NSSF Msijihusishe kwenye biashara ya Umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF Msijihusishe kwenye biashara ya Umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Oct 19, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  NSSF wana nia nzuri na ni kati ya taasisi zinazoongozwa vizuri kuliko zote Tanzania kwa mawazo yangu binafsi. NSSF ina viongozi waliofunguka kimawazo na wamaobadilika kutokana na wakati na bahati nzuri nimetokea kuwafahamu kwa ukaribu hawa viongozi.

  Ushauri wangu ni kwamba pamoja na mazuri mnayofanya NSSF msijiingize kwenye biashara ya Umeme tena kwasababu zifuatazo

  1. Matumizi ni makubwa sana: Matumizi ya kufanya biashara ya kufua mafuta kwa njia ya Gas yanaweza kufika $1 Billion hiki ni kiasi kikubwa sana kwa biashara ya umeme pekee. Vilevile kwa Fund yenu yenye $2 Billion ni karibu 50% ya fund nzima. Kuweka uzito mkubwa kiasi hiki kwenye biashara ambayo haieleweki vizuri hasa ukizingatia pesa za NSSF ni za wananchi si vizuri.

  2. Siasa: Umeme umekuwa na siasa sana hivyo viongozi wengi huko mbele watafanya mambo mengi ambayo ni ya kishabiki kufurahisha watu bila kujali hadhari za muda mrefu za huduma. Kama mfano bei serikali itakuwa na mkono mrefu kwenye bei ya kufua umeme. Wanasiasa wa serikalini hawana cha ku gain kuwasaidia nyie bali kuongoza ushabiki wa siasa.

  3. China na USA: Tanzania na East Africa kwa ujumla inapiganiwa na USA na China na vita imeanza rasmi Tanzania. USA Mfano ndiyo waliowaleta Symbion kutoka kwenye project ya kuweka umeme Afighanistan kuja Tanzania na wanataka kuwaleta GE ili walete Generators. Hizi kampuni hazilipwi na Goverment kama tunavyoambiwa bali zimehakikishiwa na USA kwamba watalipwa kwa njia ya Millinium fund na pesa kutoka kwenye budget la jeshi la Marekani. Balozi wa Marekani naye ni spy wa kijeshi na ni mwanajeshi msaafu. China nao wamekuja na mapigo kwa kutoa Mkopo wa $1 Billion kwa miaka 20 kwa rate ya 2% kwa mwaka au $60m ambayo ni ndogo sana.Wanajua atakaye control Tanzania ndiye atakaye Control Zambia, Kenya, Uganda, Congo, Rwanda, Burundi na hata Mozambique. Obama kapeleka wanajeshi 100 mwezi huu huko Uganda kupambana na waahasi lakini ukweli ni mafuta na yatapita Tanzania.

  4. NSSF Tunawahitaji: Tanzania inahitaji sana NSSF kwani Fund nyingine zimelega sana NSSF ndiyo wanaojenga mabweni ya vyuo, vyumba za polisi, nyumba za kukaa n.k. Mkitumia pesa nyingi kwenye miradi ya umeme hakuna pesa itakayobaki kwa maendeleo ya ujenzi.

  Pamoja na kwamba kuna wakati niliunga mkono hoja ya NSSF kuingia kwenye umeme sikujua watu wote na mapambano yaliyoko kwenye hili swala. Kwa manufaa ya nchi tunaomba achaneni na mambo ya umeme na rudini kwenye mambo mengine ya maendeleo.
   
 2. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  You said everything
   
 3. i

  ikhwan safaa Senior Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Niliyosema hapo juu ni muhimu NSSF wajenge Hospitali, vyuo na majengo lakini umeme utawashinda. Hauwezi kuwa na umeme wa gharama kama hivi huko mbele kwani utakuwa na kikwazo cha uchumi. Serikali itatafuta njia za kupunguza gharama za umeme na hizo hizo plan za Future Cash flow ambazo NSSF wanafikiria watapata hawatapata na pesa yao haitarudi kwani wametumia bei na gharama za sasa.
   
 5. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,221
  Trophy Points: 280
  Nyie ndio mnaotuletea nguzo zetu za umeme kutoka nje ya nchi!? Ole wenu na vizazi vyenu.
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Sasa ni kwanini NSSF ijiingine kwenye biashara za hasara Tanesco haina pesa!, corruption zimejaa Tanesco kwanini wasitumie pesa vizuri. Kuhusu nguzo hata kama ngunzo zinztoka nje za MCC Fund hizi pesa sio zetu ni za msaada. Wamarekani wanataka kila pesa ionekane imetumika vipi na Tanzania kila kitu hata nguzo ni lazima uonge kitu ambacho wenye kuendesha miradi hawawezi kufanya. Vilevile ukweli ni kwamba Tatizo la umeme haliwezi kutatuliwa na NSSF kwani ni tatizo kubwa sana na linahitaji pesa nyingi sana.NSSF ikiweka Generator zitakuwa za muda tu na si muda mrefu Tanesco watashidwa kulipa hizo Capacity charges ambazo ndiyo njia kuu ya rushwa.Kama NSSF inataka kusaidia ijenge Hospital za kisasa kwa mikoa kama Arusha, Tanga, Kighoma n.k
   
 7. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,221
  Trophy Points: 280
  Unataka kuniambia NSSF Kama private body haiwezi kujishughulisha na masuala ya kufua umeme ili kutuondoa Watanzania katika huu UOZO wa Tanesco !?

