Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,670
Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF limetoa miezi miwili kwa waajiri zaidi ya 3,000 jijini Dar es Salaam, kuiwasilisha michango ya wafanyakazi wao mara moja, na watakaokiuka watafikishwa mahakamani.
Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, James Oigo ameeleza kuwa katika jiji la Dar es Salaam pekee, hadi kipindi cha mwezi Machi, waajiri 3,234 hawajawasilisha michango ya wafanyakazi wao yenye jumla ya shilingi Bilioni 21.4 kinyume cha sheria.
Amebainisha kuwa tayari shirika hilo limewasiliana na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Mahakama kwa ajili ya kuwachukulia hatua kali za kisheria waajiri hao.
Kwa mujibu wa sheria, ni kosa la jinai kwa mwajiri anaposhindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wake, kwani adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka miwili.