Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,262
WATANZANIA WATANZANIA WATANZANIA
NIMECHOKA NIMECHOKA NIMECHOKA
NIMECHOKA NIMECHOKA NIMECHOKA
NIMENYONG'ONYEA VYA KUTOSHA, NIMESUBIRI VYA KUTOSHA, NIMEDANGANYWA VYA KUTOSHA, NIMEAHIDIWA VYA KUTOSHA, NIMECHOSHWA NA MICHOSHO YA VIONGOZI NA MAISHA DUNI YA WATANZANIA KWA UJUMLA. SAFARI HII NALIA KWA MAANDISHI KWANI SIKUBALI KUWA SOTE NI VILAZA, SI SOTE TUNARIDHIKA NA HALI ILIYOPO.....
NATAMANI KUONA NCHI YENYE MABARABARA BORA, NCHI YENYE RELI BORA, WANANCHI WALIOJAA MATUMAINI, HOSPITALI NA SHULE ZILIZO MARIDADI. NATAMANI KUONA JAMII YA WATU WAWAJIBIKAJI, NCHI YENYE WAFANYABIASHARA, WAKULIMA, WATAALAMU NA VIONGOZI WACHAPAKAZI, WAKUBWA KWA WADOGO WOTE WANAOFATA KANUNI NA SHERIA KATIKA MAZINGIRA YAO. JAMII YENYE MASHAUKU NA KUULIZA MASWALI KUJUA UKWELI, JAMII INAYOJIBIWA IKIULIZA, JAMII YENYE WATU WABUNIFU NA WATU WAJASIRI LAKINI PIA WATU WEMA NA WAUNGWANA.
Tanzania yetu, tutakuja kuona lini waziri, au walau basi naibu waziri anajiuzulu?! Iwapo kashfa ambazo mimi naamini kuwa ni kubwa kuliko zote katika nchi yetu (angalau katika kipindi cha miaka niliyo ishi na kujua yanayonizingira)zinajitokeza na kuzimika kimya kimya bila ya kuona wahusika wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria au wao kuachia ngazi kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Kashfa kama IPTL, RICHMOND, BoT, BUZWAGI na nyinginezo kadhalika bila kusahau hii mpya kabisa, ya MUHIMBILI NA UPASUAJI/UUAJI; zote naona zinapita au zitapita na kudaiwa zimechunguzwa au zinaendelea kuchunguzwa bila kuona wahusika tuliowapatia dhamana ya kutuongoza katika nyanja mbalimbali wanawajibika kwa kujiuzulu au basi kusimamishwa kazi mara moja.
Kweli sisi wagumu hivyo kujiuzulu? Au huku ni kutojua tu maadili ya uongozi bora, kusahu kanuni za uongozi? Au basi, jamii imeharibika na kuota sugu kiasi kuwa si wananchi wala viongozi wetu tu ambao hawaoni makosa, bali jamii nzima... sielewi kwa kweli. Tunaiga mengi kutoka jamii nyinginezo huko nga'ambo; kwanini basi tusiige hili la uwajibikaji pale tukoseapo ambalo mimi kinamna fulani ndilo naona limewawezesha wao kupiga hatua moja, mbili, tatu mbele zaidi ya sisi..
Angalia, mashirika ya umma mangapi yamepukutika puchukupuchu kabla ya baadhi yake kunasuliwa na PSRC?! Kuanzia UDA, TIPA, URAFIKI, TRC, Air Tanzania, n.k. yote haya yalikuwa yanajiendesha angalau kama huduma ya jamii tu pale ambapo hayakuthamini faida zaidi au kufanya vizuri. Ila kutokana na rushwa, uzembe na ubunifu duni, yameangamia mbele ya macho yetu bila kuona hata mkurugenzi mmoja anafikishwa mbele ya chombo cha dola...
Aibu kweli kweli, wakurugenzi wamekula bila kusaza na kwenda kujipatia ukurugenzi pahala pengine au hapo hapo katika kampuni iliyo nunuliwa na "wawekezaji" kwa hela mbuzi, eti tu kuwa shirika halikuweza kujinasua au kujiongoza lenyewe kwa kutegemea ruzuku za serikali.... nini kilicholifikisha shirika hilo katika hali kama hiyo kama si wizi na uzembe?! Unajua nini, ngoja ni thubutu tu kusema....WAKAMATENI WAKURUGENZI WOTE WALIO PELEKEA MASHIRIKA YA UMMA KUFIRISIKA, WAHOJINI UTAJIRI WAO NA WANAOPATIKANA NA HATIA MALI ZAO ZITAIFISHWE MARA MOJA.
Sasa hii ni nini kama si jamii ya vilaza?!..Jamii iliyozubaa kwa kukaa kimya wakati viongozi wao wakinena na kunukuu beti za ahadi kila kukicha kwenye majukwaa na kwa mashauku yasiyo aibu katika kusubiria kupandwa vichwa kutokana na vigelegele vya watu wasio matumaini bali vilio vinavyopasika kama vigelegele? Viongozi wanaopenda kuamrisha bila kutafakari wasemayo wala kutoa mifano. Viongozi wanao taja matatizo, na kuyakemea bila kuonyesha au kutamka mbinu za kuyamudu na kuyatokomeza. Jamii yenye viongozi waliojaa utawala wa imla bila kutafakari kwa makini wasemayo yana mantiki gani katika jamii kwa sasa, kesho na mbeleni.
ZIFUATAZO NI NAKALA KUTOKA KWENYE MAGAZETI HAPA TANZANIA, AMBAZO UKISOMA NA KUTAFAKARI UTAONA NI JINSI GANI NCHI YETU INAVYO HITAJI KUCHOCHEA MAPAMBANO YA KIFIKRA NA KIVITENDO ILI NCHI YETU IPATE KUSONGA MBELE BADALA YA KUDUMAA NA HIVYO KUONEKANA INARUDI NYUMA, MAANA WENZETU HATA WALIOPIGANA VITA MIAKA MICHACHE TU ILIYOPITA WATATUPITA AU WAMESHATUPITA (sidhani kama unahitaji fizikia ya kidato cha pili kuelewa hili..) :
Most 2006/07 purchases in public institutions improper`
2007-09-14 08:57:20
By Felister Peter
Seventy-one per cent of all purchases in public institutions in 2006/07 were incorrect, and did not comply with the regulations of the Public Purchase Act of 2004.
Speaking to reporters in Dar es Salaam on Wednesday, the Chief Executive Officer of the Public Procurement Regulatory Authority, Dr Ramadhan Mlinga attributed lack of knowledge on the purchasing Act as a contributing factor to incorrect procurements.
`This is the first investigation to be carried out since PPRA`s establishment in May 2005. We began with 20 public institutions and now intend to conduct inspection to another 20 public institutions between September and December this year`, said Dr. Mlinga.
Dr. Mlinga said PPRA plans to inspect 75 institutions in the financial year 2007/08, making the total number of institutions inspected reach 115 by the end of next year.
He said in the course of investigations, it was revealed that most institutions failed to comply with regulations on preparations of the annual purchasing programme by 35 per cent, and announcing tender results by 12 per cent.
It was also revealed that institutions failed to comply with requirement to have enough time to prepare tenders by 36 per cent.
PPRA found that there was no public institution that gave priority to local companies to win their tenders.
Dr. Mlinga reassured that the goal of PPRA is to conduct investigations in public institutions to understand problem areas in purchasing and see how they can be improved.
But overall, Dr. Mlinga observed that there was a need to educate officials in public institutions on regulations of the national Public Purchases Act of 2004.
SOURCE: Guardian
Asilimia 39 ya manunuzi ya taasisi za umma hayafuati utaratibu
2007-09-13 16:12:48
Na ITV Habari
Mamlaka ya udhibiti na ukaguzi wa manunuzi ya umma- ppra, imefanya ukaguzi wa shughuli za manunuzi kwa taasisi 20 za umma na kubaini kuwa asilimia 39 ya manunuzi yanayofanywa na taasisi hizo hayafuati taratibu zilizowekwa.
