Ukitoa hoja uko naye. Watu wanailaumu CCM ya miaka karibu 25 ilikuwa chini ya Nyerere. Viwanda vilikuwa vinakufa tayari kwa kukosa malighafi na vipuri. Maisha yalizidi kuwa duni na uhuru wa vyombo vya habari haukuwepo.inaonekana wewe ni mjukuu wa hao "watanzania wenye asili ya asia" pole sana.
Sawa mkumbushaji, kwahiyo aliachaje Urais. Point hapa ni kuachana na dhana kuwa aliondoka kwa hiari bali ni kushindwa kuongoza nchi kulimng'oa. Foleni za kaunguza, sukari na sabuni za kuruka, foleni za misaada ya vyakula etcSijaelewa point yako hapa nini sasa? Kwanza kwa taarifa yako NENO kung'atuka hakulitamka wakati anaachia URAIS, neno hilo alilitamka wakati anaachia uwenyekiti wa ccm mwaka 1987! Usichanganye madesa.
Nyerere aliiacha nchi ikiwa na uzalendo wa hali ya juu, nakumbuka Enzi hizo tunasoma shule ya msingi walimu walikua wanajitolea kutufundisha hata Jumamosi bila kudai malipo yoyote ya ziada, madaktari hali kadhalika, mgonjwa anapokufa mbele yao unawaona wanavyosikitika. Madereva wa makampuni kama KAMATA, KAUMA, KAURU, RAILWAY (wengi walitamka Relwe) walikua wanajiona wanalo deni kufikisha mizigo na abiria sehemu husika on time ingawa barabara zilikua mbovu sana. Kwenye vita ya Idd Amini ambayo tulilazimishwa kupigana, wananchi pamoja na wanajeshi walionesha kwamba kweli wanaipenda Tanzania yao, wapo watu waliotoa Ng'ombe, vyakula na hata watoto wao (hawakua wanajeshi) kwenda kupigana na IDD Amini. Nyerere pia aliiacha watoto wakiwa wanasoma BURE from shule za vidudu (sasa chekechea) hadi nafasi ya u profesa bure na matibabu nayo bure. Hospitali za kulipia zilikuwepo (za makanisa na zilijulikana kama hospitali za mesheni). Kwa upande wa uchumi hali iliaanza kua mbaya hasa mara baada ya vita vya IDD Amini lakini kabla ya hapo mambo yalikua safi sana. Kitu kimoja kilicho haribu sana uchumi (Vita ikiwa ni sababu) ni ile sera ya kulinda viwanda vya ndani na hence kuzuia bidhaa kutoka nje zisiingie kwa wingi, uzalishaji wa viwanda vyetu kama vya Sukari, Sabuni, Mafuta ya kula na hata TIPER ulikua mdogo kuliko mahitaji ya Watanzania na huo ndio ukawa mwanzo wa foleni kwenye maduka ya Ushirika, Duka la Kaya na RTC. Mwinyi yeye akafungua mipaka na hivyo bidhaa kua bwerere madukani but ukawa pia ndio mwanzo wa viwanda vingi kufa. Remember, dunia ya wakati huo ilikua ina policy 2 tu za uchumi, is either uwe Bepari au Mjamaa; mwanzoni mwa miaka ya 90 Ujamaa ukafa duniani na hicho ndicho kilichotokea. Hayo tu kwa UFUPI.Sawa mkumbushaji, kwahiyo aliachaje Urais. Point hapa ni kuachana na dhana kuwa aliondoka kwa hiari bali ni kushindwa kuongoza nchi kulimng'oa. Foleni za kaunguza, sukari na sabuni za kuruka, foleni za misaada ya vyakula etc
Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.
Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.
Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.
Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.
Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
Sawa mkumbushaji, kwahiyo aliachaje Urais. Point hapa ni kuachana na dhana kuwa aliondoka kwa hiari bali ni kushindwa kuongoza nchi kulimng'oa. Foleni za kaunguza, sukari na sabuni za kuruka, foleni za misaada ya vyakula etc
Una haki ya kutoa mawazo yako, Lakini baadhi yetu, na tunakuthibitishia kuwa tupo wengi, Mchango wa Nyerere kwa nchi hii haupimiki. He is the father of the nation. Nyere alileta umoja wa kitaifa, mtu unaweza ukaenda Tabora ukitokea Songea ukaishi bila matatizo. Alijenga taifa ambapo sasa tunajiita watanzania, aliweka misingi mizuri ya uchumi kwa kuleta viwanda vinavyoongozwa na watanzania wenyewe. Watoto wa maskini walisoma bure mpaka chuo kikuu. Mimi nilisoma wakati wa Nyerere na mzee wangu hakuwa na uwezo mkubwa. Nilisoma sekondari bure, nilisoma chuo kikuu bure... Kule Mlimani Enzi hizo tukienda cafeteria kulikuwa na mabomba ya maziwa..mtu unakunywa 'tani' yako. Nikiwa sekondari tulikuwa tunakwenda na sanduku tu na nguo zako. tulikuwa tunapata vitabu vyote bure pamoja na madaftari bure. Kulikuwa hakuna wizi wa vitabu kwani kila mtu ana vitabu husika. shuleni tulikuwa na swimming pool. tunaogelea na kujidai. Shuleni tulikuwa na vviwanja vitatu vya mpira wa miguu, kiwanja kikubwa cha riadha, viwanja vya netball, viwanja vya volleyball, hockey na kadhalika. Tulikuwa na indoor games nyingi tu. Wakati wa likizo tukiwa sekondari tulikuwa tunasafiri kwa kutumia travel warrants na tunapewa chakula cha njiani. Ajira ilikuwa nje nje, makampuni na mashirika mengi. Uzalendo ulikuwa mbele.Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.
Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.
Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.
Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.
Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
Uko sahihi, tatizo kuna watu wananzisha mada juu ya jambo la kusimuliwa. Sasa hasara gani kwa operation vijiji, lengo ilikua huduma za jamii kuzifikisha kirahisi, Shule, maji, barabara, Afya na huduma nyingi ambazo ni mahitaji ya jamii ambazo ni ngumu kumfuata mtu mmoja mmoja.Sijaelewa point yako hapa nini sasa? Kwanza kwa taarifa yako NENO kung'atuka hakulitamka wakati anaachia URAIS, neno hilo alilitamka wakati anaachia uwenyekiti wa ccm mwaka 1987! Usichanganye madesa.
Can you imagine..unapewa uongoze nchi iliyokuwa koloni la mwingereza..huna uzoefu wowote wa kiutawala zaidi ya kuwa mwalimu na mpigania uhuru tu...huna hata wasomi wa kutosha. waliowengi elimu zao ni kama za akina Bibi Titi..kajaribu hata kuunda Jamhuri ya Muungano bila hata ya kumwaga damu ..Niambie ni nani anaeweza kuyafanya haya katika kizazi hiki cha dotcom.Ubinadam Wa baba wa Taifa hauna tofauti na ubinadama wa binadam yeyote wa leo ila mchango wake kwa Taifa hili ni mkubwa sana, ana mazuri yake meeeengi sana aliyoyafanikisha na hakika tunapaswa kujivunia sana kwa kua na baba kama huyu, pia kuna mambo aliyoshindwa kuyatekeleza kwa ubinadam wake na hatupaswi kumlaumu ama kutungia hoja maana hata tukipewa leo hayo majukum hatutaweza kuyakamilisha Asilani. Alienda kwa amani na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina.