Bonnie1974
JF-Expert Member
- Mar 19, 2008
- 407
- 16
1.Kuporomoka kwa Simba na Yanga ni kwa sababu zimeshindwa kubadilika kutokana na kubadilika kwa nyakati.Investment zilizofanyika wakati ule kama ni zile ghorofa za msimbazi na ile ya Jangwani almost ni zilezile.No more investments.Na hata hizo zilizopo vilabu vinashindwa kuzitumia na kusubiri fadhila ya kina Dewji na Manji respectively.GT has a point ambayo labda kuieleza inakuwa shida. Nadhani anachojaribu kueleza ni madhara kwa mpira wa Tanzania yaliyotokana na Serikali kuingilia uongozi wa vilabu miaka ya 70-80.Wadau mnakumbuka jinsi Kambarage alivyowafurumua Tambwe Leya (Yanga) na Nabi Camarra(Simba) kwa PI? kwa nini alifanya hivyo wakati hao walimu walikuwa ni wazuri sana waliotengeneza timu nzuri? Mnaukumbuka mtanange mkali wa Yanga(chini ya Tambwe) vs Kwara United na Simba(chini ya Camarra) vs Hearts of Oak?Hizo ndo zilikuwa Simba na Yanga bwana! Nakubaliana na GT ilikuwepo namna,wataalam wa historia tupeni analysis,hivi vilabu havikuporomoka bure ati!!!!!!!!
2.La Pan Afrika kusambaratishwa kwa sabau za kisiaisa ni debatable.
3.Kuhusu maendeleo ya soka kwa ujumla wake, tunakumbuka ni wakati huo, kama sera ya taifa ya michezo,kila shirika la umma lilikuwa na timu ya soka.
Tunakumbuka Tumbaku,Pamba,Sigara,Pilsner ya Arusha(NDOVU),Pilsner ya DSM,Mwadui Shinyanga,RTC Kigoma,RTC Mwanza,RTC Kagera kuzitaja chache.
Sera ile ilipanuka mpaka kwenye mashule.Michezo mashuleni ilitiliwa mkazo.Tumepata kuwa na wachezaji wazuri ambao wametoka kwenye mashule.
Michezo ilikuwa kila mahala.
Kama si michezo, wewe unapenda dansi, basi kulikuwa na bendi mfano polisi,bima n.k
Nyerere alifanya sehemu yake ambayo mpaka kesho aliyofanya yanaonekana hata kama mtajaribu kuyafuta.
Tatizo ni kwamba hamwezi kufuta aliyofanya kwasababu ALIYAANDIKA KWA WINO siyo penseli.ZAIDI MTACHAFUA KARATASI.
Msihangaike kufuta hizo kurasa za Mwalimu, tatizo karatasi zetu kama taifa ni chache mno,tunaweza kukosa pa kuandika.
MNACHAFUA DAFTARI LA TAIFA,SIO LENU HILO watoto wenu watasoma nini?