Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Mkuu wangu,

Mie kijakazi wako nimeishia darasa la nne la zamani.
Samahani kama nimekukwaza kwa kujadiliana na wewe mwenye upeo mkubwa. Ila naomba usichoke kunisaidia kunifundisha mkuu wangu.

Nikisema China na Urusi nina maana nchi za kikomunisti au kwa lugha iliyozoeleka nchi ya kijamaa. Stalin alikuwa kiongozi wa Urusi (iliyoungana)

Nikisema angeleta wageni nina maana angeleta wageni kutoka magharibi (kwenye ubepari) maana mabepari ndio wanaweza kuendesha biashara yenye kuleta faida.

Mambo ya SAS na JK mie hayanihusu maana sio mada iliyopo mezani.

Nawasilisha mkuu wangu.

Ndimi,
 
Hayo niliyategemea kutoka kwako na sivinginevyo, pole bi mkubwa!
 

Na kimsingi kuna dhana ambayo imesemwa sana na mie nimeishuhudia mara kadhaa..JK ni mzito kutamka Mwl kama baba wa Taifa,uwa anaishia kusema...mzee wetu,mwl,muasisi wa taifa hili nk...nadhani realy there is something wrong to this generation of JK and his government...na hawa akina Faizafoxy ni kama mbwa maana mfuga mbwa mwenyewe ndio chanzo cha tatizo....
 
 

Hii haihusiani na thread iliyopo mbele yetu otherwise anzisha ya kwako inayojitegemea kama unataka coments. Naona umekurupuka ukastukia umeingia choo cha kile.
 
So wewe mzazi wako wa kiume mwenzetu unamuita nani? Make huwezi kumuita baba kufanya hivo utakuwa unatukuza ukatoliki. Leo nimeona faida nyingine ya jamvi hili ni ; Yaani wenye akili na wajinga wanajileta wenyewe. Pole pole twaweza kujua taifa lina mbumbu wangapi. Long live JF
 
Hii imekaa vizuri sana na ni darasa zuri sana. Mbali na kuwa ni Rais wa kwanza wa Tanzania, mazuri ya Nyerere ukiamua kuyatafuta utayapata mengi sana, ukiamua kuyaandika utaandika na hata ukitaka kufundishia utapata mambo mengi sana ambayo yanaweza kutoa msingi mzuri kwa nchi yetu na Africa kwa Ujumla. Sidhani kama kuna kiongozi yeyote Africa aliyefanikiwa kwa kiasi cha Nyerere kuweza kuishi na kusimamia kile alichoamini ni bora kwa mwafrika. Ukitaka kuandika historia ya viongozi wengi utajikuja unaaandika historia binafsi, lakini historia ya Nyerere ni ya nchi, na Africa kwa ujumla.

Kulinganisha hili na mpira wa kulipwa au eti angechukua wakoloni tuliowaondoa ili waje kutuendeshea nchi ndio inaonyesha wanaokejeli ni wavivu wa kusoma hata yale uliyoandika hapo juu, ukiachilia mbali vyanzo vingine vya habari.
 
 
Dada Mdogo FaizaFoxy (nasema hivyo kwa sababu nina uhakika mimi ni kaka yako mkubwa kiumri):-

1.Ni hivi karibuni nilikuwa Pakistan. Unapotua uwanja wa ndege Islamabad unakaribishwa na bango lisemalo "Welcome to the Islamic Republic of Pakistan". Lakini licha ya nchi hiyo kuwa ni ya mfumo wa kiislamu bado wanamuita kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo, Muhammad Ali Jinah, Baba wa Taifa "Baba-e-Qaum (بابائے قو&#1605😉".

2. Na sio Pakistan peke yake kati ya nchi za kiislamu ambako viongozi wamepewa wadhifa wa Baba wa Taifa. Kwa mfano Uturuki, Mustafa Kemal Atatürk (Atatürk = Great Father of the Turks). Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan wa United Arab Emirates (والد الأمة = Waalid Alamat) na pia Ibn Saud of Saudi Arabia ( والد الأمة = Waalid Alam)

Kwa hiyo nadhani sio kila mada ni lazima uchangie kwa mtizamo wa kidini. Waswahili husema ujanja mwingi mbele giza!
 
 

well said!
 
Hadi sasa, wachangiaji wengi, zaidi ya asilimia 90 wanakubaliana na hoja kwamba heshima ya Baba wa taifa haina mwingine zaidi ya Mwalimu Nyerere; Kinachoendelea sana sana katika mjadala ni juu ya Ubora wa Sera zake, akifananishwa na marais waliomfuata. Katika mjadala wa namna hii, tusisahau kwamba Nyerere ni Rais pekee aliyeendesha uchumi kwa sera zilizoandaliwa na watanzania wa ajili ya Maendeleo ya watanzania. Sera ya Ujamaa na Kujitemea zilikuwa home grown, hazikuwa za kushinikizwa na mataifa au taasisi za nje.

