Nyodo zingine bwana

Nyodo zingine bwana

Kuna cku nilimkuta binti mmoja nae sister duu kinyama(maana bado nina mawasiliano nae) kwenye kamtaa flani moshi ilikua around saa 5 usiku hiv mim nilikua speed kidogo so nikawa namkuta ili nimuache. Kwanza nilishangaa uck huu alafu demu yuko mwenyew pili nilivyomsogelea nikahis kind kama analia. Nilichofanya nikumpa salamu ambayo hakujibu, na tena pamoja nabkuona hajanijibu nikamuuliza kwa upole mama uck huu upo mwenyew njiani na unalia tatizo nin(yule manzi kimya tena) dah nikamwambia ila pole kwa yaliokukuta nikavuta gia ya mguu nikaongeza speed nduki. Sasa nakaribia kukunja kona hiv nasikia nyuma mtu anakuja speed mbaya kumbe bwana mimbwa imebweka ikamtoa baru hee asije kunishikilia nilishangaa sana na kuanza kunieleza matatizo yake yote.

Usista duu sio ishu
 
Mkuu pamoja na tatizo la kujishebedua la hao masista duu na kwahiyo ni busara wakibadilika, lakini mimi naliona tatizo kubwa zaidi kutoka kwa hao manesi. Ilikuwa ni wajibu wao kutoa maelekezo yanayohitajika kwa hao wadada. Kwasababu yoyote ile, hawakutakiwa kuwa-refer nje kwa wagonjwa/wateja wenzao. Kimsingi naunga mkono uamuzi wao wa kuondoka kama feedback ya huduma mbaya kwa mteja/wagonjwa.
 
Watu wawe huru......salaam si kigezo sana eti mtu fulani anakujali/heshimu. Baadhi ya jamii hapa mkoani Arusha salam si muhimu, watu wala hawasalimiani. Wanasalimiana wanaojuana tu. Namna hii ya maisha ipo hasa sehemu za Manyara, Karatu. Salam aghalabu ni kwawanofahamiana tu. Pia Kenyans wanahii lifestyle. Ni namna tu watu wamezoea.
 
Nchi ya kipuuzi sana. Mtu hapewi huduma kisa salamu! Hao manesi hawajui wajibu wao na wamekiuka kanuni za Kazi yao. Hivi ni Kazi ya nani kutoa maelezo ya taratibu za hospitalini waajiriwa wa hospital au wagonjwa wengine?

Na nyie salamu zinawaongezea au kupunguza nini hadi mshindwe kusaidia mtu kisa salamu. Upuuuzi

Kweli kabisa mkuu. Naona kuna tatizo kubwa mahali. Management mbovu!!
 
Haaaaahaaaaa mkuu usinikumbushe yaaan kuna siku nilikuwa naosha miguu sehemu fulani hivi kwenye jiji la mwendokasi kuna mdada duu nae akaja mzuri hatari nyodo tu nyoko kwa mbwembwe hatari hakusalimia wala nini akauliza tu kaka utatumia muda gani kumaliza ? akajibiwa pale akatulia akawa anachat mi nikamsalimia (usishangae kwa sababu kuna kitu nilikipenda nikawa nakitaka ikabidi tu nijishushe ) we alininyali mpaka nilitamani nimpige kibao . tukaendelea alikuwa amevaa kimin cha rangi ya kijivu weeee mungu wangu akuwa mbali si bleed ikampata ana hahaaaa utadhani nguruwe anataka kupandwa namwangalia tu.
Nikaingiwa na imani kwa kweli maana hiyo sehemu wanaume kibao nikaona tutasemwa wanawake wote na sio yeye nikaingia kwenye mkoba nikampa mtandio nilimpa mineno ya shombo akuamini
mara dada naomba number zako ili nikurudishie nguo yako nikamwambia nimekupa bure yaani simpendi mpaka kesho japo anajitahidi kweli kunileta karibu
Wewe Cessy na ubarikiwe tu,maana hamna namna,maana tumechoka sasa na ubarikiwe tuuuu.
 
Habari za jumamosi wanajamii
Jumanne ya wiki hii nilikuwa pande hospital malaria ilikuwa inanisumbua kiaina sasa nikawa nimetulia sehemu nasubiria majibu kutoka maabara.Mara wakatokea mabinti 3 masista duu kinoma wakaja karibu na nilipokuwa nimekaa hata hawakunisalimia wakawa wametulia ila nahisi lengo lao lilikuwa kupata matibabu inaonyesha mmoja kati yao alikuwa anaumwa sasa pakuanzia ikawa shida inaonyesha sio wazoefu sana pale hospitali.Tatizo likaja waanzie wapi sasa wakawa isitoshe hawajasalimia mtu yeyote pale.Walipoingia ndani wakakuta manesi wametulia sehemu wakawaulizia wanaanzaje manesi wakawaambia nendeni nje mkaulizie utaratibu kwa wenzako uliowakuta hapo nje watakuelekeza unaanzia wap na unaishia wap.Sasa kimbembe kikaanza hawajasalimia mtu yeyoye wakawa wanajistukia kwa kuona aibu waanzaje kutuulizia maana walikuja kwa mbwembe balaa.Huwezi amini waliondoka bila kutibiwa kutokana na nyodo zao
SOMO-salamu nikitu muhimu sana hasa nyie wakina dada acheni nyodo hata ni wazuri kusalimia sio kwamba kutapoteza uzuri wako,mnaringa sana utafikiri labda mna maisha mazuri sana acheni nyodo kwa watu msiowafahamu mtakosa vitu vizuri maishani
Hospital gani mgonjwa anauliza utaratibu kwa nurse anajibiwa akaulize watu/wagonjwa nje? So unprofessional.
 
