Nyalandu aifanyia kazi video ya Mch. Msigwa

Chilisosi

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
3,051
747
Ndugu zanguni,

Leo, kwa mara ya kwanza tokea Chadema iundwe, mbunge wa kutokea Chadema amefurahishwa na kazi ya waziri wa chama tawala. Mheshimiwa Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa facebook ameandika haya

Peter Msigwa

about an hour ago near Iringa, Tanzania

Nampongeza waziri, Nyalandu ,kwa hatua aliyochukua ,na kuwa waziri wa kwanza kuchukua ushauri wa kutoka Upinzani . Kwenye maswala mhimu ya kulinda maliasili zetu. Namuomba asiishie hapo , ufanyike uchunguzi wa kina kwa makampuni yote ya uwindaji ili kuhakikisha .sheria ,taratibu na kanuni za uwindaji zinafuatwa.
Jukumu la kulinda maliasili zetu ni la watanzania wote

Kwa kweli ni lazima tumpongeze mchungaji Msigwa kwa kuanza kujitambua na kuwa mwanasiasa wa kweli.

Ni wakati sasa na makamanda wengine wakaacha kutmia viroba na kuanza kujitambua kama Mchungaji.

==========================

Nyalandu aifanyia kazi video ya mch. Msigwa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza kufuta vitalu vyote vilivyokuwa chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd kutokana na kukiuka sheria za uwindaji nchini, huku akiifuta Idara ya Wanyamapori.

Uamuzi huo wa Serikali, umekuja siku chache baada ya Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuonyesha video inayoihusisha kampuni hiyo na ukiukaji wa sheria na taratibu za uwindaji.

Awali, Msigwa ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa madai hayo Mei 14, mwaka huu wakati wa uwasilishwaji wa bajeti ya wizara hiyo mjini Dodoma.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Nyalandu pia alitangaza kuifuta Idara ya Wanyamapori na kuunda Mamlaka ya Wanyamapori ili kuimarisha ufanisi katika sekta hiyo.

"Kufuatia tuhuma zilizowasilishwa bungeni kwa njia ya ushahidi wa DVD na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Peter Msigwa Mei 14, 2014… Kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 17(1) na 8(2), Nafuta umiliki wa vitalu vyote vilivyo chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd," alisema Waziri Nyalandu. Alivitaja vitalu hivyo kuwa ni Lake Natron GC East, Gonabis/ Kidunda- WMA na MKI- Selous.

"Hatua hii pia inafuta vibali vyote vya uwindaji vilivyotolewa katika msimu huu wa uwindaji. Hii iwe onyo kwa kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kwa ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu za uwindaji," alisema Nyalandu.

Aliongeza, baada ya kupata tuhuma hizo aliiagiza Idara ya Wanyamapori kufuatilia na kumhoji Mkurugenzi wa Kampuni ya GreenMiles Safaris Ltd, ndipo walipobaini makosa ya kampuni hiyo.

Aliyataja makosa hayo yaliyokiuka Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya 2009 kuwa ni pamoja na wageni wa kampuni kuwinda wanyama wasioruhusiwa wakiwemo nyani na ndege kinyume na kifungu cha 19 (1 na 2) na kuchezea watoto wa pundamilia na ngiri kinyume na kifungu cha 19 (1).

"Kufukuza wanyamapori kwa magari na kisha kuwapiga risasi wakiwa ndani ya magari kinyume cha sheria," alisema Nyalandu.

Akizungumzia hatua hiyo, Msigwa alisema ni ushahidi kuwa kambi ya upinzani bungeni inasema ukweli.

Chanzo: Mwananchi
 
viongozi wengi wangekuwa wanachukua ushauri wa wapinzani na wapenda maendeleo viongozi wakepongeza na kila mtanzania na taasisi zote hakuna engepinga.nyalandu katenda baada ya msigwa kifichua maouvu.mangapi yanafichuliwa hatuoni utekelezaji wake.2015 yaja tutashuhudia mengi ya kujisafisha.....
 
