Nyaraka za uchaguzi zakamatwa Segerea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyaraka za uchaguzi zakamatwa Segerea

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kilimasera, Nov 4, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wakati huo huo, watu wawili akiwemo msimizi mmoja wa uchaguzi kutoka kata ya Segerea wanadaiwa kukamatwa na nyaraka kadhaa za tume ya uchaguzi, ikiwamo mihuri nje ya kituo cha kujumlisha kura cha Anatoglou jijini Dar es Salaam.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana usiku zimeeleza kuwa watu hao walitoka kununua chakula walikamatwa kwa nyakati tafauti majira ya saa 3:00 usiku nje ya kituo hicho wakiwa na nyaraka hizo ambazo ziliwekwa kwenye chakula walichokuwa wamebeba.

  Tukio hilo lilizua zogo katika kituo hicho kilichozungukwa na maelfu ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakishinikiza matokeo ya jimbo hilo yatangazwe.

  Afisa huyo wa uchaguzi alikamatwa majira ya saa 3:00 usiku jana alipokuwa akirudi kununua chakula. Aliposhukiwa kuwa na nyaraka hizo, alipekuliwa na kukutwa nazo.

  "Aliporudi walimuuliza umebeba nini? Akajibu "Chakula." chanzo cha habari kilieleza na kuendelea:

  Waliendelea kumhoji "Tutaamini vipi kama umebeba chakula tu? Tunaomba tukupekue."

  Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, wafuasi hao walianza kumpekua afisa huyo kukuta pamoja na chakula, karatasi za matokeo zenye mihuri ya Nec.

  Gazeti hili lilifika eneo la tukio majira ya saa 6:00 usiku na kukuta hali ikiwa imetulia huku askari wanne wa kutuliza ghasia (FFU) wenye silaha wakiwa wamezunguka kituo hicho huku mamia ya wananchi wakisubiri matoke katika eneo hilo.

  Jitihada za gazeti hili kumpata kamanda wa polisi mkoa wa Ilala Faustine Shilogile jana usiku zilishindikana baada ya simu zake za mikononi kuzimwa.

  Katika hatua nyingine wagombea ubeunge wa CUF na Chadema waliliambia gazeti hili kuwa wamewasilisha malalamiko yao NEC, kutaka uchaguzi huo urudiwe kabla matokeo hayajatangazwa.

  Mpendazoe wa Chadema na Timangale Mussa (CUF), walisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa uchaguzi huo umegubikwa na kasoro nyingi tangu mwanzo wa mchakato wake.

  Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime alikirikupokea malalamiko hayo lakini akasema hayakuwasili kwa barua h
   
 2. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Patamu hapo!! Huu ni uchaguzi huru na wa haki
   
 3. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sisiem haioni shida endapo damu ya watanzania itamwagika ila wao waendelee kututawala kwa nguvu, hii ni laana na siku moja Mungu atawapa hukumu stahili ili kuwanusuru wa tanzania kwa utumwa huu wa ndani. Kuna haja gani kufanya uchaguzi kwa gharama kubwa na mwisho wa siku matokeo hayaheshimiwi.
  Huku ni kutukana wananchi na demokrasia kwa ujumla wake.
   
 4. M

  MSAUZI JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 228
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mumeanza mambo yenu ya jini mtu Buguruni kuonekana ofisi ya CUF
   
 5. seams

  seams Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  YOU MUST BE A SISIEM KADA HUH!!!!!!!:nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono:
   
 6. seams

  seams Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Junior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Join DateWed Nov 2010Posts2Thanks0Thanked 0 Times in 0 PostsRep Power0
  [​IMG] Re: Nyaraka za uchaguzi zakamatwa segerea

  YOU MUST BE A SISIEM KADA HUH!!!!!!!:nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono: ​
   
Loading...