Nusrat Hanje wa CHADEMA alistahili ubunge EALA

laki si pesa.

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
10,003
9,750
Wana jf.
Nimemfahamu kamanda Nusrat Hanje kwa muda mrefu ni mchapakazi, hodari, mfia chama,mwadilifu amekipigania chama kwa hali na mali pamoja na kukatwa jina kifitina kwenye ubunge wa viti maalum bado ameendelea kuwa mtiifu kwa CHADEMA.

Haiwezekani mtu kama Lawrence Masha amejiunga CHADEMA juzi tu muda wote aliokuwa CCM aliwanyanyasa sana upinzani leo anapewa ubunge lakini makamanda waliokipigania chama muda mrefu mpaka wengine kulala rumande wanatoswa .

Nusrat Hanje angeleta usawa wa kijinsia na kiimani ndani ya CHADEMA na kuondoa dhana ya ubaguzi unaohisiwa kuwepo na pia ingewasaidia sana CHADEMA kutoonekana imetekwa na makapi kutoka CCM huku makamanda waliokipigania chama muda mrefu kwa hali na mali kuwekwa kapuni huku genge la Lowasa likionekana kukiteka chama.
 
HANA ISHU HUYO NUSRAT HANJE. NI TAKATAKA TUUU, TUNAMJUA VYEMA JINSI ANAVYOTUMIKA
 
Out of nowhere utapataje mbunge wa EALA?
Makapi, maganda ya muwa ya jana nyie chungu mnaona kivuno.
Mtaendelea kuisoma namba.
Huko siko!
HUKU NDIKO.
[HASHTAG]#UsirudieKosa2020kupigiaKuraUpinzaniOvyo[/HASHTAG].
 
Kama CV yako haioneshi kama umewahi kupitia CCM then utasugua sana benchi mpaka gwanda litoboke kwa sasa.

Wenye chama wanaamini upinzani wa kweli utatoka CCM kama alivyonukuliwa Nyerere.

Vijana nendeni mkanenepeshe CV zenu CCM kwanza kigezo cha kulala selo siyo hoja kwa sasa hata mbu wanalala huko.

Mfano Bashe akihamia CDM leo hao kina Salum Mwalimu&Co wanawekwa benchi.
 
Mpaka tarehe ya leo hii,ukiondoa makada waliokuja na Lowassa ndani ya chama, hakuna damu mpya iliyochipuka from within.

Kiujumla, CHADEMA ina fail kitu kimoja mhimu sana kuliko pale zamani 2005-2010 enzi zile tulizoea kuona damu mpya ikiibuka na kupewa nafasi ndani ya chama. Siku hizi chama kinasubiri kuokota kapi na kulitumia juu kwa juu tofauti na ilivyopaswa kuwa.

Binafsi siuoni ukongwe wa hiki chama ikiwa hawathamini damu changa, hawathamini vijana waliojitolea kwa ari na mali kukipigania chama kuanzia ngazi ya shina pasipo kuwa na ofisi hadi kujulikana.

Viongozi wa juu wajitathimini upya. Kama kuanzishwa kwa chama kulikuwa ni kwa fikra huru kwaajili ya ukombozi wa Taifa, basi madaraka wanayo hodhi kwa sasa hayawafai tena. It is the time for them to step down make sioni mwelekeo zaidi ya kuishi kwa kutegemea kick za vuvuzela TL.
Kumbe ndiyo maana Mnyika haongei coz the man has just seen chama hakina muelekeo.
 
Wana jf.
Nimemfahamu kamanda Nusrat Hanje kwa muda mrefu ni mchapakazi, hodari, mfia chama,mwadilifu amekipigania chama kwa hali na mali pamoja na kukatwa jina kifitina kwenye ubunge wa viti maalum bado ameendelea kuwa mtiifu kwa CHADEMA.

Haiwezekani mtu kama Lawrence Masha amejiunga CHADEMA juzi tu muda wote aliokuwa CCM aliwanyanyasa sana upinzani leo anapewa ubunge lakini makamanda waliokipigania chama muda mrefu mpaka wengine kulala rumande wanatoswa .

Nusrat Hanje angeleta usawa wa kijinsia na kiimani ndani ya CHADEMA na kuondoa dhana ya ubaguzi unaohisiwa kuwepo na pia ingewasaidia sana CHADEMA kutoonekana imetekwa na makapi kutoka CCM huku makamanda waliokipigania chama muda mrefu kwa hali na mali kuwekwa kapuni huku genge la Lowasa likionekana kukiteka chama.
Anajua kiinglishi?
 
Kizungu kinapanda?
Kuwa kiongozi Tanzania unatakiwa kujua kusoma na kuandika,lakini kumbuka kiswahili kinatumika hadi UMOJA WA AFRIKA hivyo kizungu kwa ubunge wa A.mashariki sio hoja hapo.ila nikushauri tu mambo ya chadema waacheni waamue wenyewe kama ccm inavyo linda mikataba inayonyonya nchi yetu
 
Ndani ya CCM yamewashinda mko busy na nyumba ya jirani.Hata CCM aliyefaa zaidi ni ShyRose Bhanji
 
Kuwa kiongozi Tanzania unatakiwa kujua kusoma na kuandika,lakini kumbuka kiswahili kinatumika hadi UMOJA WA AFRIKA hivyo kizungu kwa ubunge wa A.mashariki sio hoja hapo.ila nikushauri tu mambo ya chadema waacheni waamue wenyewe kama ccm inavyo linda mikataba inayonyonya nchi yetu

Mbona umepagawa? Bunge la EALA huwa linaendeshwa kwa kiswahili au Kiingereza?
 
Kwani sifa za kuwa mbunge wa hilo bunge ni kuwa mfia chama? Hata Yesu alitoa mfano wa waliojiriwa asubuhi mchana na jioni na wote walikula dinari jipya lipi? Acha uchonganishi
 
Back
Top Bottom