Nyoka wadogo ndani na nje ya nyumba

Nyoka wadogo ndani na nje ya nyumba

Kama upo dar mjini..yaani kinondoni,migo nk na hakuna vichaka wala nyasi around..basi hiyo ni 'michezo'..hao wa kahawia nimeua sana migo..nashangaa walikua wanatokea wapi pale mapipa
 
hapana usiwe na wasiwasi ni jambo la kawaida hiyo inawezekana hilo eneo lililojengwa labda lilikuwa na mawe sana au kuna majani makavu sana yalikuwa yameoteshwa humo hivyo ni suala la muda tu wataisha ila kama kwenye msingi wa nyumba kuna mawe ni vizuri kupiga plasta kabisa na dawa wataisha hakuna uchawi hapo hata kwangu ilikuwa hivyo lakini hakuna
 
ACHA UCHAFU fanya usafi kuzunguka nyumba. fanyia usafi mazingira yote yanayozuinguka nyumba na hata kwa jilani.
usipofanya hivo, utapata taabu sana.
tatizo nadhani ni kwa jirani kuna kakichaka ila sasa yeye mbona kwake hajawahi lalamikia hili suala la nyoka!
Nyumba yake iko mbele yetu na kichaka kiko mbele yake
 
Duuhh labda ungeelezea na mazingira ya nyumba na yanayokuzunguka .

Km ni maeneo salama tu yapo wazi hamna nyasi , Basi hapo nilazima ujue nn sababu .

Ngoja waje wataalam
Kuna kichaka mbele ya nyumba ya jirani ambayo iko mbele yetu
 
Nyoka wenu ni sawa na nyoka wa kibisa, ni wale wasio na sumu. Hata hivyo nyumba yenu inakabiliwa na uchafu ndani na nje. Safisheni nyumba yenu kisha pulizeni dawa kila baada ya miezi miwili au mitatu baada ya mwaka watatoweka
ndani hakuna uchafu mkuu nje upo kwa jirani
 
Duu yani nyoka mpaka 20 unaua na bado upo tu watu mna roho zenu aisee!! Kwa nyoka mi nafikiri wapili tu ingekua nikwaheri
 
Hao ni watoto watoto msubiri mama yao utaona balaa lake, nyoka wana totolewa wengi ajabu kama ni size mmoja watoto hao
Dah itatubidi tuhame kabla mama nyoka hajaja kuwafuata watoto wake
 
Kama upo dar mjini..yaani kinondoni,migo nk na hakuna vichaka wala nyasi around..basi hiyo ni 'michezo'..hao wa kahawia nimeua sana migo..nashangaa walikua wanatokea wapi pale mapipa
Ndo hatuelewi mkuu hii idadi kwa miezi 7 si mchezoo.
 
Duu yani nyoka mpaka 20 unaua na bado upo tu watu mna roho zenu aisee!! Kwa nyoka mi nafikiri wapili tu ingekua nikwaheri
Acha Ukike Kike Wewe! kwahiyo vitoto vya nyoka uhame nyumba? tena vitoto viwili?
 
Hiyo ilishawahi nitokea , Dodoma ina ushirikina wa hivyo. Nilikua naua nyoka hadi 3 kwa usiku mmoja.
Mwanzoni nilichukulia kawaida lakini baadaye kukawa na changes sana hata za maelewano ndani ya familia.
So cha mhimu Maombi au tafuta Mchungaji aje mfanye maombi hali hiyo itakwisha na hautawaona tena!
 
Ingekuwa China wala hata tusingeona thread kama hii,
 
Kama una mtoto mchanga ndani kwako na hao nyoka umeanza kuwaona mara baada ya mtoto kuzaliwa basi ishara ya kiroho sio njema.
Ungeweka na ushahidi wa maandiko kutoka kwenye vitabu vitukufu
 
Back
Top Bottom