Inaelekea wachangiaji wengi wana nia ya kupotosha mada, nadhani mleta mada anachosema kama Dr Ulimboka alifanyiwa attempt ya kuuawa, hilo ni kosa la jinai, sasa yeye mwenyewe aliyetendewa jinai hiyo anatoa clues, ambazo siku zote ndiyo polisi huwa wanasisitiza kutaka ushirikiano huo toka kwa raia wema. Sasa hapa swala la msingi ni kwa nini polisi hawataki kuzifanyia kazi taarifa za mtu aliyekumbwa na dhahama hiyo, na kumtia mbaroni huyo mtuhumiwa ili imhoji??!! Badala yake wamemng'ang'ania yule chizi wa Kova, ambaye naye ameomba ifanyike parade ya kipolisi,ili aitwe Ulimboka, amtambue mtuhumiwa wake, je ni kwa nini na hili Polisi haawataki kulifanya??!! Kweli nimeamini nchi hii inaendeshwa kwa staili ya kimazingaombwe!!