Nyerere's legacy failed 100% (economically)

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
Nyerere legacy failed 100%.

1. Kuchagua sera za ujamaa lilikua kosa lake kwanza.

2. Kuchukua viwanda, Shule, taasisi na kuzitaifisha lilikua kosa kubwa.

3. Kuanzishwa vijiji vya ujamaa kwa kuwakusanya watu kwa mkono wa chuma was a great mistake. Watu walipoteza mali, wengine kushindwa kucope na mazingira mapya ya kulazimishwa.

4. Kuzuia mfumo wa vyama vingi na uhuru wa kukosolewa na zikabaki zidimu fikra za mwenyekiti. Here we are.

5. Kutumia rasilimali za nchi kukomboa mataifa mengine bila mkataba wa kurefund izohela baada ya Uhuru. Check Mozambique Na South wanavotufanyia wamesahau tuliyowafanyia so bora tungekuwa kama Marekan hatumii fedha zake katika vita bila return .

6. Kushindwa kuzuia rushwa serikalini na katika mashirika. Mtu anapewa umeneja wa kiwanda au taasisi anaiba anafilisi kisha anahamishwa toka sehemu moja kwenda nyingine. Ilipaswa afikishwe mahakamani na afilisiwe. Hicho ndicho kimeigwa mpaka leo.

7. Alichangia kuendelea kwa katiba inayotuumiza hii leo. Hakuamini nguvu ya upinzani, aliamini katika chama chake pekee. Ilifika anasema rais bora atatoka CCM pekee why?

Tunapaswa kumpima mtu economically kujua alifaulu ama alifeli.

Uchumi wa Tanzania upo chini sana kwasababu ya sera zetu tulizoamua kuingia bila referendum kujua kama watu wanaafiki ama la.

Siamini kama kuna haja hiyo ya kucelebrate life ya Mwl. Katika context ya economy.
 


Na Magufuli's presidency is a success story 100%, hutaki hama nchi!
 
Ndiyo tunasherehekea kila mwaka hata kama wewe na ukoo wako hamtaki.
 
yan umeandika km shairi la wahenga,
umeshindwa kunishawish,
hv unategemea Nyerere aweke concept ya vyama ving mwaka 1983 ?! ili uone yuko sawa,
rudi shule dogo, huku patakuzeesha zaid ya ss..[emoji39]
 
Na Magufuli's presidency is a success story 100%, hutaki hama nchi!

Wa kuhama nchi ni yule ambaye hata watu watoe mawazo yao. Huyo ahame dunia maana watu wanatoa mawazo yao tangu dunia imeumbwa na hawataacha kwa namna yoyote.
 
Tuna Imani na nyerere oyaa oyaa oyaaaa, nyerere kweli kwelii kweli kweli nyerereeee, hata kama hupendi, ziba macho na masikio.
 
Kuna watu.wengineo wachawi ,unaanzaje.kumkosoa nyerere wakati wanaopaswa kukosolewa hamuwakosoi
 
I am concerned about your mental health, for bringing up this thread.Nyerere was and will be remembered as the man of the people. He may have fallen short on somethings, but he delivered most of the good things that makes us call ourselves Tanzanian. Thank you.
 
Kwenye sera za uchumi alifeli tena sana tu na hata yeye mwishowe aligundua makosa yake, serikali haipaswi kufanya biashara inapaswa ku-regulate na ku support ukuaji wa biashara kisha ikusanye sehemu ya faida kama kodi.

Pia serikali haiwezi kutoa huduma zote za kijamii kwa ubora ni lazima i support na kuruhusu sekta binafsi zinazotoa huduma kama afya, elimu na fedha (benki). Yeye alitaka vyote viendeshwe na serikali mwishowe viliishia kufa tu.

Huyu wa sasa nae ameanza kuingia kwenye ka mtego ka kutamani serikali i control kila kitu, sera za namna hiyo mwisho wake ni unajulikana kabla hata haujafika.
 
Sababu ya kutoa povu ni nini! Mitume wanakosolewa seuze nyerere! Alikuwa binadamu kama binadamu wengine, na ni ukweli usio na shaka alifeli kiuchumi tena vibaya sana. Alirithi viwanda vinafanya kazi kutoka kwa wakoloni, wakati anang'atuka viwanda vilikuwa hoi bin taabani. Nyerere will always remain a true statesman but kwenye uchumi alifeli pasina shaka.
 
Nyerere's legacy may have had some failures, the man himself acknowledges that.

But beware of people who throw around "100%" easily with no qualification.

Those who know what it means do not throw it around like that, those who do, do not know what it means.
 
Wakati wake hakuchagua market economy. Si sawa kumhukumu kwa vigezo vya market economy ya sasa.
Tafuta marking scheme nyingine!
 
Ndiyo lakini bado tunampenda hivyo hivyo na hatujali maneno yenu ya majungu.
Nani kakwambia simpendi nyerere?! huwezi kukana kweli kwasababu ya mapenzi. Ukweli utabaki kuwa ukweli. Kama kupanga foleni kusubiri duka la SUKITA au TRC lifunguliwe ilikuwa ni fahari inabidi upimwe akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…