Nyerere afananishwa na Yesu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,323
33,128
10_09_net5bx.jpg
“Nyerere alikuwa mtu wa ajabu…matendo yake yanakaribia kufanana na ya Yesu. Hakika hajatokea mtu wa kuvaa viatu vyake,” anasema Mbusuro Wanzagi, mke wa 10 wa Chifu Edward Wanzagi Nyerere.

Mbusuro anasema mume wake alikuwa kaka mkubwa wa familia ya Chifu Nyerere Burito na ndiye aliyemlea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Mwalimu Nyerere alilelewa na kaka yake ambaye ni mume wangu hivyo namfahamu Nyerere kwa karibu…alijituma sana kuleta ukombozi na uhuru wa Taifa la Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla,” anasema Mbusuro. Anasema Mwl. Nyerere alifanya mambo ya ajabu ambao hayawezi kufanywa na binadamu wa kawaida kwa sababu alijitoa kwa ajili ya Taifa lake kama Yesu alivyojitoa kwa lengo la kuwakomboa wanadamu.

“Nyerere hakuwa na ubaguzi wa ndugu, kabila, rangi, dini, masikini wala tajiri. Aliwajali sana watu masikini na alikuwa wa kwanza kusalimia watu ambao walipaswa kupiga magoti na kumsalimia yeye,” anasema.

Anasema upendo wa Nyerere ulikuwa wa ajabu na alijishusha kwa kiwango ambacho binadamu wa kawaida hawezi kufikia.

“Ingawa Nyerere alikuwa kiongozi mwenye hadhi ya Kimataifa na mwenye upeo mkubwa alipenda kukaa na wazee na kusikiliza mawazo yao, pia alipokuwa anakuja Butiama alihakikisha anatembelea majirani na hasa wajane na wazee wenye shida,” anaeleza.

Tabia hiyo ilimtofautisha Nyerere na vijana wengine ambao licha ya kutokuwa na majukumu mengi, hawana tabia ya kuwajulia hali jirani wala jamaa zao.

“Achilia mbali majirani na jamaa, wapo vijana wengi wenye elimu na kazi nzuri lakini wamewasahau hata wazazi wao…hawakumbuki kwenda vijijini kuwajulia hali wazee wao,” Mbusuro anasema kwa uchungu.

Anasema suala la kumuenzi Baba wa Taifa linahitaji baraka za Mwenyezi Mungu na itakapofika muda muafaka Mungu atawasaidia Watanzania ili waweze kumuenzi kwa vitendo.

Ingawa alikuwa na kazi nyingi, Nyerere alipenda kusali, kutembelea wagonjwa pia kuhamasisha jamii inayomzunguka kuhusu umuhimu wa kuwasaidia watu wenye shida.

Pia Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa, kabla ya kufuta utawala wa kichifu na alijadiliana na ndugu yake Chifu Edward Wanzagi na kumueleza jinsi utawala huo ulivyokuwa kikwazo kwa Umoja wa Kitaifa.

“Chifu Wanzagi alikubaliana naye na hatimaye alifuta kisheria utawala huo wa kichifu….na mkakati wa kujenga Umoja wa Kitaifa ukaimarika kwa kasi,” Mbusuro anaeleza.

Padri Andrea Duda wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma, anasema kuwa hakuwahi kumuona Mwalimu Nyerere lakini anaamini kuwa alikuwa kiongozi tofauti na mwenye kipaji cha hali ya juu.

“Mimi nimetokea Poland na nilifika hapa Musoma ikiwa imepita miaka mitatu baada ya kifo cha Nyerere lakini nimesikia habari nyingi zinazomhusu,” anasema Padri Duda.

Anaendelea kusema, “kwa mujibu wa maelezo ya watu wa hapa, naona Nyerere alikuwa mwamini hai wa Kanisa Katoliki, alipenda kusali, kuhudhuria misa takatifu na kuishi maisha ya kiroho.”

Nyerere aliweka uhusiano wake karibu na Mungu na alifanya mambo mengi ya kumpendeza Muumba wake hasa kuwahimiza watu kuwa na upendo, umoja, mshikamano na amani.

Nyerere alitenga muda kwa ajili ya kusoma biblia na maandiko matakatifu. Pia aliandika vitabu vitano vya dini kwa mfumo wa utenzi ili kuhamasisha usomaji wa Biblia kwa njia ya utenzi.

Nyerere aliandika Utenzi wa Injili Kadiri ya Utungo wa Matayo, Utenzi wa Injili Kadiri ya Utungo Marko, Utenzi wa Injili Kadiri ya Utungo Luka, Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo Yohana na Utenzi wa Matendo ya Mitume.

Ujumbe wa Injili ulioandikwa na Nyerere unakusudia kufikisha ujumbe muhimu kwa jamii hususan vijana ili uweze kuzaa matunda yake ya matumaini, amani na upendo kati ya wanadamu.

Kwa mujibu wa dibaji iliyoandikwa katika vitabu hivyo na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Nyerere amefaulu kuweka sehemu ya ujumbe wa maandiko matakatifu katika mtindo wa tenzi.


http://www.habarileo.co.tz/makala/?n=3883
 
Aliyesema amekose sana , hakujawahi wala hakutakuja kutokea mwanadamu akafanana na Yesu kwa chochote.
 
Haya majani ya Jamaica,...!!! Tuwe makini sana! No Comments.
 
Back
Top Bottom