simonrajab
Member
- Jan 15, 2022
- 48
- 17
"Tumeweza kuishauri serikali kufungua kituo cha kimataifa hapa nchini kwajili ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara (Tanzania International Arbitration Centre) ili kuepukana na adha ya kwenda nje kutatua migogoro kwani ni gharama kubwa".
"TLS imekuwa ikitoa msaada wa kisheria bure kwa Wananchi ambao hawana pesa ya kupata huduma ya kisheria, ili kuwawezesha wananchi kupata haki na stahili zao".
"Moja ya mambo yanayotizamiwa ni suala la katiba mpya TLS, tunashiriki kikamilifu katika kikosi kazi kilichoundwa kukusanya maoni na nyaraka zitakazosaidia kutoa dira ya namna gani tunakwenda katika mchakato wa katiba mpya".
"Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wangu TLS imeweza kushauri zile sheria kandamizi kuondolewa au kurekebishwa ili kuimarisha misingi ya utoaji haki nchini kwa maslahi mapana ya wananchi na ustawi wa Taifa letu"
"Ndani ya Mwaka mmoja wa uongozi wangu ndani ya TLS tumejitahidi kujenga mahusiano mazuri kati ya mihimili ya kiserikali na Mawakili ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakihisi tofauti"
"Uongozi wa TLS kwa kushirikiana na Serikali tumeweza kupunguza gharama za bima ya Afya kwa Mawakili kutoka Milioni 1 hadi laki Tano"
"Kipindi cha nyuma kulikuwa na ongezeko kubwa la Mawakili feki (vishoka) lakini kwasasa tunakwenda kudhibiti hilo kwani mnamo tarehe 22 Mwezi huu(May) kwenye mkutano wa wanasheria tunakwenda kuzindua mihuri ya moto (Digital stamps) kwajili ya kuzuia mihuri na Mawakili feki mtaani"