  Hapo kwenye bold, kwa hiyo na hizo hospitali za kisasa mpelekewe huko kaskazini tena!? Duuuh Aisee!
  Kuna mikoa mingi Tanzania inahitaji Maendeleo na hizo huduma muhimu kwa Wananchi.


  Unapozungumzia suala la nguzo, hata Kama pesa inatoka mbinguni kwani kuna ubaya gani wa hizo pesa kutumika kununua nguzo zilizopo hapa nchini ili kuongezea Wananchi kipato na kukuza uchumi wa Taifa letu!?
  Au ndio tunatumia akili za ndege Chichidodo!?
   
 8. bona

  bona JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  umeonge point mkuu, kwanza tanesco katika hali ya kawaida kama lingekua linaendeshwa kiufanisi lilitakiwa liwe shirika kubwa kuliko hata NSSF, tuanzie hapo, tanesco haliitaji mkopo wala msaada wa fund from outside kwa revenue inzaopata na preferential treatment(hakuna upinzani) iliyo nayo ilitakiwa liwe shirika kubwa sana ni ubabaishaji tu wa hapa na pale!!!
   
 9. f

  frank cain JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2012
  Joined: Dec 17, 2012
  Messages: 470
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1. hivi nssf waki-anguka mazma kwenye bishara zao tuhela twetu tutapataje? maana nijuavyo mim biashara yoyote inaweza ku-fail. 2. nssf wanapofikiria kuweka hela kwenye umeme wafikirie mbali zaid. waangalie the cheap option ya kutoa umeme leo na kesho. hii itasaidia kushindana na wafua umeme wengne. lasivyo inaweza kujikuta inagharamika zaid kufua umeme kuliko wengne na kupelekea akina sie kuuziwa umem ghali au itasusiwa na tanesco kwan wengne watakuwa wanazalisha umem cheap. lazma wafocus kesho. kesho i
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Watanzania wengi hawajui tatizo la umeme Tanzania lilivyo. Tatizo la umeme Tanzania ni $2B problem na haliwezi kutatuliwa bila kubadilisha mfumo wa Tanesco ilivyosasa. Hizi program za kununua Generators ni za muda mfupi kwasababu ya uhaba lakini Tanzania haina pesa ya kutatua tatizo hili kwa sasa. Tanzania inafanya vizuri lakini kwa pesa za mkopo wanajenga pipeline kutoka Mtwara kwa $1B tumekopa kutoka China na inabidi tuwaombe USA na Korea watusaidie Generators kutoka GE, Philips na Toshiba ili tupunguze kulipa hizi kampuni Capacity Charges za kijinga. Vilevile kampuni ya Tanesco inabidi inabidi igawanyike na kuwa kampuni tatu tofauti (1) Kampuni ya kuweka umeme (2) Kampuni ya kushughulikia Generation of power (1) Billing na Customer Servive. Sasa tunataka NSFF waingize $500M je watalipwa na Goverment ambayo haina pesa ya kuwapa Tenesco kwa sasa je NSSF wakidai na kampuni za binafsi nani atalipwa zaidi? je NSSF inaweza kupeleka serikali mahakamani kudai pesa? ukweli ni kwamba kama pesa haitoshi NSSF itakuwa yamwisho kulipwa vilevile hawawezi kutatua tatizo kubwa hivi!!!. Wafanye shughuli za kusaidia jamii kama medical insurance, hospitals, housing n.k
   
 11. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Katazo lako ama onyo ni la wazi na ukweli....NSSF wamekua waki-invest katika miradi mingi ya kiserikali kama chuo cha UDOM, Nyumba za polisi, daraja la kigamboni...hii ni miradi ya kisiasa na haina tija kwa wanachama wake..
  majuzi nimewasikia watu wa mamlaka ya mifuko ya jamii ati wana sema mifuko ipo katika hali nzuri ya kifedha na inaweza kujiendesha kwa miaka 50 bila ya michango!!!! hii sio kweli ...ukweli ni kuwa hii mifuko ipo kama pyramid schemes...wanachama wapya wana ongezeka wanaostaafu wachache ...kama mfuko watakosa wanachama wapya na hawa waliopo wajitoe ....hii mifuko itakufa....
  hebu tujiulize mwana chama anafaidika nini na daraja la kigamboni? au nyumba za polisi ambapo fedha zake kurejeshwa na serikali ni mtihani mkubwa
  ukweli kama mtu anawekeza kwenye savings account kila mwezi basi atapata faida kubwa atapo timiza miaka ya kustaafu..lakini nssf hakuna kitu..wanatumia fedha zetu ...katika siasa na hakuna faida kwetu
  faida ya taasisi kushikilia fedha zako kwa miaka 20 + ni kubwa....lakini nssf ukistaafu faida unayo pewa ni kiduchu sana
  masharti ya uwekezeji katika mifuko ya hifadhi dunia nzima inatakiwa uwekezaji katika property isizidi 10%.....na hairuhusiwi kuwekeza katika miundo mbinu ya nchiii...hili RAMADHAN DAU ANALIJUA..ILA AMEKUBALI KUTUMIWA TU KISIASA....
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2013
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  classic topic
   
Loading...