Nyangwine bomu

Nyangwine bomu

Wakuu nimesikiliza mchango wa mbunge wa Tarime Nyangwine nyambari nikagundua ana mapungufu yafuatayo:-
1.Hajiamini anaongea kwa kuchekacheka.
2.Anaongea kama yupo kwenye vijiwe vya kampeni Nyamono.
3.Anapoongea hatulii kwenye kiti anakuwa kama anawashwa.

My take:
Kwa mnaomfahamu naomba mnipe mnachokifahamu kuhusu huyu mheshimiwa.
amechangia elimu yetu kushuka kwa kasi anaendelea kuwazalilisha watu wa tarime siyo kama tuwajuavyo- Heri ilo jina aitwe mbwa
 
jamani msiwalaumu wanatarime yaliyofanyika tarime nq wizi wa kura ni ya kumwachia Mungu, na ndo maana nilisha andika thread yangu hapa iliyokuwa inasema mbunge kuishi kwenye nyumba ya kupanga ni halali nilikuwa nilikuwa na maanisha huyu mbunge akuwa chaguo la wana tarime na ndo maana mpaka leo akubaliki na akienda tarime ub
 
unaona sasa....na wewe huna tofauti na huyo nyangwine:......

ameongea nini
juu ya nini
wapi
lini
na kwa nini............

Ndo tatizo la kukariri madesa. Wewe ni sawa na Nyangwine
 
wana tarime wamekosea sana kumchagua nyangwine kuwa mbunge wao.nimemsikiliza akichangia hotuba jioni hii....ni mtu ambaye hawezi kujenga hoja mtu wa kuchekacheka hata ktk mambo ambayo ni serious km mauaji ya nyamongo............amejikanyaga kwa kutaja mambo ya ajabu kama kukata watu mapanga mpaka lukuvi (ambaye wanatoka chama kimoja)ameomba afute kauli...........this is nyangwine.
Nilimsikiliza kipindi cha kuchangia bajeti ya serikali,tangu siku hiyo sitamani tena kumtazama. Leo ilipofika zamu yake nilitoka maana hiyo ni takataka,yaani anaongea mnyika then baada ya hapo unamsikiliza Nyangwine si utaona hujitendei haki. Ki ukweli I hate the guy ingawa ni schoolmate wangu pale mara secondary...
 
Kimsingi yuko shallow,hakuna mjadala hapa!mnabisha nini sasa!
 
mtu anaongea kwa wasiwasi halafu anasikilizia reaction toka upande wa chama chake! Ni kama alikuwa anaongea tu ili wanatarime wamsikie mbunge wao kuwa aliongea wanachotaka wao alafu basi! Nyambari si machachari kama wabunge wote wa Tarime waliopita na sidhani kama kweli wana-Tarime experted a simple approach like this to the gvnment from this MP!
 
Kimsingi yuko shallow,hakuna mjadala hapa!mnabisha nini sasa!
Hajui kuongea, hajui kujenga hoja, hayuko serious, hana vision etc huyu ni bogus, NATILIA SHAKA MAVITABU YAKE, NADHANI YAWEZAKUWA MOJA YA SABABU YA KUFELI WA TOTO WA SEKONDARI WANAOVISOMA!
 
Kituko kingine bungeni,kuchekacheka na kuongea pumba,anatia aibu tupu!
Jamani naona afadhali nyangwne wenu wa kuchekacheka kuliko vilaza wa dodoma mjini kuanzia huyu na wengine waliomtangulia ni matapishi matupu. Alert : MAGAMBA ACHENI KUWEKA WAGOMBEA VILAZA DOM MJINI,JIMBO MNALIGAWA KWA CDM 2015!
 
Wakuu nimesikiliza mchango wa mbunge wa Tarime Nyangwine nyambari nikagundua ana mapungufu yafuatayo:-
1.Hajiamini anaongea kwa kuchekacheka.
2.Anaongea kama yupo kwenye vijiwe vya kampeni Nyamono.
3.Anapoongea hatulii kwenye kiti anakuwa kama anawashwa.

My take:
Kwa mnaomfahamu naomba mnipe mnachokifahamu kuhusu huyu mheshimiwa.
kwani wewe ulikuwa humjui?waulize wamanyamongo wakupe undani wake.hayo mapungufu uliyaona ni machahe bali anayo mengi tu.inaonekana hata lugha kwake ni shida sijui hivyo vitabu alikuwa anaandikiwa au la.
 