Akitangaza matokeo ya ukaguzi huo jijini Dar es Salaam afisa mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo dk. Ramadhani Mlinga, amesema kufuatia matokeo hayo, wameweka mkakati wa kuboresha hali ya manunuzi ya umma kwa kutoa mafuzo kwa asasi zisizofanya vizuri.
SOURCE: ITV
Kulingana na habari hapo juu, sijui nikisema kuwa karibu asilimia 60 za bajeti ya matumizi ya offisi za serikali zinaishia kuibiwa nitakuwa nafanya makosa kweli?! Iwapo asilimia 71 hazitumiki ipasavyo...
Ajali za magari zaua watu 2,838
2007-11-20 10:11:54
Na Futuna Seleman
Watu 2,838 wamefariki kwa ajali za magari huku 15,855 wakiwa wamejeruhiwa kwa mwaka uliopita. Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nchi Kavu na Majini nchini,lililo chini ya Mamlaka ya huduma za usafirishaji wa nchi kavu na majini (SUMATRA) Bw. Oscar Kikoye jijini Dar es Salaam.
Bw. Kikoye alikuwa akizungumza ikiwa ni maadhimisho ya kuwakumbuka Watanzania walioathirika na kufa katika matukio ya ajali za barabarani.
Maadhimisho hayo yalifanyika ofisini kwake kwa kuwasha mishumaa ikiwa ni mara ya kwanza tangu Baraza hilo lilipoanzishwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Bw. Oscar, kuanzishwa kwa baraza hilo kunafuatia kikao cha Umoja wa Mataifa (UN) kilichofanyika Oktoba 2005 na kuamua kwamba siku hiyo iadhimishwe kila wiki ya tatu ya mwezi Novemba kwa nchi zote duniani.
Halikadhalika, Katibu wa Chama cha Kutetea Abiria Wanaotumia Daladala hapa nchini, Robert Muhangwa alisema kuwa siku hiyo ni ya muhimu katika jamii, kwani abiria anatakiwa kujua haki zake za msingi katika suala zima la utumiaji wa vyombo vya usafirishaji.
Wadau wakitoa elimu kwa abiria, watakuwa makini kwa kutambua haki zao za msingi, elimu ambayo kimsingi itolewe na serikali kwa kushirikiana na wadau,
alisema Bw. Muhangwa.
Alisema kuwa, ukosefu wa elimu kwa wananchi kujua haki zao, hupelekea madereva kuzidi kuendesha mwendo wa kasi kwa vile wananchi hawajui majukumu yao katika kuwadhibiti madereva hao.
SOURCE: Nipashe
Muumba Aturehemu; sheria zisizofuatwa mabarabarani kutokana na uzembe, ubishi na ujinga; magari yaliyojaza kupita vipimo kutokana na uhaba wa usafiri, mabarabara finyu kutokana na ubunifu duni na umasikini;... nini kingine kinasababisha hizi ajali, labda nimesahau moja au mawili hivi, nisaidie kuyatambua....
Halafu basi, angalia mambo ya kiimla hapa chini...
Biashara zilizofungwa kwa nyasi, majani marufuku
2007-07-20 10:41:22
Na Grace Chilongola, PST
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, imewapiga marufuku wafanyabiashara kuingiza kwenye masoko bidhaa mbalimbali zikiwa zimefungwa kwa nyasi, majani, pumba, matawi ya miti au migomba, kwa sababu huchafua mazingira.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa PST jana, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. John Lubuva, alisema kuanzia Jumapili ijayo wafanyabiashara hawatakiwi kuingiza bidhaa zao kwenye masoko zikiwa zimezungushiwa takataka hizo.
Bw. Lubuva aliwataka wazalishaji, wafanyabiashara na madalali wa mazao ya chakula, kuacha kuingiza bidhaa zao kwenye masoko zikiwa na majani.
