Nyalandu ahusishwa na Kampuni Inayotuhumiwa Kwa Ujangili

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Mambo mapya yameibuka Kuhusu kampuni ya kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helkopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani wake raia wa wingereza Ronger Gower.

FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd,Tanzania Game Trackers safari Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati Helkopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili. Kumbukumbu zilizopo Wizara ya maliasili na utalii zinaonesha kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni wa watuhumiwa wa ujangili.

Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ana uhusiano wa karibu na kampuni hizo na hata kwenye kampeni zake za kusaka urais na hatimaye ubunge, Nyalandu alitumia Helikopta ile iliyolipuliwa.

Chanzo: Jamhuri
 
Hiiiiii....sasa tafsiri yake ni nini hapa...
Wale wanaoshitakiwa kwa uuaji walimuua jangili...walikuwa kazini kuwind majangili ila wamegeuziwa kibao or what????!!!!! au mi ndio sielewi elewi...
Mimi nilijiuliza huyu Mwingereza alikuwa mlinzi wa mbuga zetu toka lini???? Chopa ilikuwa inafanya nini kwenye mbuga yetu? nikasema labda ni ulinzi wa wanyama pori kwa msaada wa watu wa UK...
 
Kwa mwendo huu sioni Tembo Tanzania miaka kumi ijayo.Ni huzuni
 
Hiiiiii....sasa tafsiri yake ni nini hapa...
Wale wanaoshitakiwa kwa uuaji walimuua jangili...walikuwa kazini kuwind majangili ila wamegeuziwa kibao or what????!!!!! au mi ndio sielewi elewi...
Mimi nilijiuliza huyu Mwingereza alikuwa mlinzi wa mbuga zetu toka lini???? Chopa ilikuwa inafanya nini kwenye mbuga yetu? nikasema labda ni ulinzi wa wanyama pori kwa msaada wa watu wa UK...

Ndivyo nami nimeelewa
 
Msifanye mchezo Katibu Mkuu wa Maliasili ni Meja Jenerali. Kumbe tunaleta mwanajeshi kupambana na majangiri wazawa ili tulete majangiri wazungu wenye kuzunguka mbugani na helkopta ili kuchagua tembo gani anafaa kama mfuga kuku anavyochagua kitoweo zizini
 
Huku ndio tulipokua tunapataka sio kuwapa mvua ya miaka 70 walio tungua helkopta wakati waratibu wao wapo mtaani wanapeta
 
Kwa mujibu wa jamuhuri waliotungua ni majangili na waliotunguliwa nao ni majangili,Ni kama hawakujuana na wa Helkopta walikuwa wakijificha kwenye kivuli cha ulinzi wa tembo.
yani majangili wa kizungu vifaa vinawarahisishia kazi yao.
 
Back
Top Bottom