Nyimbo za CHADEMA Zimekaa ki-CCM!

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,976
13,626
Tarehe 8/8/ mwaka huu,niliudhuria mkutano mkubwa wa kuzindua vuguvugu la mabadiliko, almaarufu M4C hapa ifakara. Mkutano uliohutubiwa na viongozi wakuu wa chama, mwenyekiti mh Freeman Mbowe, katibu mkuu Dr Wilbrod Slaa na baadhi ya wabunge wa cdm, mmjawapo ni dogo janja, Joshua Nassari. Katika mkutano ule pamoja na mambo mengine, tuliuziwa kadi, pamoja na cd yenye nyimbo za kuhamasisha. Hapa ndo penye hoja. Nilinunua cd si kwa 7bu nazipenda hizo nyimbo,bali kuongeza mapato ya chama. Ukisikiliza nyimbo zote zinamahadhi ya zile za ccm zilizoimbwa na "dubwana" komba wa TOT. Kuanzi ile ya People's power, Slaa kiboko ya mafisadi na nyingine zote mwimbaji ana sauti ya komba. CHADEMA kama chama makini kinatakiwa kutengeneza nyimbo zenye tenzi za kimapinduzi, zinazohamasisha, zitakazn tengeneza chuki dhidi ya utawala mbovu wa ccm. Tumechoka kusikia ladha zilezile za ki-ccm, tuwe macreator na c macopister!
 
Hata mimi sipendi walivyokopi hizo sauti!!! alafu nyimbo za kwaya zimepitwa na wakati!!
 
Wewe leo umejenga chama letu kwa mawazo muafaka!! CDM tuna nyimbo mbayaaaa kwakweli!
 
Wewe leo umejenga chama letu kwa mawazo muafaka!! CDM tuna nyimbo mbayaaaa kwakweli!

mkuu umesema vema,nyimbo kiukweli ni mbaya na hazina mvuto...kwa nini wasiwatumie watu kama Mrisho Mpoto "mjombo"(hata kama c yeye) watu kama Roma mkatoliki(hata kama c yeye) ghani zao zinaeleweka kiurahisi, zinafikisha ujumbe, hazichoshi. M2 kama mh Sugu yupo wangemtumia kutengeneza nyimbo zenye ujumbe unaopenya kwenye roho,nafsi, hata moyoni. Watengeneze na video zake, mfano tukizungumzia kashfa ya ufisadi wa richmond tuonyeshe m2 mwenye mvi,c lazima kuonyesha sura EL,na ujumbe utafika.
 
Tupe ladha unayoona ya kimapinduzi mkuu.

mkuu umeninukuu vibaya, sijasema ladha ya kimapinduzi,nimesemaa tenzi za kimapinduzi, mfano ANC kule Afrika ya kusini,walikuwa wakitumia nyimbo kama hizo kupinga ubaguzi wa rangi. Bob Marley anamusic mingi tu ya kimapinduzi...mziki kama get up stand up siyo wa kimapinduzi huo. Labda mimi ndio sielewi!
 
Kweli hata mimi nilizisikia nilipokuea mtwara... Bt ingekuwa vema kama mngependekeza sound/radha ya nyimbo mpya.
 
mkuu umeninukuu vibaya, sijasema ladha ya kimapinduzi,nimesemaa tenzi za kimapinduzi, mfano ANC kule Afrika ya kusini,walikuwa wakitumia nyimbo kama hizo kupinga ubaguzi wa rangi. Bob Marley anamusic mingi tu ya kimapinduzi...mziki kama get up stand up siyo wa kimapinduzi huo. Labda mimi ndio sielewi!

Ndio nasema tupe moja unayoweza ili iwe mfano.
 
Back
Top Bottom