Kuna ubunge wa kununua na ubunge wa kuchaguliwana bado
kuna makima wengi pale hawajui walichokwenda kufanyia bungeni
ni makosa ya wananchi yule si msaniii au amjui mwandishi wa vitabu
vya shule za chekechea ayaaa bado mtaona mengi

kikupacho raha na uchungu kitakupa
 
Muuaji wa elimu kwa kuwadesesha wanafunzi kwa kuwa spoon feed na madesa. Ubunge ni tofauti na kuandaa desa.
 
Ananikumbusha sana yule Mbunge wa zamani Stanley Kevela Yono...hawana tofauti kabisaaaa...
 
huyu ana tofauti na wabunge wa viti maalum kwanza kama kwao kapigwa
mawe na wapiga kura je anamwakilisha nani ? wewe ni mhe unakimbizwa na mawe
na wananchi uliosema wamekuchagua sasa hapo vip? kama ni mimi naachana na huyu
ubunge naendelea na shughuli nyingine mbona kazi zipo nyingi tuuu kama kilimo kwanza
uwezi basi funga mbuzi wa maziwa

kikupacho raha na uchungu kitakupa
 
Ubunge aliupata kwa kutumia fedha nyingi sana. Lakini hili sio la kumlaum hakuna mbunge wa CCM anayemzidi Nyambari Nyanwine. Hebu semeni ukweli ni mbunge ama waziri yupi anayempita Nyambari Nyangwine?

Nyambari Nyangwine hajaandika vitabu vya lugha ya kiswahili. Ila amekuwa mdhamini wa waandishi wa vitabu hivyo.
 
Jamani naona afadhali nyangwne wenu wa kuchekacheka kuliko vilaza wa dodoma mjini kuanzia huyu na wengine waliomtangulia ni matapishi matupu. Alert : MAGAMBA ACHENI KUWEKA WAGOMBEA VILAZA DOM MJINI,JIMBO MNALIGAWA KWA CDM 2015!
Well said. Na tumeanzia vyuoni hata hapa cbe tumefungua tawi. Na tuna oparesheni fungua matawi kwa mitaa na vijiji vyote vya jimbo la dodoma mjini. 2015 lazima kieleweke dodoma, hatuwaachi magamba.
 
Tarime hatuna Mbunge yule jamaa ni Ombwe. Eti wanasiasa uchwara wanaokuja kutuchongani tutawafukuza wakati yeye mwenyewe alienda waka mpiga mawe sasa nani uchwara. Af wachimba madini wa nyamongo wasipo tekeleza ahadi kwa wananchi nitawafukuza mwenyewe. Yaani huyu jamaa alikuwa anatema pumba sijawahi kuona, yaani anadhalilisha Tarime ambayo imesheheni wasomi kibao. Af nasikia ana master ya Ed in Kiswahili sasa mbona hajui hata kukiongea, maajabu duniani.
 
nadhani watu tunatofautiana sana katika kutafsiri mambo. kaongea kipi kibaya? kwani si kweli kuwa wana tarime wamechoshwa? kwani si kweli kuwa sasa wako tayari kwa lolote? kwa taarifa yenu. hamjui tu kumsoma mtu mwenye furaha, huzuni, hasira n.k. muda ule jamaa alikuwa na machungu sana na wala msione alikuwa anacheka. mimi si wa Tarime wala mwana ccm bali namuunga mkono. si mmeona hata Ndugai kampotezea Lukuvi?

kwa taarifa yenu, ujumbe not only sent, but delivered. na wasitekeleze aliyosema Nyangwine waone. kama mnataka kujua kuwa alikuwa sahihi nendeni Tarime mkawaulize wahanga juu ya alichoongea leo kama hamjakaa kimya.

Hivi wewe mtu wangu kweli ulikuwa unaangalia TV au ulikuwa unasikiliza radio kwa mtu yeyote anaye jua psychology moja kwa moja atasema yule Nyangwine hakuwa anaongea kwa hisia ya jambo husika alilo kuwa analizungumzia hivyo sikubaliani na wewe. nazani kama ulimuona Mwakyembe alivyokua ana zungumzia matatizo ya daraja ktk jimbo lake kwa bunge la 9 pia nakashifa za Richmundi hizo ndizo hisia angepaswa hata huyu Nyangwine aoneshe ,na siyo kuchekacheka pia huyo Ndugai kupotezea ni kawaida yao kulindana wao kwa wao.nazani ume nipata
 
Back
Top Bottom