Nyerere alikuwa anatisha bwana!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Salamu wanajamvi!
Ngoja niwasogezee kisa hiki cha kweli kabisa kilicho mkuta jirani wa miaka hiyo enzi za Nyerere.Huyu jirani yangu alikuwa ni KATIBU TARAFA KWA MUDA MREFU.Mwanzoni mwa miaka ya 80 Nyererealiwapeleka makada kadhaa Nchini Yugoslavia kwenda kujifunza uongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya chama na serikalini.Baada ya miezi sita wakarudi, wakaendelea na majukumu yao ya zamani.

Baada ya miezi sita hivi huyu jirani yangu akaitwa aende Ikulu tarehe aliyo pangiwa bila kukosa.Akapata wasiwasi mkuu huku akijiuliza imekuwaje yeye mpaka aitwe ikulu kwa agizo hilo kuu la bila kukosa?

Akaomba ushauri kwa rafiki yake wa karibu.Yule rafiki yake akamwambia, unajua dunia siku hizi imeharibika sana, usikute kuna adui yako kapeleka taarifa kuwa unafanya biashara ya meno ya Tembo, maana na mimi nimesikia watu wanateta mahali! Yule Katibu Tarafa akaitikia inawezekana maana binadamu kwa kuoneana kijicho huwawezi.Siku ya kwenda IKULU ikawadia.Mapema asubuhi akafika ofisini, akakaribishwa ili asubiri kuitwa aingie.

Zamu yake ikafika,akaitwa akaingia. kwa mbali akaona Nyerere anavua miwani ili amuone vizuri, akaingiwa na hofu kuu! Baada tu ya salamu yule jirani yangu akaanza kujitetea akasema,Unajua mkuu, mimi biashara ya meno ya Tembo siijui na wala sijui wanauzia wapi! watu tu wameamua kuniharibia kazi na kukuletea wewe taarifa za uongo.Mimi ni kada imaras siwezi kuhujumu Nchi yangu na kupoteza uaminifu wangu kwako na kwa serikali yako tukufu.Akaongeza kusema.

Nyerere akamwangalia kisha akamwambia, haya kapumzike kidogo hapo nje halafu nitakuita tena.Alipo toka nje akakutana na makada wenzake wakamuuliza wewe amekupangia wilaya gani?mwenzake akamwambia mimi nimepangiwa wilaya ya MUFINDI! Akabaki anashangaa! akawajibu niacheni nipumzike kwanza nitawajibu baadae.Moyoni akawaza wenzangu wamepewa ukuu wa wilaya mimi nimeishia kujichanganya kwasababu ya ushauri wa kijinga! loo salaleee! Myoni akawa anajiapiza nikirudi yule mhauri wangu atanikoma, nitaua mtu mimi.

Baadae mchana akaitwa tena kumuona Nyerere, akamwambia, nilitaka nikupe ukuu wa Wilaya ila naona bado hujaiva sana kikada nenda ukasubiri wakati mwingine.Baada ya miaka kupita akteuliwa kuwa KATIBU WA CCM WILAYA daa jamani Nyerere alikuwa hatari.
 
Hii hadithi nimeshaisikia kitambo sana tena mara kibao kila anayesimulia anafanya modification yake. Hya bana tupigeni tu.
 
Duuuh! Kiukweli jamaa alikuwa hajaiva. Hajaulizwa hata chochote lakini kaanza kujipayukia mwenyewe. Hata mimi ningekuwa mwalimu ningempa muda akomae kwanza. Ushauri wa jirani umemponza.
 
Salamu wanajamvi!
Ngoja niwasogezee kisa hiki cha kweli kabisa kilicho mkuta jirani wa miaka hiyo enzi za Nyerere.Huyu jirani yangu alikuwa ni KATIBU TARAFA KWA MUDA MREFU.Mwanzoni mwa miaka ya 80 Nyererealiwapeleka makada kadhaa Nchini Yugoslavia kwenda kujifunza uongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya chama na serikalini.Baada ya miezi sita wakarudi, wakaendelea na majukumu yao ya zamani.

Baada ya miezi sita hivi huyu jirani yangu akaitwa aende Ikulu tarehe aliyo pangiwa bila kukosa.Akapata wasiwasi mkuu huku akijiuliza imekuwaje yeye mpaka aitwe ikulu kwa agizo hilo kuu la bila kukosa?

Akaomba ushauri kwa rafiki yake wa karibu.Yule rafiki yake akamwambia, unajua dunia siku hizi imeharibika sana, usikute kuna adui yako kapeleka taarifa kuwa unafanya biashara ya meno ya Tembo, maana na mimi nimesikia watu wanateta mahali! Yule Katibu Tarafa akaitikia inawezekana maana binadamu kwa kuoneana kijicho huwawezi.Siku ya kwenda IKULU ikawadia.Mapema asubuhi akafika ofisini, akakaribishwa ili asubiri kuitwa aingie.

Zamu yake ikafika,akaitwa akaingia. kwa mbali akaona Nyerere anavua miwani ili amuone vizuri, akaingiwa na hofu kuu! Baada tu ya salamu yule jirani yangu akaanza kujitetea akasema,Unajua mkuu, mimi biashara ya meno ya Tembo siijui na wala sijui wanauzia wapi! watu tu wameamua kuniharibia kazi na kukuletea wewe taarifa za uongo.Mimi ni kada imaras siwezi kuhujumu Nchi yangu na kupoteza uaminifu wangu kwako na kwa serikali yako tukufu.Akaongeza kusema.

Nyerere akamwangalia kisha akamwambia, haya kapumzike kidogo hapo nje halafu nitakuita tena.Alipo toka nje akakutana na makada wenzake wakamuuliza wewe amekupangia wilaya gani?mwenzake akamwambia mimi nimepangiwa wilaya ya MUFINDI! Akabaki anashangaa! akawajibu niacheni nipumzike kwanza nitawajibu baadae.Moyoni akawaza wenzangu wamepewa ukuu wa wilaya mimi nimeishia kujichanganya kwasababu ya ushauri wa kijinga! loo salaleee! Myoni akawa anajiapiza nikirudi yule mhauri wangu atanikoma, nitaua mtu mimi.

Baadae mchana akaitwa tena kumuona Nyerere, akamwambia, nilitaka nikupe ukuu wa Wilaya ila naona bado hujaiva sana kikada nenda ukasubiri wakati mwingine.Baada ya miaka kupita akteuliwa kuwa KATIBU WA CCM WILAYA daa jamani Nyerere alikuwa hatari.

Wasiwasi mkuu na hofu kuu sijui huwa vipoje Mkuu?

Anyway umenikumbusha enzi za nyerere naomba tuburudike sote kwa hizi products hapa

Cooking fat.jpg
 
Nyerere alisuluhisha ugomvi wa Kawawa na Msekwa kwa staili hizo hizo
 
Back
Top Bottom