Alisema baadaye aliwaeleza kuwa ameituma Kamati ya Bunge ya Huduma ya Jamii kwanza kupokea taarifa ya serikali na kisha kwenda kufuatilia mgomo huo.
  “Kamati yetu imefanya kazi kwa muda mfupi, lakini imefanya kazi kubwa sana na kwa sababu ya udharura wenyewe ilibidi tutumie kamati ya uongozi kupokea taarifa ile na tumeipokea maana na wao wenyewe wamefika usiku,” alisema na kuongeza:
  “Ilibidi tutumie namna yoyote waweze kufika ili waweze kuitolea taarifa kwenye kamati ya uongozi yale yote waliyoyaona hata kabla hawajaandika taarifa yao yote na Kamati ya Uongozi pamoja na Kamati ya Huduma za Jamii tumefanya shughuli ya taarifa hiyo tukiwa tumepata maelezo ya wenzetu waliofika kule.”
  Alisema kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Margaret Sitta, ilipata maelezo ya madaktari na kutembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuongea na watu mbalimbali ambao walipata undani wa hali halisi.
  “Ushauri wao tumeujadili jana (juzi), usiku mpaka tumemaliza kikao kama saa 6.00 usiku baada ya saa 6.00 usiku kwa kuwa mambo yenyewe yalikuwa ni ya haraka wakanituma kutafuta viongozi wengine wa nchi Rais na Waziri Mkuu usiku jana (juzi), kwa hiyo tumeongeza na Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu wote wanakubaliana na mapendekezo yaliyotolewa na kamati,” alisema.

  Imeandikwa na Beatrice Shayo na Gwamaka Alipipi, Dar na Sharon Sauwa, Dodoma.  CHANZO: NIPASHE
   
 8. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  *Pinda asema Dkt. Mponda, Nkya nao kuchunguzwa
  *Madaktari waipongeza serikali, wakubali kurudi kazini
  *Wahadharisha madai yao kusikilizwa kabla ya Machi 3

  Grace Ndossa na Rehema Maigala

  SIKU moja baada ya wanaharakati jijini Dar es Salaam kuandamana kwa lengo la kuishinikiza Serikali ikutane na madaktari ili kuepusha vifo vya Watanzania wasio na hatia, Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, jana amewasimamisha kazi vigogo wawili wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

  Vigogo hao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa.

  Bw. Pinda alitangaza uamuzi huo Dar es Salaam jana alipokutana na madaktari waliokuwa kwenye mgomo pamoja na wauguzi ambao walipokea uamuzi huo kwa shangwe na furaha kubwa.

  Kutokana na tamko hilo, madaktari hao waliahidi kurudi kazini kuanzia leo ili kuokoa maisha ya Watanzania wanaoteseka kutokana na kukosa matibabu tangu mgomo huo ulipoanza.

  “Hatua stahiki zimechukuliwa kwa mambo yanayozungumziwa wizarani hivyo Katibu Mkuu (Bi. Nyoni) na Mganga Mkuu wa Serikali (Dkt. Mtasiwa), tunawapa barua za kuachia ngazi, lengo ni kutoa nafasi ya kufanya uchunguzi, kusafisha Wizara na jina lake.

  “Najua wataumia sana na kusema wameonewa, lakini hakuna jinsi, lazima waondoke ili kupisha uchunguzi na kusafisha jina la Wizara hii ambalo limechafuka sana,” alisema Bw. Pinda.

  Madaktari na wauguzi ambao walikuwa makini kumsikiliza Bw. Pinda akitoa tamko hilo, walionesha furaha zao kwa kupiga kelele, miluzi na kugonga meza hali ambayo ilisababisha kiongozi huyo kusitisha hotuba yake kwa muda.

  Habari za uhakika kutoka wizarani zinasema kuwa, watumishi wa Wizara hiyo wamefurahishwa na hatua ya Serikali kumsimamisha Bi. Nyoni kwa sababu wanazojua wenyewe.

  Akizungumzia hatma ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda na Naibu wake, Dkt. Lucy Nkya, Bw. Pinda alisema, viongozi hao wana kofia ya kisiasa lakini watachunguzwa.

  “Madaktari wangu chonde chonde, naomba mrudi kazini mkatumikie Watanzania, muwe na uzalendo na mzingatie viapo vyenu na moyo wa huruma,” Bw. Pinda aliwasihi madaktari hao.

  Alisema Serikali inashughulikia madai yao tume iliyoundwa kupitia madai yao, imepewa siku 14 na kupeleka majibu serikalini ili kuona utaraibu wa kuongeza posho.


  Kuhusu madai kuwa viongozi wanatibiwa nje ya nchi hata kwa magonjwa ambayo yanawezekana nchini, Bw. Pinda alisema kuanzia sasa watu wa ngazi ya chini ambao hawana uwezo ndiyo watapewa kipaumbele.

  Akizungumzia hatua ya Serikali kupeleka baadhi ya viongozi kutibiwa nje ya nchi, Bw. Pinda alisema kuanzia sasa watalazimika kupimwa na madaktari watatu ili wajiridhishe kama kuna sababu za msingi za kupelekwa huko.

  Aliagiza madaktari wote waliowahi kupewa vimemo na viongozi ili waruhusu wagonjwa fulani kwenda kutibiwa nje, waviwasilishe kwake ili hatua zaidi zichukuliwe.

