Number hii ni ya tapeli 0678396045

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,051
2,106
Wakuu,

Hiyo number hapo juu inatumiwa na tapeli anachokifanya anakutumia text anakuambia am sorry naomba unipigie ukimpigia anajifanya eti ametumiwa number yako kimakosa na shangazi yake anazidi kukuambia eti alikua anasafiri toka Morogoro to Dar na wamefika sehemu inaitwa Bwawani na gari imeharibika hivo anaomba umsaidie sh elfu saba eti akifika Dar atakurudishia.

Mimi kanitumia hiyo text leo ni mara ya pili,mara ya kwanza ilikuwa tarehe 22 June nilivyompigia nikaona maelezo yake siyaelewi nikamkaushia,leo tena kanitumia txt kama ile ya mwanzo kumpigia maelezo anayotoa ni yaleyale ikabidi nimuambie aache wizi kaniporomoshea mvua ya matusi balaa.
 
Shukrani mkuu kwa 'kupuliza filimbi ya uamsho'.Ila sasa ni vyema ukaacha kukwepa kodi.Lipa kodi tumalizie barabara sita mpaka Msamvu.
 
Wakuu,

Hiyo number hapo juu inatumiwa na tapeli anachokifanya anakutumia text anakuambia am sorry naomba unipigie ukimpigia anajifanya eti ametumiwa number yako kimakosa na shangazi yake anazidi kukuambia eti alikua anasafiri toka Morogoro to Dar na wamefika sehemu inaitwa Bwawani na gari imeharibika hivo anaomba umsaidie sh elfu saba eti akifika Dar atakurudishia.

Mimi kanitumia hiyo text leo ni mara ya pili,mara ya kwanza ilikuwa tarehe 22 June nilivyompigia nikaona maelezo yake siyaelewi nikamkaushia,leo tena kanitumia txt kama ile ya mwanzo kumpigia maelezo anayotoa ni yaleyale ikabidi nimuambie aache wizi kaniporomoshea mvua ya matusi balaa.
hivi ww mtu atakwamnbia ntumie hela ntakurudishia nkifika wakati hata humjui,,omba omba wenyewe nawapitia mbali toka niwajue wengine chuma ulete wengine ndo kazi zao,,kuna mmoja posta toka nasoma ifm yupo na hata hazeeki sijui anakula nini,,,,mimi sim za aina hiyo au sms hazina jina kama mtu haeleweki nakata,,
 
Unaanzaje kutuma hela kwa mtu humjui? Labda uamue kumpa kama sadaka
 
Wapo wengi sana sasa hivi mi pia kuna mtu alijifanya yeye ni daktari hosptali ya mkoa moro yuko wodi ya uzazi labour. Amepata tatizo yuko mikumi simu yake yenye namba ninazozifahamu ina matatizo so anatumia laini nyingine ambayo Mimi sina...hivyo anahitaji nimtumie pesa akifika moro atanirudishia. Sbbu huyo Dr ninaheshiamiana naye na alimsaidia sana wife, kwenye uzazi sikutia shaka kumsaidia.!! Kumbe nimeingia chaka.!! Mwezi mmoja baadae namuuliza Dr suala hili anakataa katakata. Na kuwa hajasafiri nje ya moro kwa kipindi kirefu, na Mimi sio Mtu Wa kwanza kulalamika kwa jambo hili... Nitaitupia namba ya huyo mhusika humu soon.huyo anayejiita Dr.
 
Utapeli mwingine unaondelea sasa ni biashara ya mashuka ya kimasai nayo watu wengi sana wanalia.. Hasa wanawake, Mara nyingi mpiga simu, tapeli atajifanya yuko mikumi. Na kuna wazungu wanahitaji mashuka ya kimasai kwa bei nzuri aliyekuwa anawaletea mwanzo haeleweki hivyo kama unaweza wewe uchukue hiyo order fasta, na ili kukutoa shaka atakuunganisha na mtu ambaye atajifanya ana huo mzigo..!! Ukiingia mkenge tu watakwambia wanataka advance.!! Watakapokuwa wakiitambulisha hii biashara mwanzo hawakwambii unahitaji kuhusu malipo ya mwanzo ..!! Na wanakwambia ni biashara itakayo kupa kama milioni mbili au tatu chapchap.! Ukija stuka umeliwa....wote hawapatikani hewani... Tafadhari kuweni makini
 
Asante kwa taarifa mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom