Mkuu, afadhali zenu zinaunganishwa, sisi wengine tukiweka nyuzi zisizoisifia chadema au kumsema negatively yule zezeta zinafutwa kabisa!Ukiweka uzi kama huu watukufu wanaunganisha
Lipi alililolisema alipokuwa anahamia chadema ambalo ccm wamelitekeleza hadi akaamua kurudi ? video yake bado ingalipo.Mkuu, wakati alipohamia chadema na kuikandia ccm mbona mlikaa kimya bila kumzuia asifanye hivyo? Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Niliweka uzi muruwa sana hapa kuhusu jambo hili lakini waka merge kwenye uzi dhaifu sana ambao hata haukuhusiana !Inaudhi sana Mkuu kwani maudhui hayaendani kabisa.
Mkuu, acha kuhamisha goal post: hoja ya msingi ni uhuru wa kusema!Lipi alililolisema alipokuwa anahamia chadema ambalo ccm wamelitekeleza hadi akaamua kurudi ? video yake bado ingalipo.
Mama mambo vipi?Niliweka uzi muruwa sana hapa kuhusu jambo hili lakini waka merge kwenye uzi dhaifu sana ambao hata haukuhusiana !
Msijifiche kwenye ka hoja kadogo, Nyalandu amezungumzia pia tabia ya kishetani ilioneshwa na viongozi wakuu wa chama kwa kushangilia kifo cha aliyekua kiongozi mkuu wa nchi.
Pili, amezungumzia demokrasia ndogo na duni iliyopo ndani ya chama. Mwenyekiti amehodhi cheo kile kwa mda mrefu. Kika anayejaribu anakutana na kisanga. Sumaye aliambiwa na Mbowe kua "sumu haionjwi" kosa la sumaye ilikua ni kutaka uwenyekiti tu.
Tatu, Tundu Lissu anongozaje chama cha siasa chenye wanachama wengi kupitia mtandao wa Twitter na wasap? Yaani wakina Heche wapo, lakini wanaongozwa na mtu aliyepo ulaya kula bata!
Nyinyi bavicha mlitakiwa kua wakali na kukisaidia chama, mpaka sasa hatujui nani atagombea 2025, hakuna hata dalili. Tutashangaa Nape akifukuzwa CCM ndio mumchukue na kumwita 'kamanda' na siku akija kuondoka mtumuita mamluki. Yaani nyinyi!
Hahaha [emoji16][emoji38] nyinyi bavicha bhana! Hapo ndio umenijibu sasa? Sasa mie na Magufuli wapi na wapi? Kama aliua si muende mahakamani? Mie nazungumza demokrasia ndani ya chama changu, kama una hoja karibu.Tabia ya muuaji magufuli je aliyewaua Watanzania chungu nzima wasio na hatia yoyote kama vile Ben Saanane na Azory Gwanda na kuwabambikia kesi Watanzania mbali mbali unaikumbuka? Acha kuonyesha ujuha hadharani ili kumtetea huyo mchumia tumbo.