Nyama ya Ng'ombe na Viazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyama ya Ng'ombe na Viazi

Discussion in 'JF Chef' started by MziziMkavu, Nov 4, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Haya na Mimi nawaleteeni vyakula na Mapishi ya Kichina Enhoo Enho

  Mapishi ya nyama slesi ya nyama ya ng'ombe na kiazi


  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji:[​IMG]
  Nyama ya ng'ombe gramu 200, kiazi kimoja?pilipili boga moja na pilipili hoho kimoja, sukari kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko viwili, wanga kijiko kimoja
  Njia:
  1. osha nyama ya ng'ombe, kata iwe slesi, changanya pamoja na chumvi, mafuta, mchuzi wa sosi, sukari, wanga.
  2. kata kiazi kiwe slesi halafu weka kwenye maji, ipakue.
  3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia slesi za nyama ya ng'ombe, korogakoroga, ipakue. Tia vipande vya pilipili boga na pilipili hoho korogakoroga, tia slesi za kiazi korogakoroga, tia chumvi, nyama ya ng'ombe korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.


  Mapishi ya supu ya mboga


  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji:[​IMG]
  Kuku mmoja, uyoga gramu 20, paja la nyama ya nguruwe lililokaushwa gramu 20, nyanya moja, nyama ya nguruwe gramu 50, mboga gramu 50, wanga kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja
  Njia:
  1.osha kuku, halafu weka kwenye sufuria, mimina maji, halafu washa moto, chemsha kwa saa 3 ili kupata supu ya kuku.
  2. osha mboga, kata paja la nyama ya nguruwe lililokaushwa, uyoga na nyanya ziwe vipande, kata nyama ya nguruwe iwe vipande halafu changanya pamoja na chumvi, uwanga.
  3. chemsha maji kwenye sufuria, halafu tia vipande vya uyoga, korogakoroga, vipakue. Tia nyama ya nguruwe kwenye maji, korogakoroga mpaka iwe na rangi ya nyeupe, ipakue.
  4.mimina supu ya kuku kwenye sufuria, baada ya kuchemka, tia chumvi, tia vipande vya paja la nyama ya nguruwe lililokaushwa, uyoga, nyanya, nyama ya nguruwe, korogakoroga, tia mboga, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.

  Mapishi ya nyama na pilipili boga na pilipili hoho


  [HR][/HR]


  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"][​IMG]Mahitaji: Nyama ya ng'ombe gramu 300, pilipili boga gramu 150, pilipili hoho gramu 150, vitunguu saumu gramu 10, mchuzi wa sosi vijiko viwili, wanga kijiko kimoja, sosi ya chaza vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja.
  Njia:
  1.kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, changanya pamoja na wanga, mchuzi wa sosi na mafuta. Kata pilipili boga na pilipili hoho ziwe vipande?
  2.washa moto, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, korogakoroga, halafu tia vipande vya vitunguu saumu, pilipili hoho na pilipili boga, korogakoroga, tia mchuzi wa sosi na sosi ya chaza, chembechembe za kukoleza ladha na chumvi, korogakoroga,ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

  Mapishi ya slesi ya nyama ya nguruwe na uyoga


  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Kwa Wale wanaotumia Kitomoto haya kazi kwenu mimi simo mchanga wa pwani huo .... Mahitaji:[​IMG]
  Nyama ya nguruwe gramu 200, uyoga gramu 100, nusu ya pilipili mboga, wanga nusu ya kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, ute wa yai moja, chumvi vijiko viwili, na tangawizi
  Njia:
  1. kata nyama ya nguruwe, uyoga na pilipili mboga ziwe slesi, koroga slesi ya nyama ya nguruwe pamoja na wanga, mchuzi wa sosi, ute wa yai na maji kidogo.
  2. washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria halafu tia slesi ya nyama, korogakoroga, tia slesi ya uyoga na vitunguu saumu, korogakoroga tia slesi ya pilipili mboga, tia chumvi korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Mapishi ya mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe yenye ladha ya pilipili hoho


  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji:[​IMG]
  mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe gramu 200, chumvi vijiko viwili, chembechembe za pilipili manga kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, sosi ya chaza vijiko viwili, vipande vya vitunguu maji, pilipili hoho gramu 10, vitunguu saumu na tangawizi
  Njia:
  1. Osha mbavu za nyama ya nguruwe, kasha changanyakoroga pamoja na chumvi, chembechembe za pilipili manga,sukari, mchuzi wa sosi, sosi ya chaza, na vipande vya vitunguu maji na tangawizi.
  2. washa moto , mimina mafuta kwenye sufuria, halafu tia mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe zikaange, mpaka ziwe hudhurungi, zipakue.
  3. baadaye, tia pilipili manga na pilipili hoho, halafu tia vitunguu saumu, korogakoroga halafu tia mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe, korogakoroga, tia karanga korogakoroga zipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

  Mapishi ya nyama ya ng'ombe na ufuta


  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji:[​IMG]
  Nyama ya ng'ombe gramu 200, ufuta gramu 20, chumvi vijiko viwili, mchuzi wa sosi kijiko kimoja,mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, pilipili manga nyeusi kijiko kimoja, sosi ya chaza kijiko kimoja, vitunguu maji gramu 5
  njia:
  1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, koroga pamoja na chumvi, mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, pilipili manga nyeusi, sosi ya chaza. Kata vitunguu saumu na pilipili hoho iwe vipande.
  2. washa moto, tia vipande vya nyama ya ng'ombe vikaange kwa dakika moja halafu tia vipande vya vitunguu maji na pilipili hoho korogakoroga, mimina sosi ya chaza, tia ufuta korogakoroga, tia chumvi, korogakoroga. Ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

  Mapishi ya vipapatiro vya kuku


  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji:[​IMG]
  Vipapatiro vya kuku gramu 500, vitunguu gramu 100, figili gramu 100, pilipili hoho gramu 20, vitunguu saumu gramu 20, tangawizi gramu 15, cumin vijiko viwili, mchuzi wa sosi vijiko viwili, sukari vijiko viwili, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja , chembechembe za pilipili manga kijiko kimoja
  Njia:
  1. kata vitunguu maji viwe vipande, kata figili iwe vipande, kata pilipili hoho iwe vipande.
  2.kata vipapatiro vya kuku viwe vipande viwili na koroga pamoja na mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia na chembechembe za pilipili manga.
  3.washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vipapatiro vya kuku kwenye sufuria vikaange mpaka viwe hudhurungi, vipakue. Washa moto tena, tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu, pilipili hoho, korogakoroga, tia vipande vya figili na vitunguu saumu korogakoroga, tia vipande vya vipapatiro vya kuku, korogakoroga, tia mchuzi wa sosi, sukari, cumin, chumvi ,korogakoroga, mimina mafuta ya ufuta , ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [​IMG]
   
Loading...