Toka mwaka 2010 increment hakuna.
Mbaya zaidi ndugu zangu hata madaraja kulingana na mikataba hiyo ni kwamba mtumishi atapanda daraja kila baada ya miaka mitatu.jambo hili nalo halifanyiki.zaidi sana mtu akikumbukwa hupandishwa baada ya miaka minne au mitano na zaidi.huu ni wizi na unyanyasaji pia.vyama vya wafanyakazi vinakata mishahara yetu kila leo lakini hatuoni wakifanya chochote kuhusu haya manyanyaso.wfanyakazi tufanyeje sasa?
increment huwa haipandi kama kutatokea mabadiliko ya mshahara (ongezeko la mshahara).. na toka 2010 kila incremental year kumekuwa na maboresho ya nyongeza ya mshahara... so hauwezi kupanda increment..
isipokuwa ikitimia miaka mitatu ya utumishi kazini hata kama bado uko mfano c1 utaruka hadi daraja d1.. hapo ndipo utakapompita huyo unayeona kaajiriwa juzi na mko sawa
...
isingetokea ongezeko/badiliko la mshahara mfano mwezi wa 7 mwakani lisipokuwepo hapo utapanda hichi kidaraja kidogo c1-c2 ...
Miaka ya nyuma licha ya ongezeko la mishahara kila mwaka annual increament ilikuwepo .hivyo kuwepo ongezeko la mwaka sio sababu ya msingi zaidi ya kuwaibia wafanyakazi.nyaraka za mishahara zinaonesha uwepo wa annual increament lakini hawatekelezi.kuna sababu gani za kuonesha kuwa jambo hilo lipo wakati sio uhalisia.hata waraka wa mabadiliko ya mishahara 2015/2016 umeonesha uwepo huo.