  “Madaktari zingatieni maadili ya kazi yenu si kukubali vimemo vinginevyo mtafanya biashara ya wagonjwa,” alisema Bw. Pinda na kuongeza kuwa, suala la kukopeshwa magari, wataingizwa katika utaratibu wa kukopeshwa vyombo hivyo vya usafiri.

  Kuhusu nyumba za kuishi, alisema Serikali itawapa posho ili kulipia nyumba kupitia mishahara yao au kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya kuwajengea nyumba.

  “Hakuna daktari hata mmoja ambaye atafukuzwa kwa sababu ya kushiriki mgomo huu, endeleeni na kazi kwa amani na kuwaonesha upendo wagonjwa,” alisema.

  Baada ya kumalizika hotuba yake, madaktari hao walimuhakikishia Bw. Pinda kuanza kazi rasmi kuanzia leo na kuitaka Serikali itekeleze ahadi yake.

  Walisema kama Serikali itashindwa kufanyia kazi madai yao kabla ya Machi 3 mwaka huu, wataamua hatua zingine za kuchukua ambazo zitakuwa ni kali zaidi.

  “Kabla ya sisi kurejea kazini, tunaomba wanaharakati wote waliokamatwa na polisi leo wakiwa katika majengo ya Hospitali hii ya Muhimbili kwa lengo la kututetea, waachiwe huru bila kuwekewa pingamizi lolote,” walisema.
   
 9. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jamani tutenganishe utendaji wa kiserikali na kisiasa. Mgogoro umesababishwa na Blandina Nyoni na mhauri wake mkuu Dr Deo Mtasiwa. Waziri ni mtu anayeandikiwa hotuba na taarifa mbalimbali. Jamani tuwe wakweli tusipende tu kukurupuka rumuonee hurunma Dt Haji Mponda na naibu wake Dr Nkya walikuwa wanafanya kazi na KM ambaye yuko corrupt vibaya sana na ambaye ungeshisi kama vile analindwa na mfumo wa usalama wa nchi. Ukizisoma tuhuma za Blandina unaona zimejaa ufisadi, ukabila na wizi wa moja kwa moja. Tuhuma hizi ziko muda mrefu lakini Dr Haji Mponda na naibu wake Nkya hawana tuhuma yeyote ya matumizi ya madaraka wala ufisadi. Maamuzi mengi ambayo yamewakwaza madaktari yamefanyika mwaka 2010 na 2011 na Blandina Nyoni aliyekuwapo hapo tangu 2008 na Dr Mtesiwa aliyekuwapo tangu 2006.

  Mtanzania yeyote angeweza kupatwa na situation iliyompata Dr Haji Mponda kwenye utendaji wa Nyoni. Naomba turejee hata kwenye utawLa wa Profesa Mwakyusa, mutakumbuka kuwa hata yeye alikuwa anafunikwa na huyu mama. Kwa mtazamo wangu mimi tatizo ni la mfumo wa utendaji wa serikali, kwa hiyo napendekeza tumpe muda Dr Haji Mponda
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mleta thread huwa ni mdini sana mpaka thread zake naziogopa!
   
 11. N

  Njaare JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Kaka/Dada,
  Mawazo kama haya ndo yanatufanya watanzania tusiendelee. Kwa nini unang'ang'ania kazi ambayo huiwezi? Umepewa uwaziri unatakiwa uisimamie wizara. Kama kuna mtu ndani ya wizara anakushinda unamwambia rais huyu mtu simwezi, mwondoe yeye au mimi niondoke. Unamkumbuka Magufuri alivyofanya kwa Ephraim Mrema? Umemwona Mkurugenzi mpya wa COSTECH alichokifanya? Matatizo yoote ya wizara ni kwa sababu ya kuwa na waziri mdhaifu. Udhaifu kwenye secta nyeti haufai.

  Naona una mawazo kuwa uwaziri ni ulaji. Bora napata maslahi yangu ya uwaziri, basi. Kwa mtindo huu hatutaendelea. Viongozi lazma wawajibike hata kama si mwizi ila kama taasisi unayoiongoza haionyeshi maendeleo inamaana huna ubunifu kwa maana nyingine huna jipya, huna mshiko, huna mvuto achia ngazi.

  Wapo viongozi (Wakurugenzi, mawaziri, maCEO) ambao si wezi ila taasisi wanazoongoza hazionyeshi kuwasaidia watanzania. Zipo zipo tu. Hao nao waachie wengine wenye ubunifu. Si lazima uwe na tuhuma za rushwa ndo uondoke. Mponda ni mmojawapo kama unavyosema hana kashfa ya ubadhirifu ila hana ubunifu. Yupo tu ili kupokea mshahara.
   
 12. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  .. Wakimfukuza watakuwa 'wamemuonea' maana kuna wengi ambao wana tuhuma za ubadhirifu lakini hawajaachishwa kazi.
   
 13. l

  lookieloo Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama nyoni hafai period asimamishwe afukuzwe haijalishi she is insnsitive she feels she is up there. Wizara ya afya inahitaji sensititive people sooooooooo fired or not fired health is not for her!
   
 14. nkawa

  nkawa Senior Member

  #14
  Feb 11, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama Nyoni? Na mganga Mkuu Dr. Mtasiwa...mahakama inamsubiri?
   
 15. l

  lookieloo Member

  #15
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo mwanzo wa exit
   
Loading...