Majighu2015
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,936
- 3,959

Imeelezwa kuwa nusu ya bidhaa mbalimbali zinazotumika nchini, zikiwamo dawa za binadamu na vifaa vya umeme, ni bandia.
Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe amesema hayo yamebainika katika utafiti alioufanya kuhusu tatizo la bidhaa feki nchini.
Akitoa matokeo ya awali ya utafiti huo uliodhaminiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Profesa Ngowi amesema kutokana na utafiti huo hali ilivyo mbaya kwa maisha ya binadamu.
Katika utafiti huo, aliwahoji watumiaji 250 wa bidhaa mbalimbali na waendeshaji wa kampuni 47 zinazotengeneza bidhaa mbalimbali nchini.
Source:Mwananchi.
Hii nchi kwa kweli ina hali mbaya..Almost kila kitu ni feki tu. Bidhaa feki,wabunge feki,viongozi feki,vyuo feki n.k Tunahitaji maombi mbadala.