Alisema sheria ndogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya mwaka 2001 ya kudhibiti na ukusanyaji wa taka, inawakataza kuingiza bidhaa katika masoko, zikiwa zimefungwa na nyasi, majani na pumba.
Alisema wafanyabishara watakaokadi onyo hilo, watachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kufikishwa mahakamani kuanzia Julai 22, mwaka huu.
Alisema onyo hilo analitoa kwa mara ya pili, kufuatia onyo alilolitoa awali kupuuzwa na wafanyabiashara hao.
Alisema majani, pumba, nyasi, matawi ya miti, yamekuwa yakisababisha uchafu na kuongeza wingi wa taka katika masoko.
Hivi karibuni Manispaa ya Ilala ilianzisha kampeni ya kusafisha masoko kila siku ya Jumamosi, ambapo iliwataka wananchi kununua bidhaa zao mapema kwani ifikapo saa 8:00 mchana, masoko hufungwa na shughuli za usafi kuendelea.
SOURCE: Nipashe
--adha waliyoipata watu katika maeneo hayo hadi kufikia kutolewa kwa onyo kwa mara ya pili inaweza kufikirika tu, lakini ninahuhakika ni adha ya hali ya juu.
--hata hivyo, lazima niulize; je, kwanini onyo la kwanza lilipuuziwa? utekelezaji wa onyo hilo ulikuwa dhaifu au haukuwa na nyenzo za kutekelezea? Kabla ya onyo la pili kutolewa, je uchunguzi ulifanyika kuona kwanini onyo la kwanza limeshindikana?
--je, nyenzo gani wafanyabiashara waliwekewa ili kuhalalisha tamko la onyo la kwanza kisha la pili? Walijengewa viwanja vya magunia vipya? Walionyeshwa jinsi ya kuozesha nyasi au pumba kama wanatumia? Je, walionyeshwa kitu gani badala ya nyasi, pumba au matawi ambavyo wangeweza kutumia bila hivyo navyo kuharibu mazingira pia?
Labda hizi habari zinaandika kishabiki, lakini maswali mengi yanajitokeza katika kusoma hiyo moja hapo juu, kunakuwepo na haja kubwa ya kuhoji jinsi viongozi wetu wanavyofikiria kabla ya kukemea au kutoa onyo.
Lowassa akemea uchomaji misitu ovyo
HabariLeo; Saturday,November 24, 2007 @00:01
WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, amekemea tabia ya wananchi wa Rukwa kuchoma misitu na ameziagiza mamlaka za mkoa huo kuwashughulikia wote watakaobainika kufanya hivyo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kubaini kukithiri kwa uchomaji moto misitu katika maeneo mengi alimopita wakati wa ziara yake ya siku nne mkoani humo.
Sasa nauliza, hili ni tambiko gani la kuchoma moto?" aliuliza Waziri Mkuu wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela.
Wakati akiwa uwanjani hapo, Lowassa alishuhudia chanzo cha maji katika milima ya Mbizi kikichomwa moto na akawataka wananchi wajionee namna wanavyoharibu mazingira hivyo kuathiri pia upatikanaji wa maji.
Ndugu zangu wana Rukwa, nawaomba kwa dhati, nilidhani mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuchoma moto, kumbe nyie mnaongoza, alisema Waziri Mkuu.
Katika maeneo yote alipopita, Waziri Mkuu alizungumzia suala la uchomaji moto misitu na kuonya kuwa endapo vitendo hivyo vitaendelea, wananchi watakosa pa kuishi na akawauliza wataenda kuishi wapi.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Naibu Waziri ya Mambo ya Ndani, Lawrance Masha na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ludovick Mwananzila
Source: Habari Leo.
Cheo ni dhamana...
