Nukushi ya JK. Nyerere: Onyo kwa magamba, changamoto kwa magwanda

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,857
1,936
Maana ukweli ni huu: Kwamba chama sicho chombo cha Serikali. Serikali ndicho chombo ambacho Chama hujaribu kutekeleza matakwa ya watu na kuyahudumia masilaha yao. Kwa hivyo ni wajibu wa chama kuamua misingi mikuu ambayo Serikali itaendeshea shughuli zake; ni wajibu wake kuamua siasa ambazo Serikali yake itazifuata. Bila shaka, Chama hakiwezi kuwa badala ya Serikal; hakiwezi kufanya kazi iliyotafsiriwa ya kutunga sheria na kuzitekeleza, ambayo ni wajibu wa Serikari kuifanya.

Lakini Chama chenye mizizi yake katika mioyo ya watu tu, chenye wafanyakazi wenye ari vijijini na kwenye miji nchini mote-Chama cha namna hiyo ndicho tu kinachoweza kuiambia Serikali ni nini matilaba ya watu, na kama matilaba hayo yanatekelezwa kwa njia ya kuridhisha. Chama kama hicho ndicho kinachoweza kuhakikisha kwamba Serikali na watu wanashirikiana kutekeleza matilaba ya watu- People's Congress, tarehe 7 Juni, 1968.

My Take: Tukiwa tunaendelea kukijenga Chama chetu(CDM) kuelekea 2015 ni busara kuacha na kujiepusha na malumbano yanayochochewa na watu/ wanachama wasio na nia nzuri na chama chetu. kuana wanachama wanaibuka na kukishambulia chama wakitumia sababu zilezile za 'UDINI' na 'UKANDA' na nyinginezo nyingi. Ni muda wa Chama kuanza kuhakiki uhalali wa wanachama wake kimatendo na kimaadili.

Ni muda muafaka wa kuanza kujenga chama 'MJINI' na 'VIJIJINI' heko kwa makamanda wote walioko mstari wa mbele huko Shinyanga na Tanzania nzima. Na sisi hapa Mara tunaendelea kuwafikia wote walioko vijijini na katika wilaya ya Serengeti. Ni lazima tuwasemee wote wa mijini na vijijini na kuacha umbeya na uzandiki usiokuwa na maan tukielekea kupata katiba mpya.

Kwa magamba, fahamuni tu chama si Serikali, kumekuwa na kasumba ya kudhani ukiwa kiongozi wa magamba basi wewe ni kiongozi wa serikali. Wamekuwa wakiamuru polisi kupiga raia katika mikutano mbalimbali. Wengine wanakagua miradi ya maendeleo na hawana mamlaka ya kufanya hivyo kisheria.

Wanamagwanda tuwaunge mkono makamanda wote walio mstari wa mbele kujenga chama, ni lazima chama kijengwe sasa na si wakati mwingine. Ni lazima tujenge nchi yetu kwa kuwaelimisha wananchi juu ya haki zao za msingi na wajibu wao kwa taifa lao. Tuache majungu ya udini na ukanda na sijui nini....

Kama hutaki 'go and eat a coke'
 
Back
Top Bottom