Nyongeza ya mishahara: Wafanyakazi tusimlaumu Rais Magufuli, tujilaumu sisi wenyewe na TUCTA yetu kwa Usingizi wa Pono

NUMET

New Member
Nov 19, 2015
2
2
Rais JPM anatuamsha usingizini.

Nyongeza Ya Mshahara haijawahi kuwa keki hadi iletwe mezani kwenye kisosi.

Suala hili la nyongeza Ya Mshahara kwa sekta ya umma binafsi nalitazama katika mtazamo wa aina mbili.

1. Wafanyakazi kupitia shirikisho lao la TUCTA wameacha misingi Na malengo ya vyama vya Wafanyakazi Na kubuni utamaduni mwingine wa kizembe Kabisa.

Hakuna mwajiri ataamka asubuhi na kuwaongeza Wafanyakazi Mshahara wakati anawalipa zaidi au Sawa Na kima cha chini cha mshahara. Maboresho yote ya masilahi Na mazingira bora ya kazi, ni tunda la majadiliano Ya pamoja, Na makubaliano yakishafikiwa yanakuwa sheria, hakuna anayeweza kuyachezea akabaki salama. Sasa leo Wafanyakazi sekta ya umma wanalalamika kwamba Rais amegoma kuwaongeza Mshahara, Naomba niulize, kupitia vyama vyenu ni lini mlikaa Na mwajiri (Serikali) mkakubaliana juu Ya nyongeza Ya mshahara? Na je, mlikubaliana nyongeza Ya asilimia ngapi?

Kama kweli mlikubaliana, hamna haja Ya kulalamika, nemdeni CMA (Commission For Mediation and Arbitration) mkashinikize makubaliano yenu yatekelezwe, Na kama hamkuwahi kujadiliana Na mwajiri wenu basi kaeni kimya njaa iwaume ndo mpate kujitambua.

Badala Ya kumpigia kelele mheshimiwa Rais, wapigieni kelele viongozi wenu wa vyama vya Wafanyakazi wanaochukua ada zenu ili ziwasaidie kuendesha majadiliano Na badala yake wanasubiri miujiza Na huruma ya mwajiri iwaongeze mshahara.

2. Kwa upande wa pili naona pengine Mh. Rais alikuwa na nia kabisa ya kuwaongezea mshahara, lakini alipoona watu aliowaahidi wamelala usingizi wa pono akaamua kubadili gia angani maana wahenga walisema, mtoto asielia hanyonyeshwi.

Na pengine Anafanya hivi kuwakumbusha vyama vya wafanyakazi kutimiza wajibu wao wa KUDAI, KULINDA, KUTETEA Na KUBORESHA masilahi ya Wafanyakazi badala ya kusubiri mwajiri (serikaki) ajiamlie mwenyewe bila kushauriana Na upande wa Wafanyakazi.

USHAURI

Kwakuwa Serikali ilitoa ahadi za nyongeza ya Mshahara katika namna Na maeneo tofauti tofauti , ni busara Serikali kuangalia namna ya kuongeza Mshahara kwa utaratibu iliouahidi. Bila kufanya hivyo wafanyakaI watakuwa wameumizwa sasa kwa shida Kubwa iiliyosababishwa Na viongozi wa vyama vya Wafanyakazi.

Nicomedes M Kajungu
Katibu Mkuu
NUMET
 
Ya mishahara JPM yupo sahihi
Yeye sio wa kwanza duniani kutoongeza mishahara wafanyakazi hadi mambo yawe safi zaidi.
 
Ndugu watumishi wa umma mmeamkaje? Nawatakia uchapaji mwema wa kazi
 
mshahara uongezwe kwa wale wanaojituma tu..

sio sahihi mkuu wa mkoa kama makonda alipwe sawa na mkuu wa mkoa wa pwani au morogoro..

watu wanaojituma kama makonda ndio waongezwe mshahara peke yao
 
Rais JPM anatuamsha usingizini.

