Mkuu
ndege JOHN hakuna mnyama ambaye haliwi. Suala ni mnyama yupi analiwa na nani. Ukifika Nigeria au kwa wanaopakana na mbuga/misitu ndiyo utathibitisha ninachokwambia.
Kenge hata uzaramoni analiwa vizuri tu. Anajulikana kama mburu. Huko Mtwara wanaliwa panyapori, vyura wakubwa wanjano na kadhalika. Mbwa huliwa kimila uheheni, ubenani na uluguruni.
Sisi wangoni tunakula panyapori tunaowaita mbewa na wadudu wa aina mbalimbali. Upareni wanakula kobe na mayai yake; kilombero huko na kwawahadzabe wanaliwa ngedere na nyani na kadhalika na kadhalika.