Nyama kuanza kutengenezwa maabara

Nyama kuanza kutengenezwa maabara

Mimi siwezi kula hiyo vitro
Illuminat watatumaliza, nani aliyewaambia tunateseka au tunapata shida kupata nyama,wamesha haribu karibia grains zote na kumsababishia mwanadamu kila aina ya taabu na magonjwa ya ajabu ajabu na sasa wamehamia kwenye nyama,navyofahamu tunavyopenda sifa za kijinga vitu hivi vitaingia bongo kwa speed ya ajabu vikichagizwa na serikali na wanasiasa.
 
V3-300x200.jpg

Wanasayansi wameaanza kutengeneza nyama maabara waliyoipa jina la nyama ya Vitro au "Vitro meat" kwa kimombo ili kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama.

Kwa kawaida nyama yoyote hutengenezwa kutokana atoms mbalimbali. Kama unaweza kutengeneza atoms kwa njia tofauti na ya kawaida, basi pia unaweza kutengeneza nyama.

Ukipewa vipande viwili vya nyama kimoja kilichotokana na mnyama aliyechinjwa na nyingine aina ya Vitro ambayo hutengenezwa maabara ni vigumu kuelezea tofauti yake kutokana na kufanana kwa muonekano na hata ladha.
Maabara sasa inafanya kazi ya kutengeneza nyama ambayo ni sawa na nyama uliyozoea kununua buchani.

Profesa wa Molecular Biology, katika Chuo Kikuu cha Stanford, alinukuliwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza akisema inawezekana kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama kwa kuwa nyama sasa inaweza kutengenezwa maabara.

“Sina nia ya kutengeneza vyakula vipya kwa watu wasiokula nyama. Natengeneza chakula kwa ajili ya wanaokula nyama na ambao wana nia ya kula nyama. Hii itawasaidia kupata nyama bila shurba.

“Nyama ya Vitro haitokani na kiumbe hai hivyo haiwezi kufa na hii naletea tofauti kubwa katika upatikanaji wake. Kiuchumi, gharama za uzalishaji wake ni kubwa na hivyo kufanya uzalishaji mkubwa kuwa changamoto. Pia kutokana na ushawishi wa wafugaji wakubwa Marekani na sehemu nyingine duniani, inawezekana kuwa na vikwazo vya kisheria,” anasema Profesa huyo.

Gharama kubwa za uzalishaji wa nyama ya Vitro inaweza kuwa ndiyo kikwazo kikubwa katika uzalishaji wake. Hata hivyo, ugunduzi wa hivi karibuni kwenye teknalojia ya uzalishaji wake unategemea kupunguza gharama.

Kwa sasa kampuni kubwa ikiwamo New Harvest na Modern Meadow zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nyama hii inazalishwa kwa wingi na kuwafikia walaji wengi.

Chanzo: Mtanzania
Watakula wenyewe uchafu huo. Na yakianza kuuzwa mahotelini, sili chakula safarini au nagona kusafiri kabisa.
 
haiwezi kuitwa nyama, waite jina jingine tu!
3D meat (3D food printing)!

Sidhani kama haya mabadiliko ya tabia ya nchi yatatukwepesha kula vyakula vya maabara. Miaka kumi ijayo huenda bio food ndio ikawa mtindo wa kisasa hasa kwa maskini ambao wako tayari kula chochote kitachoweza kuokoa uhai. Tuendako, vyakula flesh kutoka shamba vitakuwa vya wenye pesa. Refer junky foods kwenye shopping malls za watu wa kipato cha chini huko ulaya na marekani halafu uone tuendako.
Umenena vyema sana mkuu. Utafiti kwa sasa umekazia kwenye njia mbadala za uzalishaji chakula kwa kuwa njia zilizozoeleka kama kilimo na ufugaji wa wanyama vinakumbwa na changamoto nyingi mfano ukame, gharama kubwa sana uzalishaji (ambazo hupelekea bei za chakula kuwa juu) na uchafuzi wa mazingira.
Hivyo basi ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia mbadala au vyanzo vya food production ni muhimu katika kuhakikisha kuwa dunia inajilisha yenyewe miaka mingi ijayo.
 
Mbona uliweza kula nyama za wanyama wakuchinja?

Haya mambo ni mazoea tu na tamaduni ulizozikuta au ulizozirithi ulipokuja hapa duniani. Ndio maana unaona leo kuna watu wanakula nyoka, panya, nguruwe n.k lakini hapo hapo kunawengine hawatumii unajua kwanini?
..wataalamu wanaita food sovereignty...
Sidhani kama haya mabadiliko ya tabia ya nchi yatatukwepesha kula vyakula vya maabara. Miaka kumi ijayo huenda bio food ndio ikawa mtindo wa kisasa hasa kwa maskini ambao wako tayari kula chochote kitachoweza kuokoa uhai. Tuendako, vyakula flesh kutoka shamba vitakuwa vya wenye pesa. Refer junky foods kwenye shopping malls za watu wa kipato cha chini huko ulaya na marekani halafu uone tuendako.

Umesema kweli. Sasa hivi tuhimize wakulimawatunze mbegu za mazao ya asili. Bila hivi watu wa kada ya chini watakuwa watu wakuugua "magonjwa mapya" kwakula junk foods. Lakini pia serikali isipolinda watu wake inasikitisha zaidi. Niliona sehemu eti kuna wakulima huko Iringa (Kama sijakosea) wamekatazwa kumiliki mbegu za asili ya mazao wanayozalisha. Najiuliza serikali itakuwa inafanya kazi ya kutetea big corporations tu wanaotafuta super normal profit kwa mgongo wa mkulima masikini?
 
Back
Top Bottom