Chilisosi, Hivi ni nani amenza kujitambua? Waziri ambaye mara nyingi amekuwa anapewa ushauri mzuri wa kuboresha utendaji na akapuuzia, lakini pale anapoona kabanwa anaamua kuupokea ushauri huo (kwa shingo upande??) au waziri kivuli ambaye kila siku anashauri na anapuuzwa???
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zanguni,

Leo, kwa mara ya kwanza tokea Chadema iundwe, mbunge wa kutokea Chadema amefurahishwa na kazi ya waziri wa chama tawala. Mheshimiwa Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa facebook ameandika haya

Peter Msigwa

about an hour ago near Iringa, Tanzania

Nampongeza waziri, Nyalandu ,kwa hatua aliyochukua ,na kuwa waziri wa kwanza kuchukua ushauri wa kutoka Upinzani . Kwenye maswala mhimu ya kulinda maliasili zetu. Namuomba asiishie hapo , ufanyike uchunguzi wa kina kwa makampuni yote ya uwindaji ili kuhakikisha .sheria ,taratibu na kanuni za uwindaji zinafuatwa.
Jukumu la kulinda maliasili zetu ni la watanzania wote

Kwa kweli ni lazima tumpongeze mchungaji Msigwa kwa kuanza kujitambua na kuwa mwanasiasa wa kweli.

Ni wakati sasa na makamanda wengine wakaacha kutmia viroba na kuanza kujitambua kama Mchungaji.

isije kuwa wanatumia viroba kwa kuwa uwezo wao unaishia hapo, manake bia ishavuka 2000 sehemusehemu, wakati kiroba unakunywa hata ukiwa na mia 700. Dompo ya dodoma 13,000. Makamanda hela ya namna hiyo wanayo?
 
chezea video ile lazima waziri angechukua hatua.Wapinzania mbona huwa wanashauri mengi mazuri ila serikali huwa haitaki kuchuka kuhofia watapata sifa.
 
Ndugu zanguni,

Leo, kwa mara ya kwanza tokea Chadema iundwe, mbunge wa kutokea Chadema amefurahishwa na kazi ya waziri wa chama tawala. Mheshimiwa Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa facebook ameandika haya

Peter Msigwa

about an hour ago near Iringa, Tanzania

Nampongeza waziri, Nyalandu ,kwa hatua aliyochukua ,na kuwa waziri wa kwanza kuchukua ushauri wa kutoka Upinzani . Kwenye maswala mhimu ya kulinda maliasili zetu. Namuomba asiishie hapo , ufanyike uchunguzi wa kina kwa makampuni yote ya uwindaji ili kuhakikisha .sheria ,taratibu na kanuni za uwindaji zinafuatwa.
Jukumu la kulinda maliasili zetu ni la watanzania wote

Kwa kweli ni lazima tumpongeze mchungaji Msigwa kwa kuanza kujitambua na kuwa mwanasiasa wa kweli.

Ni wakati sasa na makamanda wengine wakaacha kutmia viroba na kuanza kujitambua kama Mchungaji
.

Yamekuwa hayo tena Chilisosi
 
Rambi rambi za wajane wa mwangosi utarudisha lini?
Rudisha kwanza rambi rambi za wajane tutakuelewa!
 
Hili jamaa lina akili za kitoto sana..halafu halina heshima..watanzania inabidi tujifunze kujiheshimu na kuheshimu watu.. wengine sisi tunaosupport cdm ni watu na akili zetu..pengine hata wewe tumekuzidi kielimu, kiuelewa, kifedha nk..unapotuita wanywa viroba unakua ni ujinga na utoto.. Grow up
 
Aliyejitambua ni yule aliyepewa ushauri akaufanyia kazi..! Wewe una akili ndogo,unashauriwa na wenye akili kubwa,na unafanyia kazi! Yupi kajitambua sasa hapo! Ni sawa na dent umemfundisha kafaulu na unampongeza,sasa yupi kajitambua hapo. Hongera sana Nyalandu a.k.a Jangiri
 
Binafsi nawapongeza wote, lakini sana pongezi ziende kwa msigwa! Naomba wizara zingine ziige mfano huu hasa wizara ya katiba na sheria, ifanyie kazi ushauri wa waziri kivuli wa katiba na sheria ili tupate katiba ya wananchi na sio ya vyama!
 
Fukuza huyo msaliti ameishaanza kununuliwa na CCM inakuwaje mpaka amsifu waziri wa CCM?Hivi huyu naye sio msaliti kweli?
 
Ndugu zanguni,

Leo, kwa mara ya kwanza tokea Chadema iundwe, mbunge wa kutokea Chadema amefurahishwa na kazi ya waziri wa chama tawala. Mheshimiwa Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa facebook ameandika haya

[h=5]Peter Msigwa[/h]about an hour ago near Iringa, Tanzania

Nampongeza waziri, Nyalandu ,kwa hatua aliyochukua ,na kuwa waziri wa kwanza kuchukua ushauri wa kutoka Upinzani . Kwenye maswala mhimu ya kulinda maliasili zetu. Namuomba asiishie hapo , ufanyike uchunguzi wa kina kwa makampuni yote ya uwindaji ili kuhakikisha .sheria ,taratibu na kanuni za uwindaji zinafuatwa.
Jukumu la kulinda maliasili zetu ni la watanzania wote

Kwa kweli ni lazima tumpongeze mchungaji Msigwa kwa kuanza kujitambua na kuwa mwanasiasa wa kweli.

