Nyalandu: Mimi kama sehemu ya sera za CHADEMA nitahakikisha ninaunganisha watu wa aina zote

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
nyalandu.jpg

Kada mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Lazaro Nyalandu amesema hatua ya maamuzi yake ya kujiunga na Chama Cha hicho hakushawishiwa na mtu yoyote bali ni kiu yake ya kujenga sera mbadala kwenye medani za siasa za upinzani nchini.

Nyalandu amesema “safari hii sio kwa sababu ya mtu au mimi mwenyewe, ili taifa lifanikiwe, mimi kama sehemu ya sera za CHADEMA nitahakikisha ninaunganisha watu wa aina zote wanaotoka kwenye historia mbalimbali ya taifa kupitia ukuaji wa demokrasia nchini."

“Siasa ni watu ili tuweze kufanikiwa kama taifa, ni muhimu mimi kama Nyalandu mtu akinikosoa nakubaliana naye ila nitamuombea aishi maisha marefu ili ninapofanikiwa kwenye siasa za upinzani wajionee wenyewe." Ameongeza Nyalandu

Mwishoni mwaka jana kada huyo akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini alitangaza kujivua nyadhifa zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuomba ridhaa ya kujiunga CHADEMA kwa madai ya kukosekana kwa demokrasia ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka Nairobi Kenya kuzungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi.
 
Naona jamaa anakuja kwa kasi kweli.....Hii inaitwa maandalizi ya 2020....Nafasi ya URAIS kupitia CHADEMA....All in all CHADEMA haikutakiwa kabsa kuwafanya hawa WANA CCM kuwa wasemaji wa CHAMA HADHARANI.....hawa ndio wanaoharibu upinzani HUYU NYALANDU ni miongoni mwa watu wanaotaka URAIS wa nchi hii kwa sapoti ya wezi wa RASILIMALI ZETU...kwenda kwake chadema ni njia mbadala ya yeye KUPATA NAFASI
 
Naona jamaa anakuja kwa kasi kweli.....Hii inaitwa maandalizi ya 2020....Nafasi ya URAIS kupitia CHADEMA
Vita ya uenyekiti Chadema ndio imeanza Nyalandu akiamua Mbowe hakatizi.Watu wawili wakiamua kushika uenyekiti Chadema ambao Mbowe hana ubavu wa kuwazuia ni wawili tu nao ni Nyalandu Na Lowasa.Lema Na Lisu wapiga kelele tu wanategemea ushawishi wa kelele zao tu lakini hao wawili Lowasa Na Nyalandu waziweza Kelele Na wana pesa za Ku backup up kelele zao. Kama Chadema inasema kuna watu wao wananunuliwa basi hao wawili wakiamua kununua wajumbe wa mkutano wawape kura uwezo huo wanao wa kununua Na kumtupilia mbali Mbowe.Lema Na Lisu nao wameshaanza kampeni za kusaka uenyekiti lakini hawatafika mbali hata ujumbe wa kamati kuu hawataingia
 
Back
Top Bottom