nusura apoteze maisha kwa kunywa sumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nusura apoteze maisha kwa kunywa sumu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE Salome Khalifan [32] mkazi wa Mburahati, nusura apoteze maisha kwa kunywa sumu kwa kile alichodai ni kudhalilishwa na mumewe.
  Chanzo cha karibu cha habari hii kimedai kuwa, juzi jioni majira ya jioni Salome alimgundua mumewe kuwa alikuwa akimnyemelea kimapenzi binti ambaye walikuwa wakimlea nyumbani hapo ili awe mpenzi wake.

  Binti huyo jina kapuni[ 19] ni mtoto wa dada yake na Salome ambaye alimchukua kuishi nae nyumbani kwake baada ya wazazi wake kufariki.

  Imedaiwa kuwa binti huyo alifika nyumbani kwa Salome miaka mitano iliyopita mara baada ya kupoteza wazazi wake ambapo alikuwa akiishi mkoani Morogoro.

  Imedaiwa kuwa, mume wa Salome alikuwa akimsumbua binti huyo kumtaka kimapenzi na binti huyo alikuwa akigoma kwa kumuheshimu mama yake mdogo.

  Imedaiwa kuwa, awali mume huyo alipokuwa akimuhitaji binti huyo alimdokeza Salome lakini siku zote Salome alikuwa akimbishia binti huyo kwa kudai mume wake hawezi kufanya upuuzi huo.

  Hata hivyo imedaiwa kuwa mara kadhaa alivyokuwa akisumbuliwa na baba huyo, binti huyo alimtaarifu Salome ambaye alimkanya binti huyo asitoe taarifa kwa ndugu yoyote kuhusiana na hilo.

  Hata hivyo kadhia hiyo ilipozidi binti huyo aliripoti kwa mama yake mkubwa ili aweze kumchukua na kuondoka mahali hapo kwa kuwa baba huyo alikuwa akimsumbua na kumpa maneno makali na kumlazimisha.

  Imedaiwa kuwa juzi jioni Salome alimkuta mumewe akiwa ameketi Sebuleni akiwa anamshika sehemu za mwili binti huyo na kuamini alilokuwa akiambiwa na mwanae ni kweli tupu.

  Mara baada ya kurekodi tukio hilo mumewe alimuomba radhi na kudai walikuwa wakitaniana na binti huyo.

  Kutokana na aibu aliyoipata kwa mwanae mwanamke huyo alitoka nje na kuelekea dukani kwenda kununua sumu ili ajiue kwa kuwa aliona amedhalilishwa na mumewe.

  Imedaiwa kuwa mara baada ya kurudi na kufanikiwa kupata sumu ya kuulia wadudu aliingia ndani kwake na aliiandaa ili aweze kuinywa na ndipo alipokutwa na binti huyo na kumsihi asiendelee na zoezi hilo lakini alishidwa nguvu na ndipo binti huyo alitoka nje kutoa taarifa kwa majirani kuomba msaada na kuingia ndani humo na kukutwa alikunywa kidogo kati ya ile aliyoiandaa.

  Salome alipewa maziwa na kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa zahanati ya karibu kwa matibabu.
   
Loading...