Ni wakati sasa na makamanda wengine wakaacha kutmia viroba na kuanza kujitambua kama Mchungaji.

Wabunge wa upinzani wengi walishajitambua na hawana sababu za kujitia uzuzu ispokuwa kwa mkono wa bepari mjamaa, Hata CCM pia wengi wanajitambua ila wanajitia uzuzu kwa kulinda matumbo yao na matibabu ya nje ya nchi.
Siku zote tunachotaka wananchi ni mali zetu zitunzwe na tunufaike nazo bila kujali mchukua hatua ni CCM au Upinzani. Rejea kauli ya Nyalandu bungeni alivyopuuza swala hili kwa kujibu kebehi eti wawindaji wote wametimiza vigezo ndio maana wakapewa kazi hizo. Leo tumeshuhudia sheria zetu zikishika hatam ambacho ndio kiu yetu. Serikali sasa ifanye hivyo Kwa Majina aliyonayo jk ya wauza unga, IPTL, ESCROW ACOUNT, Kampuni za Madini,
bidhaa feki, Wabadhirifu ofisi za umma, Wala rushwa akiwemo vijisent, Fedha za Uswiss na zinginezo, watoe utaratibu wa kurithishana madaraka n.k. Wananchi tutawapongeza kila kukicha na kuwaongeza muda wa kutuongoza. Tumechoshwa na kauli kama hii tena bungeni kwa vigogo kuuza unga "Tukianza kutajana hapa hakuna atakaebaki" . Hakuna wa kupongeza kauli hii ispokuwa mateja.
 
isije kuwa wanatumia viroba kwa kuwa uwezo wao unaishia hapo, manake bia ishavuka 2000 sehemusehemu, wakati kiroba unakunywa hata ukiwa na mia 700. Dompo ya dodoma 13,000. Makamanda hela ya namna hiyo wanayo?

na wewe unahitaji kujitambua
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza kufuta vitalu vyote vilivyokuwa chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd kutokana na kukiuka sheria za uwindaji nchini, huku akiifuta Idara ya Wanyamapori.

Uamuzi huo wa Serikali, umekuja siku chache baada ya Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuonyesha video inayoihusisha kampuni hiyo na ukiukaji wa sheria na taratibu za uwindaji.

Awali, Msigwa ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa madai hayo Mei 14, mwaka huu wakati wa uwasilishwaji wa bajeti ya wizara hiyo mjini Dodoma.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Nyalandu pia alitangaza kuifuta Idara ya Wanyamapori na kuunda Mamlaka ya Wanyamapori ili kuimarisha ufanisi katika sekta hiyo.

“Kufuatia tuhuma zilizowasilishwa bungeni kwa njia ya ushahidi wa DVD na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Peter Msigwa Mei 14, 2014… Kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 17(1) na 8(2), Nafuta umiliki wa vitalu vyote vilivyo chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd,” alisema Waziri Nyalandu. Alivitaja vitalu hivyo kuwa ni Lake Natron GC East, Gonabis/ Kidunda- WMA na MKI- Selous.

“Hatua hii pia inafuta vibali vyote vya uwindaji vilivyotolewa katika msimu huu wa uwindaji. Hii iwe onyo kwa kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kwa ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu za uwindaji,” alisema Nyalandu.

Aliongeza, baada ya kupata tuhuma hizo aliiagiza Idara ya Wanyamapori kufuatilia na kumhoji Mkurugenzi wa Kampuni ya GreenMiles Safaris Ltd, ndipo walipobaini makosa ya kampuni hiyo.

Aliyataja makosa hayo yaliyokiuka Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya 2009 kuwa ni pamoja na wageni wa kampuni kuwinda wanyama wasioruhusiwa wakiwemo nyani na ndege kinyume na kifungu cha 19 (1 na 2) na kuchezea watoto wa pundamilia na ngiri kinyume na kifungu cha 19 (1).

“Kufukuza wanyamapori kwa magari na kisha kuwapiga risasi wakiwa ndani ya magari kinyume cha sheria,” alisema Nyalandu.

Back
Top Bottom