NSSF. NPF , PPF LAPF Tunataka zaidi ya Tower | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF. NPF , PPF LAPF Tunataka zaidi ya Tower

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zing, Jun 30, 2009.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Jamani sijui wenzangu mna mtazamo gani juu haya mashirika ya niliyoyataja hapo juu ne mengine kama hayo katika kuwawezesha wananchi.

  Binafsi naona mashirika haya kwa kiasi kikubwa hayawatendei haki wanachi ambao ndio wadau wakubwa na wachangiaji kwa kukatwa mishahara kila mwezi

  Cha kushangaza mashirika haya hayaweki msukumo wa kuwa na miradi amabyo inawelnga zaidi wadau wakubwa ambao wengi ni kipato cha kawaida.mashirika haya yaningia kwenye si tu miradi mikubwa bali ambayo haina manufaa kwa wanachi wa kawaida.

  Mashiriaka haya yanaangalia zaidi faida yao badala ya kuangalia faida gani wananchi wa kawaida wanapata.

  kipi chenye faida zaidi kwa jamii kati ya kujenga jengo kubwa ( Tower) ambazo zinapangishwa kwa biashara au kujenga nyumba ndogo ndogo na kuziuza kwa mikopo kwa wananchi?

  Mimi naona haya mashirika yaanaitakiw ayabadilishe mtazamo na ikiwezezekana serikali iyalazimishe yajenge nyumba kwa ajili ya makazi badal aya kwenda kwenye miradi yenye mtazamo wa faida zaidi na isiokuwa na faida kwa wanachi

  Nina uhakika mfanyakazi anayestaafu hawezi kufaidika na mfumo ulipo wa haya mashirikia zaidi ya kumdidimiza kwenye umasikini. kwani kwa thamani ya shilingi yetu inavyoshuka haya mafao hayana faida kabisa.

  Miji na vitongoji vitapangika na kupendeza zaidi kukiwa na uniform construction. Miji inayopendeza ya ulaya ni mfano mizuri wa miradi kama hii. Mfano ule mradi wa NHC wa nyumba za makazi tegeta ungetekelezwa kila mkoa na haya mashirika nadhani tungekuwa mbali kwa suala la mipango miji

  Changamoto natoa kwa haya mashirika yaachane na niradi maghorofa na badala yake yajaribu kuangali faida ya wadau zaidi kuliko faida zaid. Hii ni mifuko sio kampuni.

  Chanamoto nyingine kwa wadau walio tanzania ni tujaribu kujiuliza tutapokea shilingi npi kwa mwezi tukijalliwa kustaafu?

  Nawasilisha
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Waanze kutoa mikopo kwa wanachama na pia wapunguze miaka ya kuwa mwanachama wa kuduma kutoka miaka 10 hadi 5 kwani kuna kazi za mikataba pia.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Hivi unaelewa NSSF inavyo fanya kazi au basi tuu umeingia kuja kumwaa vitu?

  kuna namna nyingi ya kujua jinsi inavyofanya kazi na nadhani kwako first stop ingekuwa ni Parliament Act ya kuundwa kwa NSSF kisha baada ya hapo ndio ungeelewa hipi pesa zao zinavyokuwa invested badala ya kuingia humu na kuwka vitu bila ya kuwa na supporting data na statistics ku back up post yako

  -nawasilisha
   
 4. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hay ni mashirika ya kinyonyaji. Yanachua hela kwa wanachama na kufanya nazo biashara na faida inayopatikana hawagawani wawekezaji ambao ni wanachama wa haya mashirika. Inasikitisha baada ya hela yako kufanyia biashara kwa muda mrefu unachorudishiwa ni ile hela yako na interest ambayo ni kama 4%. Faida kubwa inayopatikana kutokana na investment ya hela zetu inakwenda wapi? Kama ulikuwa unafanya kazi miaka ya sabini na mshahara wako ulikuwa shs 1,200/- leo hii watakurudishia shs 240/- yako bila kuzingatia inflation iliyotokea hapa kati. It is a mare thieving
   
Loading...