Lowassa: Marufuku mifugo kuingizwa bonde ziwa Rukwa
Basil Msongo, Sumbawanga
HabariLeo; Saturday,November 24, 2007 @00:05
WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, amepiga marufuku kuingizwa kwa mifugo katika bonde la ziwa Rukwa na wakati wowote kuanzia leo atamwagiza Waziri wa Kilimo aende kulitazama bonde hilo kuona namna linavyoweza kutumika kwa kilimo.
Ameagiza mamlaka za mkoa huo zisiwabughudhi wafugaji ambao tayari wana mifugo katika bonde hilo, lakini wasiruhusu mifugo mingine kuingia.
Lowassa aliyasema hayo alipozungumza na wakazi wa kata ya Msinda wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne iliyoanza Jumanne wiki hii.
Aliwaeleza wakazi wa eneo hilo lililopo chini ya mlima Muze, kuwa bonde lao ni zuri, lina rutuba ya kutosha na zao lolote linaweza kustawi hapo, hivyo lazima litumike kwa kilimo chenye tija.
Kwa mujibu wa Lowassa, endapo bonde hilo litatumika vizuri kwa ajili ya kilimo linaweza kuulisha mkoa huo wote, Iringa na Mbeya hivyo haoni sababu ya kutolitumia kikamilifu.
Lowassa alitoa changamoto kwa Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya kutumia uzoefu, umaarufu na uwezo wake wa ujasiriamali kuona namna bonde hilo linavyoweza kutumika kwa ukamilifu kwa kilimo cha kisasa.
Alisema bonde hilo lina maji ya kutosha, hivyo kila kitu kinastawi hivyo akamuagiza pia Mzindakaya na viongozi wengine wa eneo hilo wapitie mpango wa Taifa wa kuendeleza kilimo kuona namna wanavyoweza kulitumia kwa ukamilifu kuongeza tija katika kilimo.
Kabla ya kuzungumza na wananchi hao, Waziri Mkuu alifungua josho la mifugo la kijiji cha Mfinga lililojengwa kwa gharama ya Sh milioni 17.
Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha wafugaji na wazalishaji mali wa Mfinga, Nathani Kisusi, alimweleza Waziri Mkuu kuwa josho hilo limejengwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maisha bora na kuongeza kipato kupitia sekta ya mifugo.
Lengo kuu la ujenzi wa josho la Mfinga ni kuzuia vifo vya mifugo vinavyosababishwa na magonjwa yanayoenezwa na kupe. Asilimia 75 ya vifo vya ndama katika kata ya Mpito na Mfinga vinasababishwa na magonjwa yanayoenezwa na kupe, alisema Kisusi.
Wanaushirika hao waliishukuru serikali kwa kuwapatia dawa ya kuogeshea mifugo ya ruzuku, lakini walisema bei bado ni kubwa kwa wafugaji walio wengi kwa kuwa lita moja ya dawa hiyo wanauziwa kwa Sh 34,500.
Source: HabariLeo
'Top Down management approach' inaweza kufanya kazi kama inatekelezeka ipasavyo. Lasivyo inapotumika katika mfumo wa jamii kimakosa makosa huonekana kama 'jamii hiyo ni ya kijeshi' au darasa fulani hivi kwenye shule yenye msimamo wa udikteta.
Viongozi wanapokurupuka au kujiandaa na kutoa maonyo au kukemea fikra na matendo wasiyoafiki au yasiyo afikika katika jamii zao ni bora wafanye hivyo kistaarab na kiuungwana kwa kuonyesha mifano bora na mbinu za kutatua matatizo hayo. Kukemea au kuamuru tu hakutoshi. Kwani wao pia kama wananchi na watu tuliowapatia dhamana kwa kutuomba kuwapigia kura au kuwachagua ili kutuongoza, tunaweza pia kuwakemea pale tunapoona mahitaji yetu muhimu hayatimiliki mwaka nenda rudi.
