kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,888
- 17,295
Ziko nyimbo ambazo Radio na TV zetu wanazipiga hewani asubuhi, mchana na hata jioni bila kujali nani anasikiliza akiwa nani wapi. Jana nilikwenda kumfuata binti yangu shuleni kumrudisha nyumbani, kwenye gari nilikuwa ninasikiliza Radio fulani, mara wakaanza kupiga music fulani humo ndani maneno yake ni "hakuna refa kitandani, ananipa raha ile mbaya, sikuachi, anavyokukurika kwenye chaga....", kwa aibu kubwa nikabadilisha station kutafuta redio nyingine lakini huko nako nikasikia "mwanaume mashine, chapa chapa chapa...., wamekosa marinda..., nikabadilisha harakaharaka baada ya kumuona binti yangu amenyamaza kimya na kuangalia pembeni kama mtu aliyeshikwa na huzuni nikabadilisha station kwenda radio nyingine nikasikilizaaaa, mwisho wake nikasikia tena "unanikuna ile mbaya tukiwa kitandani, ukirudi kwangu nakupa mhogo wa jang'ombe...." kuona hivyo nikazima radio na kuweka flash yangu ya nyimbo za zilipendwa za akina TX Moshi William, Mbwembwe, King Kikii.
Hoja yangu hapa ni wapi taifa hili tunalipeleka? vyombo vyetu vya habari vinaendeshwa na "wahuni" wasioijua jamii?. Lakini wanaosimamia vyombo hivi vya habari wako wapi, au wanasikiliza na kuchukulia hatua vyombo vinavyowasema vibaya wanasiasa tu? Mbona watoto na maadili ya jamii hayalindwi?
Hivi nyimbo zenye ujumbe wa kuhamasisha ngono kwa watoto wetu ambazo huwezi kuzisikiliza ukiwa pamoja na wazazi, watoto na watu wengine unaowaheshimu kwa mujibu wa maadili yetu hazifahamiki?