Nyongeza Ya Mshahara haijawahi kuwa keki hadi iletwe mezani kwenye kisosi.

Suala hili la nyongeza Ya Mshahara kwa sekta ya umma binafsi nalitazama katika mtazamo wa aina mbili.

1. Wafanyakazi kupitia shirikisho lao la TUCTA wameacha misingi Na malengo ya vyama vya Wafanyakazi Na kubuni utamaduni mwingine wa kizembe Kabisa.

Hakuna mwajiri ataamka asubuhi na kuwaongeza Wafanyakazi Mshahara wakati anawalipa zaidi au Sawa Na kima cha chini cha mshahara. Maboresho yote ya masilahi Na mazingira bora ya kazi, ni tunda la majadiliano Ya pamoja, Na makubaliano yakishafikiwa yanakuwa sheria, hakuna anayeweza kuyachezea akabaki salama. Sasa leo Wafanyakazi sekta ya umma wanalalamika kwamba Rais amegoma kuwaongeza Mshahara, Naomba niulize, kupitia vyama vyenu ni lini mlikaa Na mwajiri (Serikali) mkakubaliana juu Ya nyongeza Ya mshahara? Na je, mlikubaliana nyongeza Ya asilimia ngapi?

Kama kweli mlikubaliana, hamna haja Ya kulalamika, nemdeni CMA (Commission For Mediation and Arbitration) mkashinikize makubaliano yenu yatekelezwe, Na kama hamkuwahi kujadiliana Na mwajiri wenu basi kaeni kimya njaa iwaume ndo mpate kujitambua.

Badala Ya kumpigia kelele mheshimiwa Rais, wapigieni kelele viongozi wenu wa vyama vya Wafanyakazi wanaochukua ada zenu ili ziwasaidie kuendesha majadiliano Na badala yake wanasubiri miujiza Na huruma ya mwajiri iwaongeze mshahara.

2. Kwa upande wa pili naona pengine Mh. Rais alikuwa na nia kabisa ya kuwaongezea mshahara, lakini alipoona watu aliowaahidi wamelala usingizi wa pono akaamua kubadili gia angani maana wahenga walisema, mtoto asielia hanyonyeshwi.

Na pengine Anafanya hivi kuwakumbusha vyama vya wafanyakazi kutimiza wajibu wao wa KUDAI, KULINDA, KUTETEA Na KUBORESHA masilahi ya Wafanyakazi badala ya kusubiri mwajiri (serikaki) ajiamlie mwenyewe bila kushauriana Na upande wa Wafanyakazi.

USHAURI

Kwakuwa Serikali ilitoa ahadi za nyongeza ya Mshahara katika namna Na maeneo tofauti tofauti , ni busara Serikali kuangalia namna ya kuongeza Mshahara kwa utaratibu iliouahidi. Bila kufanya hivyo wafanyakaI watakuwa wameumizwa sasa kwa shida Kubwa iiliyosababishwa Na viongozi wa vyama vya Wafanyakazi.

Nicomedes M Kajungu
Katibu Mkuu
NUMET
Ikifika 2019 mtadanganywa na kinyongeza ili mumpe kura 2020
 
Hii ni fulsa kwa Wafanyakazi wa umma.
Kuwa, wasibweteke kusubiri mishahara, waanze kutumia elimu walizozipata zilizoko kwenye vyeti vyao vilivyohakikiwa, kubuni njia ya kujiongezea kipato.
Kama wanavyeti halali, basi waitumie fulsa hii ya kauli ya Mheshimiwa Raisi kubadili mtindo wa maisha yao waliyoizoea.
Hii itawasaidia sana hata siku za kustaafu, watakuwa wamesha jiimarisha kimaisha.
Hii ni fulsa kwenu Wafanyakazi wa umma.
 
Ujumbe wangu kwa kila mfanyakazi mwajiriwa:
[D]Dai haki baada ya kuwajibika[/B]
 
Back
Top Bottom