Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Siasa hizi zinanikumbusha hadithi ya Nyani Mwenzetu.
Miaka ya nyuma nyani walikuwa wakipata shida sana huko porini. Binadamu alikata misitu chakula kikawa cha shida sababu miti imekatwa na matunda hamna kwa ajili ya jamii hii ya wanyama. Kukawa na ukame pia sababu ya kukosekana mvua.
Nyani wakaamua kufanya kikao. Kwenye kikao hicho wakaamua kuwa wafanye madawa ya kumbadilisha nyani mmoja wao awe binadamua halafu aende kuwasaidia kuwatetea kule kwa binadamu linapokuja suala la kukata miti n.k
Nyani wote wakachanga walichonacho wakaamua kumpeleka huyo nyani aliyechaguliwa kwa mganga. Mganga akafanya dawa mara yule nyani akageuka binadamu mzuri na mwenye nguvu, busara na hekima. Wale nyani wakamfanyia sherehe wakamuaga aende mjini kuonana na binadamu.
Akiwa huko njiani akakuta kuna mtoto wa mfalme yupo shambani anacheza na wenzie. Nyani watano wakatumwa waende kuwashambulia kwa kushtukiza walinzi wa yule mtoto. Wakalemewa wakakmbia wakmwacha mtoto. Yule binadamu aliyekuwa nyani akajitokeza na kujifanya akipambana nao na hatimaye wakakimbia akamwokoa mtoto wa mfalme aliyekuwa amezingirwa. Habari zile zikafika kwa mfalme akashukuru na kufurahi sana na mwishowe akamwalika yule binadamu na kumpa uwaziri wa ulinzi.
Binadamu nyani ilikuwa awasaidie nyani wenzie walioko porini kwa kuwajengea mazingira salama ya wao kuishi wakitegemeana na binadamu ambaye aliamua kuwatekeza na kuwafanya kitoweo huku akiwaharibia mazingira yao ya kustawi. Yule binadamu akapewa nyumba ,mke na maisha mazuri sana huku akisahau kabisa jambo alilokuwa ametumwa.
Kwa kutaka sifa kwa mfalme, akawa mkali sana kwa hbari zozote za nyani kula mahindi au kuingia pale kijijini. Akaweka na tamko kuwa ikitokea Nyani ameonekana popote pale apigwe mshale. Lengo lake lilikuwa ni kuangamiza nyani wote ili asirudi tena kuwa nyani. Alishapendezwa na maisha ya binadamu.
Habari zile zilipowafikia nyani walihuzunika sana. walilia na kuomboleza baada ya kuona kwa sasa kasi ya kuuawa inazidi na maisha yanakuwa magumu zaidi kwao. Walikamatwa wakakatwa ndimi zao, wakanyongwa au kupigwa mishale. Wakasemezana wao kwa wao hadi nyani mwenzetu ametugeuka?
Wakakusanyika tena nyani wote porini. Wakaamua kuchanga tena pesa nyingi sana waende kwa mganga akawasaidie kuwapatia dawa wamrudishe yule binadamu awe nyani kama wao. Mganga akawapatia dawa. Wakatuma nyani wawili waende mjini kwenye jumba la yule binadamu nyani usiku wa manane wakapige ngoma na huku wakiimba.
"Alikuwa kwetu, alikuwa sisi, ametoka kwetu na arudi kwetu.... huku wakipiga ngoma na kuruka ruka. Yule binadamu nyani apolisikia wimbo ule ghafla akaanza kubadilika..a Akaanza kuota manyoya na kubadilika umbo... Mwishowe akakmbilia dirishani na kuruka kutoka nje.... akatokomea huko porini.....