Nyerere alivyoiua timu ya PanAfrican | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere alivyoiua timu ya PanAfrican

Discussion in 'Sports' started by Game Theory, Mar 30, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Juzi nimepita pale kabuni na nikasikitishwa sana na hali tuliyonayo na makundi yaliyo oongezeka pale ..lakini mkitaka kujua nani aliiua mpira wa miguu Tanzania na aliyepeleka kua vilabu kama Pan African basi mchawi wetu si mwinginebali ni Nyerere kupitia swahiba wake Gama Abdel Nasser wa Egypt ambaye alimpa technique ya kutulazimisha kuwa kila kiongozi apitishwe na UMOJA WA VIJANA matokeo yake watu wa ajabu ajabu leo utashangaa kuwaona wanataka kuongoza vyama vya michezo hapa Nyumbani
   
  Last edited by a moderator: Mar 30, 2009
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii habari imekaaje? Sijaelewa kitu hebu nisaidiwe!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Game Theory,
  Mkuu hata mimi sijakuelewa.. unazungumzia club ya mpira ya PanAfrika?..sasa vipi na Nyerere tena! mbona nakumbuka ndio wakati walikuwa mabingwa 1983 kabla Nyerere hajaachia ngazi na kwa miaka minne yote toka 1979 hadi 1983 walikuwa juu kichizi wakiogopwa Afrika nzima..

  Hata hivyo nifahamishe zaidi kuna siasa gani zilitumika maanake hata mimi mwenyewe nilikuwa Shabiki wa PanAfrika..
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Wewe Yanga tu. Ulikwenda Pan kwa sababu Yanga walikuwa vilaza kandamili.
   
 5. K

  Karandinga Member

  #5
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Useless post!!
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  yaani nimesoma mara mbili mbili siilewi......GT siku hizi madeni mengi rent na makablasha mengi kadata......
   
 7. RR

  RR JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  GT,
  I guess you were in a rush...please come back and say what you wanted to say.
   
 8. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #8
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sema mtani wangu wa jadi,
  Naona GT kabwaga nyuzi kisha kaingia mitini!
  Ujumbe haueleweki kamwe!
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  GT has a point ambayo labda kuieleza inakuwa shida. Nadhani anachojaribu kueleza ni madhara kwa mpira wa Tanzania yaliyotokana na Serikali kuingilia uongozi wa vilabu miaka ya 70-80.Wadau mnakumbuka jinsi Kambarage alivyowafurumua Tambwe Leya (Yanga) na Nabi Camarra(Simba) kwa PI? kwa nini alifanya hivyo wakati hao walimu walikuwa ni wazuri sana waliotengeneza timu nzuri? Mnaukumbuka mtanange mkali wa Yanga(chini ya Tambwe) vs Kwara United na Simba(chini ya Camarra) vs Hearts of Oak?Hizo ndo zilikuwa Simba na Yanga bwana! Nakubaliana na GT ilikuwepo namna,wataalam wa historia tupeni analysis,hivi vilabu havikuporomoka bure ati!!!!!!!!
   
 10. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Pan Africa Walikuwa Mabingwa 1982 sio 1983 Rekebisha Hapo Na kwa Kuongezea Wao ndio mabingwa wa awali wa iliokuwa LIGI KUU YA MUUNGANO, msimu huo wakiitwa mataji mawili Ubingwa wa bara na wa Muungano Wakisaaidiwa saana na uongozi Chini ya Marehemu Alhaji Mangara Tabu Mangara,Shiraz Shariff wacahezaji Mahiri adolph Rishard,Peter Tino(aliewaua Yanga)Abdalah Burhan,Ali Katolila,John Faya,Gordian Mapango,Jaffar Abdulrahman,Salum Carlos mwinyimkuu,Idd Msaka(Ali Yusuph)Ibrahim Kiswabi,Jellah Mtagwa,Leodigar Tenga,Mohammed Yahya Tastao,Doto Ruta Mokilli,Mkweche,Ngulungu nk.
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bila kumsahau Juma Pondamali "Mensah" golini!
   
 12. M

  Mundu JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nyerere alipenda michezo lakini hakupenda kashfa pia.. nakumbuka Taifa Stars ilienda kucheza Sudan halafu vijana wetu walicheza vifua wazi kisa jezi zilisahaulika Dar. Naye alikuwepo pale uwanjani Khartoum (kama sikosei).