Kuanzia mwaka 1985 alipochukua nchi Mwinyi, Marais wote wamekuwa wanatekeleza Sera na Maamuzi ya WorldBank, WTO, IMF, kama mashatri ya kupata misaada; Wakubwa wa OECD countries wamewapa hawa mapacha watatu dhamana ya kusimamia interest zao, that's how ukoloni mamboleo is working at present. Kwahiyo hawa mapacha watatu wakati wote, kwa kupitia misaada na mikopo yao, wanashinikiza kwa nchi maskini, sera ambazo zitawanufaisha OECD countries, sana sana kwenye sekta za madini, mafuta na mazao ya kilimo (sio ya chakula). Pia misaada yote na fedha zote wanazotoa wanataka ziende kwenye sekta ambazo zinafanya uchumi wetu uwe efficient for exports, mfano miradi ya barabara, lengo sio ili kijiji A na B viweze kufanya commerce kirahisi zaidi au kuwa na mawasiliano bora zaidi, bali kuongeza efficiency in terms of movement of cash crops na madini, from mikoani, kuja bandarini DSM for exports. Nia ya wakubwa hawa is to make sure that Sub Saharan Africa remains the rural back yard for Europe and North America. Bajeti zetu miaka yote zinapitiwa na kuhakikiwa na wakubwa hawa, wao ndio wanaamua nini iwe priority kwa mwaka ujao wa fedha. Huwa wanaamua iwe elimu, Kilimo, Miundombinu, etc ka jinsi wanavyotaka. Ushahidi huu upo hate kwenye tafit mbali mbali - google ‘Aid conditionality' to poor countries.

Kwa miaka kadhaa sasa, wakubwa hawa wamerudisha mambo mengi ya Mwalimu baada ya kuwa criticized sana juu ya sera zao ambzo zimemfanya mtanzania kuwa maskini zaidi. Mfano wanajitahidi sana kurudishia serikali maamuzi juu ya kuwekeza kwenye elimu – e.g; shule za kata sio ubunifu wetu, sisi ni watekelezaji.

Kwahiyo tumpime Nyerere kama Rais mwelekezaji dhidi ya Rais Mwinyi, Mkapa, na Kikwete kama marais watekelezaji. Hata kama mwaka 1985 asingekuwa Mwinyi Rais bali Amina, Peter, Rashidi, au veronica, Rais huyu angeitwa jina lile lile Mzee "RUKSA" kama angekuwa Peter au Rashidi; au Mama "RUKSA" kama angekuwa Amina au Veronika.
 
 

Brilliant point.
 


Mkuu ungepenyezea Mkuu wa Kaya habari hii wakati wa sherehe za uhuru wa Tanzania Bara/Tanganyika juzi 9/12/2011. Ingependeza kweli.

Vinginevyo, naunga mkono hoja.
 
hakika wewe ni great thinker!
sasa ngoja tusubiri mitazamo ya kina FF,RITZ,MS,REJAO ili tujue nao wana maoni gani
Nilikuwa najiuliza ni nini chimbuko la hii tabia iliyoanzan siku hizi za karibuni ya kumchafua Mwl. J.K. Nyerere. Sasa nimeanza kuelewa kidogo na itakuwa vizuri kufuatilia na kujua hao wanaofanya hivyo wanafanya kwa sababu gani na kwa faida ya nani hapo baadae. Hii campaign itagonga mwamba tu kwa sababu huwezi kujisafisha mwenyewe wakati wewe u mchafu kwa kutaka kumpaka mwingine matope.
 
Mchambuzi,
Sasa kama mpo mnaoelewa kinachoendelea kwa kiwango kikubwa namna hii, kwa nini mko kimya? Hayo unayosema ni maelekezo toka nje watawala wetu wanayaorodhesha kama mafanikio kila uchao na wanataka tuamini hivo. Ingieni angalau Bungeni mpaze sauti huko zenye kuleta tija na mabadiliko ya maana.
Badala yake wasomi kama akina Zitto wanajielekeza kwenye mambo ya kuwapa umaarufu wa haraka kama posho. Bunge lijalo la January nadhani watajadili ndoa za jinsia moja!
 
Mchambuzi, nimekuvulia kofia. Kuna swali ningeomba yeyote mwenye kujua anisaidie: Kuna kazi fulani tulikuwa tunafanya wiki chache zilizopita, kuna point tulilazimika kupata kanda za taarifa za habari na magazeti ya miaka ya '70 na 80. Baada ya kumaliza navyo, nilitaka kupitia karibu kila kitu katika magazeti na taarifa hizo, pamoja na mengine mara kwa mara unasikia/soma kitu kama hiki...'Rais wa JMT amemstaafisha kwa manufaa ya umma aliyekuwa meneja/mkurugenzi wa .....' Je hii ina uhusiano wowote na hiyo inayosemwa kuwa walioharibu hawakuchukuliwa hatua?! Mzee mmoja ameniambia kuwa huko kustaafishwa kwa manufaa ya umma kuliwakumba wengi.
 
FP
Ukitazama mantik nzima ya vijiji vya ujamaa iikuwa nzuri na inasimama mpaka leo. Lakini kuna baadhi ya maeneo kulingana na utaratibu wao maisha.( eg ufugaji 100%) hawakuwa na utamaduni wa settle. So hilo iuwa ni tatizo moja Lakini failure ya vijiji vya ujamaa sehemu chache haiwezi kufunika sucess ya vijiji vya ujamaaa sehemu kubwa ya Tanzania


Unapokuwa na uhaba wa resoruces (wich is always the case) lazima kuna kitu kifanyike (organisation) Sasa kama unalaumu vijiji vya ujamaa ebu fafanu ungefanya nini wakati cha tofauti japo kuweka shule mbili za primary kwenye jamii zilizotawanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…