Ntozi na "Big Agenda"Unastahili kipindi na Samia!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Tunaona waandishi wengi wakifanya Interview na Viongozi wetu mara nyingi nchini.

Lakini kuna mahali wanapwaya sana,pale wanaposhikwa na vigugumizi kuuliza maswali magumu.
kwa Viongozi wetu kuhusiana na hali halisi ya wakati kuendana na matarajio ya wananchi.

Kwa muda sasa Mtangazaji Aloyce nyanda wa Star TV na kipindi chake cha The Big Agenda.
Amejizolea umaarufu kutokana na jinsi anavyoendesha vipindi vyake kwa weledi.

Kupitia ukurasa huu nampendekeza #Aloycenyanda aandae mahojiano maalumu na mheshimiwa Rais wa JMT,
Samia Suluhu Hassan ikiwa ni moja ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja akiwa madarakani.
Tunatarajia atatimiza kiu ya Watanzania wengi kwa maswali yasiyo na woga bali yenye kutimiza majibu kwa wananchi.
Code:
 
ALOYCE NYANDA NA MASWALI MAGUMU,NA SALIM KIKEKE NA MASWALI NYANYA KWA MAMA SAMIA,

Nimeshangazwa na kinachoitwa mahijiano kati ya Mhe Samia suruhu hasana raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania na salim kikeke mwandishi nguli na mtangazaji wa BBC londani,kiukweli hayakuwa mahojiano,ulikuwa ni mzaha na porojo za kitoto kabisa,yaani ni bora umemsikiliza aloysi nyanda wa kipindi cha the big agenda,
 
Ki ukweli Salim kikeke anaonesha uwezo mdogo sana wa kuuliza maswali. Ni Kama huwa Hana maandalizi. Huwezi ona amenukuu sheria, hotuba au mlolongo furani wa mambo.

Pia anauliza maswali ambayo ni mepesi sana. Kingine anashindwa kuongoza mhojiwa wake. Hii hupelekea mhojiwa kujibu kadri atakavyo na kuchagua maswali. Hakika salim unaonesha viwango vya chini Sana. Hata Kama ni kuogopa au kujipendekeza huku kumezidi. Natamani hii nafasi angeipata zuhura yunus wa BBC ( achana na huyu wa ikulu) nahisi tu ngefaidi Sana.

Tasinia ya habari pia hapa kwetu ni majanga matupu. Pamoja na hayo doto blendus na odemba wako vizuri sana. Hawa kweli wanaweza kufanya maojiano ya kitaifa.
 
Tunaona waandishi wengi wakifanya Interview na Viongozi wetu mara nyingi nchini.

Lakini kuna mahali wanapwaya sana,pale wanaposhikwa na vigugumizi kuuliza maswali magumu.
kwa Viongozi wetu kuhusiana na hali halisi ya wakati kuendana na matarajio ya wananchi.

Kwa muda sasa Mtangazaji Aloyce nyanda wa Star TV na kipindi chake cha The Big Agenda.
Amejizolea umaarufu kutokana na jinsi anavyoendesha vipindi vyake kwa weledi.

Kupitia ukurasa huu nampendekeza #Aloycenyanda aandae mahojiano maalumu na mheshimiwa Rais wa JMT,
Samia Suluhu Hassan ikiwa ni moja ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja akiwa madarakani.
Tunatarajia atatimiza kiu ya Watanzania wengi kwa maswali yasiyo na woga bali yenye kutimiza majibu kwa wananchi.
Code:
Naunga Mkono Hoja...
P
 
Viongozi wa star tv Kama mko humu
Andaeni mahojiano na mh raisi kwenye mahojiano asimame aloyce nyanda / odemba
 
Back
Top Bottom