  Hakutaka aibu tena ya kujishughulisha na michezo ya majukwaani hadi anastaafu... Akajirudia kwenye mchezo wake wa Bao!!!
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hujakosea, ila hiyo aibu aliitaka mwenyewe kuweka watendaji wasiowafuatiliaji, kwa iliyokuwa serikali yake.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  GT is exercising his right to be a senile "eldery statesman".

  Kuna wajomba wajomba fulani wakubwa na kila mtu katika familia anawajua, waliteeesa sana zamani, lakini wameishia kulosti labda mipombe etc, hawakosi cha kusema.

  Sasa wanafikiri kwa kuwa walikuwa relevant siku za nyuma, basi wataendelea kuwa relevant hata kwa kutupa post za kivivu zisizo na kichwa wala mguu.
   
 15. U

  Umushoshoro Senior Member

  #15
  Apr 1, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hamuwezi kumuelewa GT kama hamjui historia ya Yanga na Pan Africa.

  Nyerere alikua yanga damu,na aliitumia vyema kujiimarisha na kujitanua kisiasa.

  Kupasuka kwa Yanga,kulipelekea kuundwa kwa Pan African Football Club

  Hawa wengi walikua watoto wa Mjini Dar,wasomi,wafanya biashara,wakurugenzi na mameneja serikalini na kada fulani ya watu wajanja ambao wanaweza kukufanya uamini kua usiku ni mchana!

  Tukio hilo lilizua hofu ya chini kwa chini kua kundi hili laweza kupunguza nguvu ya chama tawala likiachiwa huko mbeleni.

  Naam kazi ikaanza,wakapandikizwa usalama wa Taifa huko matokeo yake timu ikawika kwa miaka 10 ya mwanzo tu.

  Baadhi ya wajanja na wazito wa Pan Africa walikua:-

  1.Al-haj Omar Muhaji(Waziri wa zamani mambo yandani)
  2.Sammy Mdee
  3.Shiraz Sharrif
  4.Kitwana Kalima
  5.Mangara Tabu etc etc

  Kwa hiyo Nyerere aliona akiwaachia hawa watapanuka nchi nzima na kumwaga upupu
   
 16. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Kwa hiyo kwa miaka 10 mizima aliiacha iwike?? Kwa jinsi tunavyomjua Nyerere, Si angeweza hata kuizima baada ya Msimu Mmoja tu na mtu yoyote aifanye fyoko?? Why leave it for Ten Years???
   
 17. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Sahihisho Dogo tu, Mkuu. Hii ilitokea hapa hapa kwenye uwanja wetu wa Taifa (Uhuru!) kati ya mwaka 1970 ama 71 wakati wa sherehe za Uhuru a.k.a 9 Disemba!
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  GT,

  ..hivi Pani haikufa kutokana na ukata na uhuni wa wafadhili wake kama Dewji?

  ..ilifika kipindi mpaka Majimaji ya Songea wakaiba wachezaji toka Pani.

  ..wachezaji ninaowakumbuka kusaidia kutwaa ubingwa wa Tanzania ni hawa hapa:-

  ..1.Ally Yusufu 2.Mohamed Mkweche 3.John Faya 4.Rashidi Iddi "chama" 5.Jella Mtagwa

  6.Salum Mwinyimkuu "Carlos" 7.Abdala Burhani 8.Hussein Ngulungu 9.Ali Katolila

  10.Mohamed Yahaya "Tostao" 11.Peter Tino

  ..Leodgar Tenga "msomi", na Mohamed Rishard "Adolf", walikuwa wameumia wakati huo. miaka hawa jamaa wanacheza ilikuwa ukiumia goti basi ndiyo mwisho wa career yako.

  ..Juma Pondamali,Jafari Abdulrahmani, na Gordian Mapango, walikuwa wamepoteza nafasi zao ktk kikosi cha kwanza.
   
 19. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  This is not JF tunayoifahamu
  Unaposema aliua PAN AFRICA unatakiwa kueleza alifanya mambo moja, mbili, tatu then tunajadili.
  Wazee mnashusha hadhi ya jamvi.
   
 20. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Now you are talking.
   
Loading...