Nyimbo za dini kupigwa club hii imekaaje?

Zipigwe Tena kwa sanàà!
Tena ingependeza iwe kama kuna sehemu kule Moshi ikifikia muda ule Malaika Gabriel Alipo Mpa Habari Maria Kumzaa Yesu!
Kengele Ikigonga vilabuni wanywaji wanaachia kunywa, na kusimama na mmojawapo kuanza wimbo sala wa!; Malaika Gabriel Akampasha Habari Bikira Maria....
INGEPENDEZA
 
Kwani samaki wanavuliwa hewani, huyo DJ yuko sahihi kabisa maana watu wa huko ndio wanahitaji ukombozi zaidi kuliko hata waliopo kanisani. Kwa maandiko yenyewe yanasema kulikua na mchungaji moja akichunga kondoo wake sasa ikatokea kondoo mmoja kapotea ikabidi awaache wale kondoo wengine ili akamtafute kondoo mmoja aliyepotea
 
Kuna siku nilijichanganya club moja hapo mabonenng Johannesburg wakaweka nyimbo za dini mbili mfululizo tena wanaziimba bila hata kuelewa maana yake mwimbo wa " hakuna Mungu kama wewe" na nimeuona mkono wa bwana...nilifarijika sana ingawaje niliusikiliza sehemu sio..
hizo ngoma hadi kwa Madiba wanazijua????

Na hapa zimepigwa aisee
 
Wanazionea nyimbo za injili ila kama wana jeuri na wanajiamini wapige nyimbo za kaswida waone shoo yake.
ilipigwa moja na video yake

DVJ aliiweka nayo ina VIBE kinouma jamaa wanacheza na KANZU na kile vilemba vyekundu ila kwa macho ya gambe nliwaona kama ni Wahindi
 
Kwani samaki wanavuliwa hewani, huyo DJ yuko sahihi kabisa maana watu wa huko ndio wanahitaji ukombozi zaidi kuliko hata waliopo kanisani. Kwa maandiko yenyewe yanasema kulikua na mchungaji moja akichunga kondoo wake sasa ikatokea kondoo mmoja kapotea ikabidi awaache wale kondoo wengine ili akamtafute kondoo mmoja aliyepotea
Pamoja sana mkuu ngoja tuhubiriwe kila sehemu tukumbushwe juu ya Mungu na Wokovu.
 
Huo ni mkesha kama mikesha mingine wacha Mungu aabudiwe kwa style tofauti.....ila hakuna biti kali club au bar kama HAKUNA MUNGU KAMA WEWE 😂

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Pamoja sana mkuu ngoja tuhubiriwe kila sehemu tukumbushwe juu ya Mungu na Wokovu.
🙌🙌 Tatizo sijui ni watu au dini zenyewe zinakua biased ila ukienda kwenye ukweli watu wa namna hiyo ndio wanahitaji zaidi neno la mungu kuliko waliopo makanisani na misikitini
 
Back
Top Bottom