Yaani pale tunapoona ahadi za hospitali, mashule na walimu hazitimiliki. Ahadi za mabarabara zinazidi kusogezwa mbele na chaguzi zinapokuja wanatuahidi yale yale tena... Hapo basi tunabidi kuwakemea kama vile wao watukemeavyo, na ndipo 'top down' management approach inapogeuka kuwa 'bottom up' ghafla... labda ujiulize, katika mfumo uliojijenga wa top-down, je hili linakubalika?! Hapa ngoja tu nirudie tena usemi wa wahenga wetu kuwa, 'mkuki kwa nguruwe...'
Amtaka Waziri ashughulikie matatizo sekondari Kantalamba
HabariLeo; Saturday,November 24, 2007 @00:03
WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, juzi alimwamuru Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ludovick Mwananzila, asishiriki kwenye ziara aliyoifanya jana asubuhi mjini Sumbawanga, aende katika shule ya sekondari ya Kantalamba kushughulikia matatizo kati ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Alitoa agizo hilo katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga baada ya mmoja ya wanafunzi wa Kantalamba kumweleza kuwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita hawana mwalimu hata mmoja, hivyo wanachofanya ni kuseremua yaani kukariri tu.
Mwanafunzi huyo, Prosper Kanyombo pia alimweleza Lowassa kuwa wanalishwa chakula kibaya, hivyo kuathiri afya zao.
Waziri Mkuu alimwita Mkuu wa Shule hiyo atoe maelezo, lakini hakuwapo uwanjani hapo hivyo akamtaka Mwananzila ajibu tuhuma hizo hapo hapo uwanjani, hali iliyosababisha wananchi waliokuwapo uwanjani hapo kushangilia wakiwamo wanafunzi wa shule hiyo.
Mwananzila alikiri kuwapo kwa upungufu wa walimu katika shule hiyo, lakini akasema kuna walimu sita wa vidato vya tano na sita kati ya walimu 39 waliopo shulemi hapo.
Alisema walimu ni wachache kwa kuwa baadhi ya wanaopangiwa kufundisha Rukwa huenda katika mikoa mingine na kwamba, mfuko wa kutoa hamasa kwa watumishi uitwao Mfuko wa Mwalimu Nyerere umesaidia kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
Naibu Waziri alikiri pia kwa wanafunzi hao wamekuwa wakila chakula kibaya kwa kuwa ndicho kilichokuwa kikipatikana kwa kuwa waliokuwa wakipeleka chakula katika shule hiyo na shule nyingine walikuwa hawajalipwa fedha zao.
Mwananzila alisema Oktoba 10 mwaka huu serikali ilianza kuwalipa wafanyabiashara hao, hivyo wanafunzi hao wataanza kupata chakula kizuri.
Alimuagiza mkuu wa shule hiyo akae na walimu na wanafunzi wakubaliane chakula gani wanapenda kula ili wasome vizuri.
Source: HabariLeo.
Nimechoka nimechoka nimechoka, kwani naamini kabisa kuwa Tanzania yetu si nchi yenye vilaza wote, pamoja na kuwa baadhi yetu wanaweza kuwa. Tanzania yetu si nchi ya viongozi wenye imla na kukurupuka kwani baadhi ya viongozi wetu wanaonyesha umaridadi, utanashati na uwajibikaji unaozingatia kanuni zote na maadili ya uongozi.
Tatizo, kukaa kwetu kimya na upole wetu, muungano na undugu wetu, amani na utulivu wetu unafanywa uwe chombo cha kutuangusha badala ya kuwa nyenzo madhubuti ili kutuhamasisha na kutuendeleza. Kibaya zaidi ni kuwa, mfumo wa maisha yetu, kama vile mazingira ya kijamii, uchumi, sheria na siasa zetu umejijengea mizizi na kutufanya sisi sote tuamini kuwa hatuwezi kubadilika na kuleta mapinduzi ya kifikra na vitendo katika kuiendeleza nchi yetu. Kingine kilichojiotea mizizi na cha kusikitisha ni kuwa kuhoji viongozi wetu ni kukosa maadili na kukiuka tamaduni zetu.
MUNGU IBARIKI NCHI YETU TANZANIA NA BARA LETU AFRIKA. AMINA!
SteveD.