Nyakahura Secondary School - msaada Contact Address

mlukosi

Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
53
Reaction score
20
Habari za leo jamani. ninahitaji msaada wa mawasiliano ya moja kwa moja wa shule ya Nyakahura Secondary. kijana wangu kachaguliwa huko.
 
Nyakahura unajua ilipo kwanza? kama kijana kasoma mjini sidhani kama mazingira ya huko yatakua rafiki kwa kujisome
 
Ingia kwenye website yake contacts utapata
 
Habari za leo jamani. ninahitaji msaada wa mawasiliano ya moja kwa moja wa shule ya Nyakahura Secondary. kijana wangu kachaguliwa huko.
Nyakahura ipo Mkoa wa Kagera.

Kwa kukusaidia, nimekuambatanishia na Joining Instructions ya Mwaka Jana. Naamini itakusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Maandalizi mema.
 
Attachments

Nyakahura unajua ilipo kwanza? kama kijana kasoma mjini sidhani kama mazingira ya huko yatakua rafiki kwa kujisome
Umekaririshwa nyambizi wewe!! Siku hizi pale kuna umeme full time, siyo enzi za wakimbizi wa Rwanda hizi! REA imefanya yake huko, kama Nyakanazi tu kwenyewe sasa pana umeme sembuse Nyakahura? Wacha kumtisha mtoto wa mwenzio. Hali ya hewa iko njema sana pale utafikri uko Rwanda vile!
 
nashukuru sana , form uloambatanisha imeniwezesha kumpata Head Teacher na kasema Joining instructions ni hadi wiki ijayo,,,,ingawa mabadiliko yakuwa kwenye gharama zaidi kwa ufupi....ahsanteni sana
 
Umekaririshwa nyambizi wewe!! Siku hizi pale kuna umeme full time, siyo enzi za wakimbizi wa Rwanda hizi! REA imefanya yake huko, kama Nyakanazi tu kwenyewe sasa pana umeme sembuse Nyakahura? Wacha kumtisha mtoto wa mwenzio. Hali ya hewa iko njema sana pale utafikri uko Rwanda vile!
Asante kwa kuniita nyambizi,uwe na siku njema .niko familiar na maeneo hayo,nilijaribu kuongea kitu ninachokifahamu.kuwa mstarabu hata kama mtu katoa comment inayokinzana na maono yako
 
Kaka achana nao usibishane sana
anayeijua NYAKAHURA vizuri hatothubutu kutoa ushauri wa kumpeleka mwanafunzi pale
ulichokitolea tahadhari mimi nakielewa sana kazi ni kwake kukubali ushauri wako au kuukataa
ila nyakahura si sehemu rafiki kwa mwanafunzi kuishi na kusoma NUKTA.
 
Ninatazama acsee results zao zinaridhisha.... Ttzo hasa hapo ni lipi!?
 
Achana na hao wagonjwa mkuu,, yamekaa kukariri kuishi mjini utafikri yenyewe yamezaliwa mjini!! Nyakahura mbona pazuri kwa kupiga shule?
 
Inaonyesha Tanzania hii ili uwe mjini ni lazima uwe Dar, yaani Nyakahura/ mzani pale ni bush????
 
Back
Top Bottom