Mkuu hata mie nimeshindwa kuelewa huyu ni ME au KE
Wewe ni mtoto mzuri. Hongera sana kwa utu wako.

Ila mkuu ninachojua wewe ni jinsia ya kike, sasa mbona umemsifia sana huyo duu mwenzio na ukaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa alikuwa na kitu ambacho ulikipenda? Ha ha ha
 
si unajua watoto wa kike alisuka vizuri nilitamani aniambie amesuka wapi mkuu
 
nilipenda nywele zake kwa kweli alisukwaaa haswaaa
Sasa kama unapenda nywele nzuri za bandia(natural grown hair),si ungeniambia mimi tu?,mambo yote nafanya kwa DHL,UPS,FEDEX,hakuna uzia,halafu unaenda Boutique and Hair Salon ya nguvu hapo jirani Johanesburg,makaburu wakaset ki uhalisia,sio kwenda Sinza Shekilango kwa machangu.
 
Haaaaahaaaaa mkuu usinikumbushe yaaan kuna siku nilikuwa naosha miguu sehemu fulani hivi kwenye jiji la mwendokasi kuna mdada duu nae akaja mzuri hatari nyodo tu nyoko kwa mbwembwe hatari hakusalimia wala nini akauliza tu kaka utatumia muda gani kumaliza ? akajibiwa pale akatulia akawa anachat mi nikamsalimia (usishangae kwa sababu kuna kitu nilikipenda nikawa nakitaka ikabidi tu nijishushe ) we alininyali mpaka nilitamani nimpige kibao . tukaendelea alikuwa amevaa kimin cha rangi ya kijivu weeee mungu wangu akuwa mbali si bleed ikampata ana hahaaaa utadhani nguruwe anataka kupandwa namwangalia tu.
Nikaingiwa na imani kwa kweli maana hiyo sehemu wanaume kibao nikaona tutasemwa wanawake wote na sio yeye nikaingia kwenye mkoba nikampa mtandio nilimpa mineno ya shombo akuamini
mara dada naomba number zako ili nikurudishie nguo yako nikamwambia nimekupa bure yaani simpendi mpaka kesho japo anajitahidi kweli kunileta karibu
Safi sana kwa ujasili wako wa kumsadia alie kuzihaki..
 
Watu wawe huru......salaam si kigezo sana eti mtu fulani anakujali/heshimu. Baadhi ya jamii hapa mkoani Arusha salam si muhimu, watu wala hawasalimiani. Wanasalimiana wanaojuana tu. Namna hii ya maisha ipo hasa sehemu za Manyara, Karatu. Salam aghalabu ni kwawanofahamiana tu. Pia Kenyans wanahii lifestyle. Ni namna tu watu wamezoea.
Inabidi mjipime au msijichanganye na jamii zingine..
 
Labda kidogo mimi nipo tafauti na watu wengine....lakini mimi kwa kuwa najua kuwa tunaishi katika nyakati ambazo heshima na uungwana vinaonekana kama kujipendekezwa huwa sihangaishwi na jambo hilo.....kwa kuwa nina amini kuwa salamu ya mtu yoyote yule haina tija yoyote kwangu na kama nipo kwenye nafasi ya kumsaidia mtu huyo nitamsaidia kwa kadri ya uwezo wangu ili yeye mwenyewe aone aibu kuwa alichokifanya sio ambavyo watu wanapaswa kuishi......Bila ya shaka hata nyinyi mngetakiwa kwanza mumsaidia ili ajue kuwa ubinaadamu ni zaidi ya kuwa mlimbwende......
 
Mtu unaumwa waenda hospitali, kibongo anza kusalimia kuanzia kushoto mpaka kulia na nyumba na mbele! Bure kabisa, kwani lazima?! Ukienda hospitali kuna mapokezi, na ndio maana wapo pale, bado tunafanya mambo na kazi kimazoea sana, kupoteza muda na kulazimisha mambo ya kijinga kabisa, hao manesi wanatakiwa kupigwa chini, salaam sio lazima, hakuna sheria inayolazimisha umsalimie mtu, na wala wewe usiache saidia mtu sababu hajakupa salaam, ushamba tu huo..
 
Back
Top Bottom