NUKUU ZA LEO; By Malisa GJ,

NUKUU ZA LEO; By Malisa GJ,

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,141
Reaction score
96,171
NUKUU ZA LEO;

By Malisa GJ,

1. “Madaraka hulevya, lakini madaraka makubwa hulevya chakari.” Lord Acton.

2. "Binadamu wote ni sawa, lakini baadhi ya binadamu wana usawa zaidi kuliko wengine" George Orwell.

3. "Sayansi haisemi uongo, lakini uongo unaweza kusemwa kwa sayansi" Richard Feynman.

4. "Jifanye kama mtu mwenye nguvu unapokuwa dhaifu, na jifanye dhaifu unapokuwa na nguvu" Sun Tzu.

5. "Sheria mbovu huundwa kutokana na hofu ya watawala kupoteza mamlaka" Sarah Vowell.

6. "Wanaoweza kukufanya uamini upuuzi, wanaweza pia kukufanya utende ukatili." Voltaire.

7. "Tofauti ya busara na upumbavu ni kwamba, mtu mwenye busara anaweza kujifunza kwenye swali la mpumbavu lakini mpumbavu hawezi kujifunza kwenye jibu la mwenye busara." Bruce Lee.

8. “Siasa ni sanaa ya kufanya watu waamini kuwa wanashiriki maamuzi lakini kumbe tayari yalishafanywa.” Noam Chomsky.

9. “Demokrasia ni mfumo ambao watu huchagua nani awadanganye kwa miaka michache ijayo." George Shaw.

10. “Mtu akipoteza uwezo wake wa kuuliza maswali, tayari ameshapoteza uhuru wake.” Arundhati Roy.

11. "Uongozi si cheo, bali uwezo wa kuhimili lawama bila kupoteza mwelekeo. Mtu anayeshindwa kuhimili lawama hafai kuwa kiongozi" John Maxwell.

12. "Uongo ni silaha ya kwanza ya dikteta, na ukimya ni silaha ya mwisho ya raia. Dikteta haogopi kelele za raia bali ukimya wao" Isaac Asimov.

13. "Wakati wa giza, hata mshumaa mdogo huonekana kama jua." Desmond Tutu

14. Tofauti kati ya akili na hekima ni kwamba, akili ni kujua nini cha kusema, hekima ni kujua lini useme na wapi pa kusemea." Confucius.

15. “Thamani ya juu kabisa ya uhuru ni uwezo wa raia kuhoji mamlaka. Kama unaogopa kuhoji, basi ujue bado upo kwenye ukoloni.” Carl Sagan.

Dressed by Mapero-suit
 
Madaraka katika uongozi hayapiganiwi kama vita bali huja yenyewe!

Ogopa sana yule anayeyagombania madaraka kwa udi na uvumba,kwani huyo ni hatari iliyo kuu .

Uongozi siyo vita ya jihadi,bali uongozi hutoka kwa mungu.

Wala usimuonee wivu yule anayefaidika kwa uongozi kwani muda ni mfupi na ulimwengu huu hauna raha wala maana yoyote!

Ulimwengu umeumbwa kwa mfumo wa balansi,kwa mzani wa ajabu katika ulinganyo hasi na chanya,hukupata leo,katukuu katapata tena kwa urahisi wa ajabu.
#mansa mussa!
 
NUKUU ZA LEO;

By Malisa GJ,

1. “Madaraka hulevya, lakini madaraka makubwa hulevya chakari.” Lord Acton.

2. "Binadamu wote ni sawa, lakini baadhi ya binadamu wana usawa zaidi kuliko wengine" George Orwell.

3. "Sayansi haisemi uongo, lakini uongo unaweza kusemwa kwa sayansi" Richard Feynman.

4. "Jifanye kama mtu mwenye nguvu unapokuwa dhaifu, na jifanye dhaifu unapokuwa na nguvu" Sun Tzu.

5. "Sheria mbovu huundwa kutokana na hofu ya watawala kupoteza mamlaka" Sarah Vowell.

6. "Wanaoweza kukufanya uamini upuuzi, wanaweza pia kukufanya utende ukatili." Voltaire.

7. "Tofauti ya busara na upumbavu ni kwamba, mtu mwenye busara anaweza kujifunza kwenye swali la mpumbavu lakini mpumbavu hawezi kujifunza kwenye jibu la mwenye busara." Bruce Lee.

8. “Siasa ni sanaa ya kufanya watu waamini kuwa wanashiriki maamuzi lakini kumbe tayari yalishafanywa.” Noam Chomsky.

9. “Demokrasia ni mfumo ambao watu huchagua nani awadanganye kwa miaka michache ijayo." George Shaw.

10. “Mtu akipoteza uwezo wake wa kuuliza maswali, tayari ameshapoteza uhuru wake.” Arundhati Roy.

11. "Uongozi si cheo, bali uwezo wa kuhimili lawama bila kupoteza mwelekeo. Mtu anayeshindwa kuhimili lawama hafai kuwa kiongozi" John Maxwell.

12. "Uongo ni silaha ya kwanza ya dikteta, na ukimya ni silaha ya mwisho ya raia. Dikteta haogopi kelele za raia bali ukimya wao" Isaac Asimov.

13. "Wakati wa giza, hata mshumaa mdogo huonekana kama jua." Desmond Tutu

14. Tofauti kati ya akili na hekima ni kwamba, akili ni kujua nini cha kusema, hekima ni kujua lini useme na wapi pa kusemea." Confucius.

15. “Thamani ya juu kabisa ya uhuru ni uwezo wa raia kuhoji mamlaka. Kama unaogopa kuhoji, basi ujue bado upo kwenye ukoloni.” Carl Sagan.

Dressed by Mapero-suit
Umenukuu Nukuu zenye Philosophy za kiwango ambacho wote tungeziishi Taifa letu lingefikia kilele cha matamanio,matarajio na mafanikio tunayostahili siyo tunayopewa au kuletewa.
Sadly,CCM wanaamini kuwa wanachowaza/wanachofanya ndiyo mwisho wa miisho kama Chura Kisimani.
 
Nukuu zimekaa poa sana. Hakika zitaishi milele na milele.
 
Back
Top Bottom