Nukuu juu ya chama

May 6, 2019
5
15
“Kazi ya chama cha siasa kilicho imara ni kuwa kama daraja la kuwaunganisha watu na Serikali waliyoichagua, na kuiunganisha Serikali na watu inayotaka kuwahudumia. Ni wajibu wa Chama kuwasaidia watu kuelewa Serikali yao inafanya nini na kwa nini; ni wajibu wake kusaidia watu kushirikiana na Serikali yao kwa juhudi ya pamoja ili kuundosha umaskini ambao umetuelemea. Na ni wajibu wa Chama pia kuhakikisha kwamba Serikali inaendelea kuyajua sana maoni, shida na matakwa ya watu. Ni wajibu wake kuwasemea watu. Pia ni wajibu wake kuwaelimisha watu na kuwasaidia kuona shughuli za Serikali zina maana gani kuhusu usalama wao wenyewe wa siku zijazo na fursa zao wenyewe za siku zijazo”.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
Mkutano Mkuu wa Chama cha Uganda People’s Congress (UPC)
Tarehe 7 Juni 1968.
De Informer: GUBE 9GB

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom